Mtu mkubwa ana agenda ya kishetani; Watanzania tusijigawe

mkurugenzi wa mashtaka
mwanasheria mkuu
Majaji
Hawa wote hawawezi kuuhukumu mfumo maana ndio umewaweka hapo
 

Hiyo hoja ya katiba inaenda kujadiliwa kwenye bunge gani? Kumbuka kiongozi wa bunge ni mwenyekiti wa bunge, huyu ndio mwenye maamuzi hoja ipi iingie ndani ya bunge, na ukumbuke katibu wa bunge ni mteule wa rais asiyetaka katiba mpya. Unazungumza nadharia na sio uhalisia. Mwenye maamuzi na hilo bunge ni rais Magufuli, na anachotaka ndio kinajadiliwa bungeni, na asichokitaka hakijadiliwi.
 
Kuna muda niiwaona Wakenya ni wajinga na wapenda shari, kumbe sisi wa TZ ndiyo wajinga zaidi - unatawaliwa na mtu anayevunja katiba kwa makusudi kabisa afu unabakia kimya kwamba eti Mungu akusaidie - Mungu huwa hasaidii wajinga.
 
hizi ndo facts za kusema flan anaongea/anaandika sasa! tatzo letu kubwa ni kugeuza siasa/uongoz kuwa ajira. hivyo hata msomi anayetegemewa na wengi anajitoa faham za kuhubiri ukweli.
 
Muasisi wa haya haelewani na mke wake
 
Sijui nashindwa kutabiri mwisho wa hii safari ya visasi,itakuwaje kwa ustawi wa hili Taifa, ndio kwamba uchumi wetu itakuwa kwa kasi kwa kuwanyima wengine kuongea
 


Natamani hiki ulichoandika wakisikie wapinzani wote..
Shida tuna viongozi wanalalamila kila kukicha
 
Mchwa umeingia ndani ya Nyumba imara Jina Tanzania ulianzia kona moja inayoitwa mahakama ulipotafuna udongo wa kona hii ulipoona wenye nyumba wamelala usingiz wa pono na hawatafuti kuudhibit kwa dawa ya kuusupress ,ukaruka kwa furaha ukaingia kona ya Jina polici ,ulipoona huku nako wamelala wanakoroma ukacheza bamping kw style ya Aina yake,ukaenda kwenye kona ya Jina NEC. Ukauma weeee ukaona nako wameskia utamu..Sasa umeingia kona ya wenye nyumba wananchi .almaruufu kama Parliament huko sasa..unaruka na kukanyaga iwe ni vyombo vya kulia ama mashuka vyote vululuu Maweee eewe Tanzania yangu weeee!!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Huko ndiko tweshafika.
 
Huko ndiko tweshafika.
 
Mkuu mbona umeshikilia bango Wabunge wa viti maalum bila kuwajali ndugu zetu walio magerezani kisa uchaguzi?? Suala la Katiba siyo la Chadema wala ccm bali ni la Taifa. Kama wewe unaamini kuwa Katiba bora ni kwajili ya kuwawezesha Upinzani kushinda na siyo kwa maendeleo ya Taifa letu basi endelea kuwapigia chepuo Wabunge wa viti maalum.
 
Katiba mbovu
 
Since 2015 we are under Bahima empire note that .
 
Mkuu umeandika vizuri, Mimi nina marafiki wengi tu wa ccm, na makada wa kweli, nashukuru bado tuko vizuri japo nimewatangazia kuchukua KADI ya chadema maana sikuwai kua na chama,
Sasa tangu juzi wanaanza nitumia msg, kwamba nitafakari mahamuzi yangu
Sasa najiuliza kwani kuwa ndani ya chama mbadala na wakati lengo kuu ni moja kulitumikia taifa ni dhambi?
Nina wasi wasi wa kuwapoteza ndugu zangu Hawa na rafiki zangu Hawa, maana binafsi hua naamini kile moyo unaamini ,Sasa mfano ukifika nikaonekana na msimamo huu sijui ila haiwezi nibadilisha
 
mkurugenzi wa mashtaka
mwanasheria mkuu
Majaji
Hawa wote hawawezi kuuhukumu mfumo maana ndio umewaweka hapo
Unajua kwan nini UK mbali na mapungufu yake ipo 'stable'? Kumbuka inasemwa waziri Mkuu ndiye mtendaji lakini Malkia ndiye mwenye nguvu 'zisizoonekana' kwa macho ya wananchi na walimwengu katika uendeshaji wa serikali ya nchi hiyo. Ukitumia jicho la Tatu, utagundua nguvu kubwa (very strong 'shadow power') kupitiliza za Malkia si UK pekee hata baadhi ya nchi! Lakini, nchi ya UK ipo stable. Brexit, ilikuwa ni kurejesha mamlaka ya Malkia yaliyokuwa yanatikiswa na EU! Anayo mamlaka sasa !

Unafiki waweza kuwa na tija kwa wasiojielewa ama kwa wale waliokubuhu kwenye unafiki huo. Labda Tanzania 'tumeshindwa' kuwa wanafiki ! Unafiki unajenga imani kwenye 'malengo hewa'. Ukikubali unafiki, unakubali kuandaa matatizo lukuki ya kukuangamiza huko mbeleni. Nadhani tusipo kuwa wanafiki tutafika mbali katika kujitegemea kikweli kweli !!!

Isome vizuri post hii, mleta mada na wahusika wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…