Mtu mkubwa ana agenda ya kishetani; Watanzania tusijigawe

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
3,970
2,000
Zoezi la kutaka kuonyesha kama siasa ni vita na upinzani ni uadui limeshika kasi hapa nchini!

Uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye hili zoezi na wananchi na viongozi kwa ujumla wamejikuta wakiingia katika huu mtego bila kujua lengo la muasisi wa zoezi.

Watanzania wamefungamana sana;
1. Kifamilia.
2. Kidini
3. Kikabila
4. Kibiashara
5. Shuhuli za kijamii kama vile sherehe na misiba.

Ukitaka kuwagawa kwa kutumia siasa, utafanyaje kwenye mahusiano ya kifamilia, kidini, kikabila, kibiashara na shughuli za kijamii?

Leo chakula alichokua anakula Lema kimehamishiwa kwa Gambo kwa kutumia nguvu. Gambo mtaani ni jirani yangu na tunashirikiana nae pamoja na familia yake kwenye shughuli za kijamii. Lema ni shemeji yangu maana nimeoa kwao.

Sasa ukitaka kuonyesha Lema ni mtu mbaya sana na Gambo ni mtu mzuri sana, mimi nitasimamia upande gani? Makwazo ni budi kuwapo ila ole wake anayeyaleta. Yampasa kufungwa jiwe la kusagia shingoni mwake na atumbukizwe kwenye kina kirefu cha maji!

Ni muda sasa wa kutafakari lengo la muasisi huyu wa siasa za kibaguzi. Ilikuwaje tukaishi pamoja na kwa umoja na upendo chini ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete?

Nini kimeenda vibaya?

Tumefikaje hapa?
 
Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,455
2,000
Watanzania tuna haki ya kulaumiwa zaidi kuliko hata viongozi wetu;

Haya yote tumeruhusu sisi watanzania yatokee, tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "MTAZAMO WAKE" kuwa ndio mtazamo wa taifa zima. Hata kama mtazamo wake una madhaifu na si mzuri kwa ustawi wa taifa.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "CHUKI ZAKE" kuwa ndio chuki za taifa zima. Mtu akiwachukia watu fulani basi anataka taifa zima liaminishwe na liwachukie.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja "KUJIAMINISHA KWAMBA YEYE HAKOSEI" na yupo juu ya kila kitu mpaka Katiba ya nchi. Ana haki ya kuamua "NANI ANA HAKI YA KUISHI/NANI ANATAKIWA AFE".

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja awe na "KINGA YA KUTOKUULIZWA CHOCHOTE" atakachofanya au atakachoamua. Kana kwamba taifa hili "AMERITHISHWA KAMA MIRATHI" kutoka kwa ma babu zake ambao ndio lilikua mali yao.

Kwanini nasema sisi watanzania tuna kila sababu ya kulaumiwa?

Aliekuwa Rais Wa Indonesia, Suharto, aliiba sambamba na kufanya matumizi mabaya ya pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 15 mpaka USD $ Billioni 35.

Aliekuwa Rais Wa Philipines, Ferdinand Marcos, aliiba sambamba na kufanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 5 mpaka USD Billion 10.

Aliekua Rais Wa Zaire, Mobutu Sese Seko, na Aliekuwa Rais Wa Nigeria, Sani Abacha, walifanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wao USD $ Billion 5 kila mmoja.

Kashfa ya miaka ya hivi karibuni, nchini Brazil, iliopewa jina la "LAVA JATO" iliwa gharimu watu zaidi ya "11" wakiwemo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa duniani (Kutoka Brazil mpaka Peru). Na walifungwa.

Aliekuwa Waziri Mkuu Wa Malaysia, Najib Razak, ameshatakiwa na anafanyiwa uchunguzi wa ubadhirifu wa USD $ Billion 4.5 wakati wa madaraka yake. Pesa nyingine alitumia kumnunulia mke wake vito vya dhahabu na almasi za bei ya juu sana.

NB Wenzetu walifanya nini mpaka wakapatia, na sisi watanzania tunafanya nini mpaka tunakosea???

Rais Wa Peru, Pedro Pablo Kuzcynski, kutokana na kashfa ya Brazil nilio ainisha hapo juu alilazimika "KUJIUZULU" baada ya bunge la peru kuitisha kikao na kupiga "KURA YA PAMOJA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Iliitishwa na wabunge wa chama chake na upinzani pamoja.

