Mtoto wa nje kaja kujitambulisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa nje kaja kujitambulisha!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 26, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hebu tuchukulie kwamba, ukiwa umekaa nyumbani kwako, anafika mgeni. Huyu mgeni ni mtoto wa miaka 10 hivi. Mkeo anamkaribisha na anaingia sebuleni ulipo.

  Anasalimia na baada ya salaam, mkeo anamuuliza shida yake. Kumbuka, mkeo ndiye aliyemkaribisha na kumuuliza maswali. Mtoto ni mtoto, kwani anasema wazi kwamba , ‘amekuja kwa baba yake' ambaye ni wewe.

  Ina maana wewe ndiwe baba yake! Hukuwa hata siku moja maishani mwako umefikiria kwamba, ulikuwa na mtoto wa nje. Ghafla anakuja huyu mtoto na kusema mbele ya mkeo kwamba ni mwanao.

  Hebu niambie, je ungekuwa ni wewe ungefanyaje?
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kama ulikuwa unafahamu kwamba una mtoto nje na hukuwa muwazi kwa mkeo, hilo litakuwa kosa kubwa sana kwa upande wako. Lakini kama ulikuwa huna habari na akaja mtoto, inabidi mmdadisi vema maana anaweza kuwa amekosea njia au nyumba.
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mtoto ni mtoto kama wa kwako mweleweshe mkeo ampokee,amlee kama wake!finished
   
 4. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Never leave any marks behind you if you are sure of not going back
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Mambo hayo ya kuanza ngono ukiwa darasa la tatu ndio yanayoleta yote haya
   
 6. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama ni wa kabla ya ndoa no problem. Wa baada ya ndoa kasheshe!
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,277
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Ngumu kumshawishi kuwa ulikuwa huna habari
   
Loading...