Mtuhumiwa Escrow, Harbinder Sethi akimbizwa Muhimbili

the deadline

Member
Joined
Sep 26, 2013
Posts
62
Reaction score
106
MG_0600.jpg

HATIMAYE mtuhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amepata ruhusa ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Ruhusa ya mtuhumiwa huyo kupelekwa Muhimbili umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Awali Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ilizuia mtuhumiwa huyo kwenda kutibiwa Muhimbili.

Hakimu Huruma Shahidi alipokea maelezo ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kwamba tayari Takukuru amepelekwa Muhimbili na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Viongozi wetu wajifunze kuheshimu na kulinda haki za watu na binadamu. Harbinder Singh Seth pamoja na ukubwa wa tuhuma zake lkn bado ni binadamu na hivyo anastahili kuthaminiwa na kuheahimiwa kama mwanadamu.

Sioni sababu ya suala la matibabu yake kuwa sehemu ya mabishano mahakamani.
 
Na afungwe pingu za kutosha mikono yote na miguu yote sio mwisho wa siku atoroke tuambiwe ooooh! Tulimfunga mkono mmoja kumbe mkono wenyewe bandia katoroka hatutawaelewa.
 
Tulia tu nahisi ndo yatakayotokea
 
Na afungwe pingu za kutosha mikono yote na miguu yote sio mwisho wa siku atoroke tuambiwe ooooh! Tulimfunga mkono mmoja kumbe mkono wenyewe bandia katoroka hatutawaelewa.
na kesi yenyewe mshtaki ashinde, tumechoka kushindwa
 
Ndiyo huyu wanasema ana puto tumboni?
Ana kijiti mkuu,sasa subiri ripoti ya daktari utaambiwa matatibabu yake ni nje ili apewe kibali tu na mahakama,atayeyukia canada huko ndiko pango la mafisadi na kuanza kufungua makesi
 
hivi watuhumiwa wa eskrow ni wawili tu!?...

wale wa Mkombozi benk wangeonganishwa na hii kesi maana na wao ni wanufaika na watuhumiwa wa kutakatisha pesa chafu....
 
Walitaka huyu Singh afariki ili ushahidi upotee. Huwezi kumyima mtu bila sababu hongera Mheshimiwa hakimu.
 
Huyu guru ni hatari kwa kutoroka na kufeki kila jambo, kumbuka alikamatiwa uwanja wa ndege akitaka kutoroka..hayo mandevu yenyewe ni ya kujifanya mcha mungu kumbe wezi yeye na mwenzake.
 
MG_0600.jpg

HATIMAYE mtuhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amepata ruhusa ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Ruhusa ya mtuhumiwa huyo kupelekwa Muhimbili umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Awali Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ilizuia mtuhumiwa huyo kwenda kutibiwa Muhimbili.

Hakimu Huruma Shahidi alipokea maelezo ya Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai kwamba tayari Takukuru amepelekwa Muhimbili na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Kwa nini amekamatwa?
Si zile tuliambiwa kuwa zilikuwa pesa za madafu na zilikuwa Mali yao ni kina lugemalila.
 
Back
Top Bottom