Rais Wa Guatemala, alilazimika KUJIUZULU" baada ya bunge la nchi hio kumtolea "KINGA YAKE KIKATIBA", mchakato uliofanywa na chama chake na vyama vya upinzani.

Rais Wa South Africa, Jacob Zuma, alilazimika "KUJIUZULU" baada ya chama chake kumpa muda wa miezi 3 ajiuzulu au waitishe hoja bungeni ya "KUMPIGIA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Alijiuzulu kabla hata ya huo muda wa miezi mitatu kuisha. Sasa hivi ana kesi mahakamani za ufisadi.

Mnamo mwaka 2017, South Korea, walimtoa madarakani Rais wao Park Geun-Hye, kwaajili ya kashfa ya rushwa na kashfa za ubadhirifu. Mwaka 2018 alitiwa hatiani kwa makosa ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na vitisho (Alihukumiwa kifungo cha miaka 24).

Wenzetu kiongozi (Awe Rais au Waziri Mkuu) akifanya ubadhirifu/rushwa/kuvunja katiba/matumizi mabaya ya pesa za wananchi, basi hata kama ana mapembe au mkia, atatolewa kwa nguvu. Na mara nyingi viongozi hao wanatolewa madarakani kwa shinikizo/maamuzi ya "VYAMA VYAO WENYEWE" ili kulinda heshima ya chama kwa wanachama wao. Sisi wanasiasa pamoja na viongozi wa usalama wa nchi wanalilia uteuzi na tamaa ya kipato bila kujali taifa linaelekea wapi.
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,502
2,000
Tamaa ,kibri, ushamba, eti kishindo kwa garama ya kuharibu umoja na ustawi wa taifa letu.Hakuna mwenye furaha si yeye,wateule na hata raia.
 
MERCYCITY

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
761
1,000
Watanzania tuna haki ya kulaumiwa zaidi kuliko hata viongozi wetu;

Haya yote tumeruhusu sisi watanzania yatokee, tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "MTAZAMO WAKE" kuwa ndio mtazamo wa taifa zima. Hata kama mtazamo wake una madhaifu na si mzuri kwa ustawi wa taifa.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "CHUKI ZAKE" kuwa ndio chuki za taifa zima. Mtu akiwachukia watu fulani basi anataka taifa zima liaminishwe na liwachukie.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja "KUJIAMINISHA KWAMBA YEYE HAKOSEI" na yupo juu ya kila kitu mpaka Katiba ya nchi. Ana haki ya kuamua "NANI ANA HAKI YA KUISHI/NANI ANATAKIWA AFE".

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja awe na "KINGA YA KUTOKUULIZWA CHOCHOTE" atakachofanya au atakachoamua. Kana kwamba taifa hili "AMERITHISHWA KAMA MIRATHI" kutoka kwa ma babu zake ambao ndio lilikua mali yao.

Kwanini nasema sisi watanzania tuna kila sababu ya kulaumiwa?

Aliekuwa Rais Wa Indonesia, Suharto, aliiba sambamba na kufanya matumizi mabaya ya pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 15 mpaka USD $ Billioni 35.

Aliekuwa Rais Wa Philipines, Ferdinand Marcos, aliiba sambamba na kufanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 5 mpaka USD Billion 10.

Aliekua Rais Wa Zaire, Mobutu Sese Seko, na Aliekuwa Rais Wa Nigeria, Sani Abacha, walifanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wao USD $ Billion 5 kila mmoja.

Kashfa ya miaka ya hivi karibuni, nchini Brazil, iliopewa jina la "LAVA JATO" iliwa gharimu watu zaidi ya "11" wakiwemo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa duniani (Kutoka Brazil mpaka Peru). Na walifungwa.

Aliekuwa Waziri Mkuu Wa Malaysia, Najib Razak, ameshatakiwa na anafanyiwa uchunguzi wa ubadhirifu wa USD $ Billion 4.5 wakati wa madaraka yake. Pesa nyingine alitumia kumnunulia mke wake vito vya dhahabu na almasi za bei ya juu sana.

NB Wenzetu walifanya nini mpaka wakapatia, na sisi watanzania tunafanya nini mpaka tunakosea???

