life coach
Senior Member
- Apr 11, 2017
- 121
- 401
Kuna nadharia nyingi ambazo zimekuwa zikieleza kuhusu asili ya binadamu.Kwa wakristo,Biblia imeeleza pia kuhusu asili au chimbuko la mwanadamu.
Biblia imeeleza jinsi mtu alivyopatikana tu,ila haikueleza jinsia ya mtu huyo.
Sasa kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana ambao unasema ya kuwa mtu wa kwanza kuumbwa (Adamu) alikuwa ni mwanaume.
Sijajua nadharia hii imetokea wapi au msingi wale au hata lengo lake ni nini,maana Biblia haikuwai kusema kwamba mtu huyo wakwanza kuumbwa ni mwanaume.
Andiko la biblia ambalo lilionesha uumbaji wa kwanza wa mtu ni " NA TUUMBE MTU KWA MFANO WETU"
Maelezo kuhusi jinsia yakafuata baadae bila kuonyesha kwamba wakwanza kuumbwa alikuwa na jinsia gani.
Nikiwa nafahamu ya kuwa kanuni ya uumbaji wa mungu ni wa vitu viwili viwili,mfano nuru na giza,usiku na mchana,mema na mabaya, mwanamke na mwanaume,ardhi na mbingu nk,nakuwa sina shaka kabisa ya kuwa mtu wa kwanza kuumbwa hakuna mwanaume.
Nawasilisha na baadhi ya mistari ya Biblia ambayo inasapoti maelezo yangu.
WanaJF naomba tusome na kuchambua kwa makini kwani lengo la uzi huu ni kupeana elimu.
Mwanzo 1:26-28
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; WAKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba MTU kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, MWANAUME na MWANAMKE ALIWAUMBA.
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 5:1_3
1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke ALIWAUMBA, akawabariki akawaita jina lao ADAMU, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
Karibuni.