Wakuu, kama huwa mnasoma Gazeti la Raiamwema, ile sehemu ambayo Dada mmoja huwa anamwandika barua Mchumba wake Frank, huyo dada hua anajiita Hidaya, nadhani mtakuwa mnaelewa, wahusika wakuu kwenye hiyo makala ambayo hutoka kila wiki ni Waziri mmoja kwenye serikali ya mikiki, mke wa waziri huyo almaarufu kama MB, then kuna Hidaya mwenyewe na binti boss a.k.a BB, mara nyingi sana huyu BB htofautiana sana na baba yake ambaye ni waziri, mtizamo wake saa zote huwa umekaa ni CDM zaidi tu, ninahakika mwandishi wa makala hiyo ameisha fanya research ya kutosha kwenye hizo nyumba za wakubwa na kugundua mengi tu, ukweli watoto wengi wa wakubwa hawakubaliani kabisa na hali halisi ya jinsi magamba wanavyo endesha nchi, nina mfano 1, Kingunge mmoja wa usalama wa Taifa huwa na wakati mgumu sana nyumbani kwake, watoto wake wote incuding mke wake wote damu yao ni upinzani tu, hukia hatua watoto wanamwambia baba yao na kwamba wao ni vidole viwili tu, so please msimhukumu huyu dogo Wasira JR. hiyo ndio hali halisi wakuu, wengine hawawezi kuwa wanafiki, roho zinawauma, kuongelea/kusifikia kitu usicho kiamini, walio wengi hawawezi, maanake unakuwa kama mtumwa hivi, saa zote roho inakusuta!