Rais Wa Peru, Pedro Pablo Kuzcynski, kutokana na kashfa ya Brazil nilio ainisha hapo juu alilazimika "KUJIUZULU" baada ya bunge la peru kuitisha kikao na kupiga "KURA YA PAMOJA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Iliitishwa na wabunge wa chama chake na upinzani pamoja.

Rais Wa Guatemala, alilazimika KUJIUZULU" baada ya bunge la nchi hio kumtolea "KINGA YAKE KIKATIBA", mchakato uliofanywa na chama chake na vyama vya upinzani.

Rais Wa South Africa, Jacob Zuma, alilazimika "KUJIUZULU" baada ya chama chake kumpa muda wa miezi 3 ajiuzulu au waitishe hoja bungeni ya "KUMPIGIA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Alijiuzulu kabla hata ya huo muda wa miezi mitatu kuisha. Sasa hivi ana kesi mahakamani za ufisadi.

Mnamo mwaka 2017, South Korea, walimtoa madarakani Rais wao Park Geun-Hye, kwaajili ya kashfa ya rushwa na kashfa za ubadhirifu. Mwaka 2018 alitiwa hatiani kwa makosa ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na vitisho (Alihukumiwa kifungo cha miaka 24).
Hongera kwa uchambuzi wako mzuri
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,171
2,000
Unashangaa Lema kupigwa Chini??

Kwani Yeye ndo mmiliki wa Wana Arusha

Yaani ushangae mtu kuondolewa madarakani Kupitia vyeo vya kuchaguliwa kwa Kura za wananchi kwamba wanamtaka Nani Kwa wakati huo siyo??

Punguzeni mahaba
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,171
2,000
Mwenye mahaba ni wewe usieona mapungufu ya uchafuzi uliofanyika
Utalalamika mpaka lini bila Kuchukua hatua?

Kwanza kabisa mnapaswa kukubali yaliyotokea ili SASA muanze kutazama uchaguzi ujao, kuna malalamiko ya Katiba, sjui tume huru n.k, muanze kushughurikia hayo na kuyapazia sauti Kwa nguvu zote

Sasa nyinyi mmekalia kulalamika utadhani kutabadirika chochote

Kitu kingine mlichofanya cha kijinga ni kukakataa kupeleka wabunge viti maalmu

Kinachowafanya mkatae kupeleka hakipo Ila ni Ujinga wa kususa usio na faida yoyote

Uchaguzi huu mmeuona mapungufu yake ni mengi na hakuna dawa ya kuyatibu, kinachopaswa ni watu wenye akili iliyo na Afya mkae, mfanye tathimini, na Naamini baada ya tathimini mtajiridhisha kwamba, kushindwa kwenu, kumesababisha vitu vingi, moja wapo ni tume isiyo huru, Katiba mbovu isiyozingatia matakwa na mahitaji ya sasa

Na mtakuja kugundua kuwa, kushindwa kwenu ni Kwa sababu ya vitu hivyo viwili na sio kupungua Kwa Kura

Na baada ya hapo, hakuna haja ya kuzira, muwekeze Kwenye kutafuta haki hizo
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,360
2,000
Unashangaa Lema kupigwa Chini??

Kwani Yeye ndo mmiliki wa Wana Arusha

Yaani ushangae mtu kuondolewa madarakani Kupitia vyeo vya kuchaguliwa kwa Kura za wananchi kwamba wanamtaka Nani Kwa wakati huo siyo??

Punguzeni mahaba

Kura za kwenye mabeg, na matokea ya mfukoni ya vyombo vya dola tumeyaona kwa macho yetu, usiwasingizie wananchi jambo ambalo hawajalitenda.
 
Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,598
2,000
Watanzania tuna haki ya kulaumiwa zaidi kuliko hata viongozi wetu;

Haya yote tumeruhusu sisi watanzania yatokee, tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "MTAZAMO WAKE" kuwa ndio mtazamo wa taifa zima. Hata kama mtazamo wake una madhaifu na si mzuri kwa ustawi wa taifa.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "CHUKI ZAKE" kuwa ndio chuki za taifa zima. Mtu akiwachukia watu fulani basi anataka taifa zima liaminishwe na liwachukie.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja "KUJIAMINISHA KWAMBA YEYE HAKOSEI" na yupo juu ya kila kitu mpaka Katiba ya nchi. Ana haki ya kuamua "NANI ANA HAKI YA KUISHI/NANI ANATAKIWA AFE".

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja awe na "KINGA YA KUTOKUULIZWA CHOCHOTE" atakachofanya au atakachoamua. Kana kwamba taifa hili "AMERITHISHWA KAMA MIRATHI" kutoka kwa ma babu zake ambao ndio lilikua mali yao.

Kwanini nasema sisi watanzania tuna kila sababu ya kulaumiwa?

Aliekuwa Rais Wa Indonesia, Suharto, aliiba sambamba na kufanya matumizi mabaya ya pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 15 mpaka USD $ Billioni 35.

Aliekuwa Rais Wa Philipines, Ferdinand Marcos, aliiba sambamba na kufanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 5 mpaka USD Billion 10.

Aliekua Rais Wa Zaire, Mobutu Sese Seko, na Aliekuwa Rais Wa Nigeria, Sani Abacha, walifanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wao USD $ Billion 5 kila mmoja.

Kashfa ya miaka ya hivi karibuni, nchini Brazil, iliopewa jina la "LAVA JATO" iliwa gharimu watu zaidi ya "11" wakiwemo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa duniani (Kutoka Brazil mpaka Peru). Na walifungwa.

Aliekuwa Waziri Mkuu Wa Malaysia, Najib Razak, ameshatakiwa na anafanyiwa uchunguzi wa ubadhirifu wa USD $ Billion 4.5 wakati wa madaraka yake. Pesa nyingine alitumia kumnunulia mke wake vito vya dhahabu na almasi za bei ya juu sana.

NB Wenzetu walifanya nini mpaka wakapatia, na sisi watanzania tunafanya nini mpaka tunakosea???

Rais Wa Peru, Pedro Pablo Kuzcynski, kutokana na kashfa ya Brazil nilio ainisha hapo juu alilazimika "KUJIUZULU" baada ya bunge la peru kuitisha kikao na kupiga "KURA YA PAMOJA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Iliitishwa na wabunge wa chama chake na upinzani pamoja.

Rais Wa Guatemala, alilazimika KUJIUZULU" baada ya bunge la nchi hio kumtolea "KINGA YAKE KIKATIBA", mchakato uliofanywa na chama chake na vyama vya upinzani.

Rais Wa South Africa, Jacob Zuma, alilazimika "KUJIUZULU" baada ya chama chake kumpa muda wa miezi 3 ajiuzulu au waitishe hoja bungeni ya "KUMPIGIA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Alijiuzulu kabla hata ya huo muda wa miezi mitatu kuisha. Sasa hivi ana kesi mahakamani za ufisadi.

Mnamo mwaka 2017, South Korea, walimtoa madarakani Rais wao Park Geun-Hye, kwaajili ya kashfa ya rushwa na kashfa za ubadhirifu. Mwaka 2018 alitiwa hatiani kwa makosa ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na vitisho (Alihukumiwa kifungo cha miaka 24).
Huko ni kwa binadamu lakini hapa kwetu mambo ni vululu vululu.Hakuna sheria wala Katiba inayozingatiwa kwa sasa ni kazi tuuuu.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,360
2,000
Utalalamika mpaka lini bila Kuchukua hatua?

Kwanza kabisa mnapaswa kukubali yaliyotokea ili SASA muanze kutazama uchaguzi ujao, kuna malalamiko ya Katiba, sjui tume huru n.k, muanze kushughurikia hayo na kuyapazia sauti Kwa nguvu zote

Sasa nyinyi mmekalia kulalamika utadhani kutabadirika chochote

Kitu kingine mlichofanya cha kijinga ni kukakataa kupeleka wabunge viti maalmu

Kinachowafanya mkatae kupeleka hakipo Ila ni Ujinga wa kususa usio na faida yoyote

Uchaguzi huu mmeuona mapungufu yake ni mengi na hakuna dawa ya kuyatibu, kinachopaswa ni watu wenye akili iliyo na Afya mkae, mfanye tathimini, na Naamini baada ya tathimini mtajiridhisha kwamba, kushindwa kwenu, kumesababisha vitu vingi, moja wapo ni tume isiyo huru, Katiba mbovu isiyozingatia matakwa na mahitaji ya sasa

Na mtakuja kugundua kuwa, kushindwa kwenu ni Kwa sababu ya vitu hivyo viwili na sio kupungua Kwa Kura

Na baada ya hapo, hakuna haja ya kuzira, muwekeze Kwenye kutafuta haki hizo

Kama ww unaamini katiba ina mapungufu na haiendani na wakati wa sasa, ww umefanya nini ili kuibadili? Huna uhalali wowote wa kumpangia mtu ajadili nini. Kama mtu akaamua kujadili uchaguzi ni haki yake, kama ww unaona unaweza kujadili yajayo ni haki yako pia.
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,171
2,000
Kura za kwenye mabeg, na matokea ya mfukoni ya vyombo vya dola tumeyaona kwa macho yetu, usiwasingizie wananchi jambo ambalo hawajalitenda.
Mkuu, Chadema haikuanguka Kwa kiasi kikubwa kama ilivyotokea na sio kwamba wananchi hawakuipigia kura, hapana

Chadema na Vyama vingi vya siasa, huwa vinaangushwa na Katiba mbovu pamoja na tume!!

Naamini kwa Hilo ndio imekuwa fimbo ya vyama pinzani kuadhibiwa,

Kama ni hivyo, Kwa maoni yangu, ni Chadema kukubali hili lililotokea na kesi ikawa ni Katiba na tume huru, na wabunge wa viti maalumu wakaruhusiwa kwenda, Kwa sababu Kilicho waadhibu Vyama pinzani sio uchache wa Kura Bali tume mbovu na Katiba yake, na badala yake vyama hivi kuanzia sasa vikajikita kudai Katiba na tume huru,
 
paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,171
2,000
Kama ww unaamini katiba ina mapungufu na haiendani na wakati wa sasa, ww umefanya nini ili kuibadili? Huna uhalali wowote wa kumpangia mtu ajadili nini. Kama mtu akaamua kujadili uchaguzi ni haki yake, kama ww unaona unaweza kujadili yajayo ni haki yako pia.
Sawa na sjamkatalia kuongea atakalo, Nami nimetoa maoni yangu juu ya kulalamika kusikokuwa na mwisho
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,326
2,000
Watanzania tuna haki ya kulaumiwa zaidi kuliko hata viongozi wetu;

Haya yote tumeruhusu sisi watanzania yatokee, tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "MTAZAMO WAKE" kuwa ndio mtazamo wa taifa zima. Hata kama mtazamo wake una madhaifu na si mzuri kwa ustawi wa taifa.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja kulazimisha "CHUKI ZAKE" kuwa ndio chuki za taifa zima. Mtu akiwachukia watu fulani basi anataka taifa zima liaminishwe na liwachukie.

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja "KUJIAMINISHA KWAMBA YEYE HAKOSEI" na yupo juu ya kila kitu mpaka Katiba ya nchi. Ana haki ya kuamua "NANI ANA HAKI YA KUISHI/NANI ANATAKIWA AFE".

Tunaruhusu mtu mkubwa mmoja awe na "KINGA YA KUTOKUULIZWA CHOCHOTE" atakachofanya au atakachoamua. Kana kwamba taifa hili "AMERITHISHWA KAMA MIRATHI" kutoka kwa ma babu zake ambao ndio lilikua mali yao.

Kwanini nasema sisi watanzania tuna kila sababu ya kulaumiwa?

Aliekuwa Rais Wa Indonesia, Suharto, aliiba sambamba na kufanya matumizi mabaya ya pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 15 mpaka USD $ Billioni 35.

Aliekuwa Rais Wa Philipines, Ferdinand Marcos, aliiba sambamba na kufanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wake kati ya USD $ Billion 5 mpaka USD Billion 10.

Aliekua Rais Wa Zaire, Mobutu Sese Seko, na Aliekuwa Rais Wa Nigeria, Sani Abacha, walifanya ubadhirifu wa pesa za wananchi wao USD $ Billion 5 kila mmoja.

Kashfa ya miaka ya hivi karibuni, nchini Brazil, iliopewa jina la "LAVA JATO" iliwa gharimu watu zaidi ya "11" wakiwemo wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara wakubwa duniani (Kutoka Brazil mpaka Peru). Na walifungwa.

Aliekuwa Waziri Mkuu Wa Malaysia, Najib Razak, ameshatakiwa na anafanyiwa uchunguzi wa ubadhirifu wa USD $ Billion 4.5 wakati wa madaraka yake. Pesa nyingine alitumia kumnunulia mke wake vito vya dhahabu na almasi za bei ya juu sana.

NB Wenzetu walifanya nini mpaka wakapatia, na sisi watanzania tunafanya nini mpaka tunakosea???

Rais Wa Peru, Pedro Pablo Kuzcynski, kutokana na kashfa ya Brazil nilio ainisha hapo juu alilazimika "KUJIUZULU" baada ya bunge la peru kuitisha kikao na kupiga "KURA YA PAMOJA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Iliitishwa na wabunge wa chama chake na upinzani pamoja.

Rais Wa Guatemala, alilazimika KUJIUZULU" baada ya bunge la nchi hio kumtolea "KINGA YAKE KIKATIBA", mchakato uliofanywa na chama chake na vyama vya upinzani.

Rais Wa South Africa, Jacob Zuma, alilazimika "KUJIUZULU" baada ya chama chake kumpa muda wa miezi 3 ajiuzulu au waitishe hoja bungeni ya "KUMPIGIA KURA YA KUTOKUA NA IMANI NAE". Alijiuzulu kabla hata ya huo muda wa miezi mitatu kuisha. Sasa hivi ana kesi mahakamani za ufisadi.

Mnamo mwaka 2017, South Korea, walimtoa madarakani Rais wao Park Geun-Hye, kwaajili ya kashfa ya rushwa na kashfa za ubadhirifu. Mwaka 2018 alitiwa hatiani kwa makosa ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na vitisho (Alihukumiwa kifungo cha miaka 24).
Umeongea ukweli mtupu!

Yupo mtu hapa nchini ambaye anajiona kuwa ana *capacity" sawasawa na Mungu!

Anavitumia vyombo vya dola kuwaadhibu viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani pasipo sababu yoyote ya msingi

Analolisema yeye ndiyo inakuwa ni sheria ya nchi..........

Analolitaka yeye ndiyo linakuwa........

Ni hatari sana kama Taifa, kuwa na mtu wa aina hii, ambaye haijali na kuisigina sigina hata Katiba ya nchi, ambayo ndiyo sheria mama, aliyoapa kuitii na kuiheshimu kabla hatujamkabidhi majukumu aliyo nayo hivi sasa
 
Chunda

Senior Member
Apr 7, 2016
180
250
Utalalamika mpaka lini bila Kuchukua hatua?

Kwanza kabisa mnapaswa kukubali yaliyotokea ili SASA muanze kutazama uchaguzi ujao, kuna malalamiko ya Katiba, sjui tume huru n.k, muanze kushughurikia hayo na kuyapazia sauti Kwa nguvu zote

Sasa nyinyi mmekalia kulalamika utadhani kutabadirika chochote

Kitu kingine mlichofanya cha kijinga ni kukakataa kupeleka wabunge viti maalmu

Kinachowafanya mkatae kupeleka hakipo Ila ni Ujinga wa kususa usio na faida yoyote

Uchaguzi huu mmeuona mapungufu yake ni mengi na hakuna dawa ya kuyatibu, kinachopaswa ni watu wenye akili iliyo na Afya mkae, mfanye tathimini, na Naamini baada ya tathimini mtajiridhisha kwamba, kushindwa kwenu, kumesababisha vitu vingi, moja wapo ni tume isiyo huru, Katiba mbovu isiyozingatia matakwa na mahitaji ya sasa

Na mtakuja kugundua kuwa, kushindwa kwenu ni Kwa sababu ya vitu hivyo viwili na sio kupungua Kwa Kura

Na baada ya hapo, hakuna haja ya kuzira, muwekeze Kwenye kutafuta haki hizo
Umeandika kama vile wewe halikuhusu na utakuwa salama sana. Uadui na chuki zinazosambazwa zinatuweka katika uhasama usiokuwa na sababu. Hivi mtu akiwa na mawazo tafauti na ya kwako ni adui yako? Maisha yanakuwa magumu kila kukicha, tatizo ni nini na je matatizo haya yanabagua kwa chama tawala na mwenye mawazo mbadala (mpinzani) ? Naona kuna shida mahali fulani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom