Mtoto wa mwanasiasa waziri alivyonitapeli

Mtoto wa mwanasiasa waziri alivyonitapeli

Elizaa

Senior Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
136
Reaction score
48
Hii ni story ya kweli imenitokea mimi mwenyewe.

Nimetapeliwa na mtoto wa mheshimiwa waziri wa serikali ya Tanzania, kijana huyu ambae alikuwa akinitafuta kwa kila njia mpaka kufika nyumbani kwangu, ambapo alinikosa na kuacha ujumbe wenye jina lake na no ya simu ya Assistant wake au Engineer wake. Kwasababu hili jina lilikua si geni kwangu nikaamua kumpigia kujua anachonitafutia ni nini.

Tulionana mlimani city siku iliyofuata nikiwa na mume wangu, Kijana alijieleza sana kwamba alikuwa anasoma chuo kikuu nje ya nchi, wiki mbili zilizopita ndio amerudi, akaamua kunitafuta. Anaamini naweza kumsaidia. Anataka niwe partner kwenye kampuni yake maana alieko nae amekosa kuwa mwaminifu. Kwamba huyu partner wake amekuwa anatumia vibaya pesa ambazo alikua anamtumia kwa ajili ya office wakati akiwa Masomoni.

Kwamba baada ya kutoka Masomoni amemuomba baba yake ampe nyumba, ambayo iliachwa na marehemu mama yake, huwa inakodishiwa kwa dola 3000$ ili awe anapata pesa za matumizi, lakini baba yake akakataa, Na kwa sababu hana jinsi yoyote ya kupata pesa ndio maana anataka niwe patner katika kampuni yake maana anaamini naweza kumsaidia kampuni yake iweze kupata pesa.

Nikamwambia siwezi kukujibu haraka maana mimi tayari nina kampuni yangu na bado ni changa na inafanya biashara tofauti kabisa na ambayo anafanya yeye. Nitaona kama naweza kukuunganisha na mtu yeyote ambae ataweza kukusaidia.

ITAENDELEA KESHO NITAWEKA PICHA NA MAJINA YAKE KAMILI SEHEMU YA MWISHO YA STORY
Kesho yake nikaongea na mkurugenzi wa shirika moja linalohusika na vijana, yule mkurugenzi akamkaribisha ili waongee aone atamsaidia vipi. Kijana akaja kwa mkurugenzi na mimi nilikuwepo ili kusikia atamueleza nini, Kijana akajieleza kwa huyo mkurugenzi jinsi alivyo na mipango ya maendeleo na anataka msaada wa ushauri maana tayari amefungua kampuni ya ulinzi na ya Intertainment nia yake kubwa ni kujenga matandao mkubwa kwa kuwa anategemea kuja kuwa kiongozi kama baba yake baada ya miaka kadhaa.

Mkurugenzi alimsikiliza kwa makini na akamuuliza anataka kusaidiwa nini? akasema jinsi ya kujikimu hapa mjini ili aweze kujipanga kwa kuwa ndio ametoka chuoni. Mkurugenzi akaahidi kumsaidia wakati miradi ya vijana itakapoanza.

Baada ya hapo kwa kuwa aliniambia hana nauli wakati akija nilitoa sh 10, 000/= nikampa kama nauli.

Akaondoka na sisi tukaondoka pamoja mume wangu, hatukuwasiliana mpaka baada ya wiki mbili aliponipigia akitaka kujua kama nipo Dar, nilikua safarini kikazi nikamwambia niko safarini, akataka kujua narudi lini, nikamwambia narudi baada ya wiki moja. Kwa kawaida huwa nafanya shughuli zangu na mume wangu kwa hiyo nikamuelezea mume wangu kuhusu hiyo simu niliyopokea.

Tuliporudi Dar baada ya siku moja akani sms, nikamuuliza unashida gani? akaniambia anaomba pesa kidogo ili aweze kufuatilia mambo ya kazi mjini, sikuona ni jambo la ajabu mtu kuomba msaada, kijana alionekana kuwa mkristo mlokole ambae ni mcha Mungu kweli kweli.

Kwa kuwa nilikua mitaa ya mwenge nikamwambia tukutane Mlimani city nikampa sh 20,000/= Wakati huo nilimuuliza utaishi vipi kwa kuomba na wewe ni mwanaume, si utafute kazi! akajibu ndio maana kila siku anaenda town ili kuona kama kampuni yake inaweza kupata pa kuanzia, Nikampa idea ambayo inaendana na biashara yake, akaifurahia sana na mara moja kuanza machakato wa kuanza kuifanyia kazi hiyo Idea. Ili kwa msaada zaidi nikamshauri amueite yule patner wake ili tuongee pamoja kama wataona Idea wanaweza kuifanyia kazi watakua wamepata pa kuanzia.

Zikapita siku kadhaa,Wakatupeleka kwenye office yao iliyoko Mbezi Park ambayo ipo mpaka sasa, Tukaona office iko sawa na wanaonekana ni vijana waliojipanga,hatukuwa na sababu ya kuwa na mashaka tena. Baada ya hapo tukaondoka tukawaacha na Idea.

Lakini kwa kuwa kijana alikua aishi kulia shida nikaanza kufikiria ni jinsi gani nitamsaidia ili asiendelee kuniomba pesa. Kwa kuwa mara nyingi tunakuwaga nje ya nchi nikamshauri mume wangu kuwa tumuachie kijana kiasi cha bidhaa tunazouza ili awe anauza ili ile faida atakayopata imsaidie.

Pamoja na kufuatilia baadhi ya mambo tunayofuatilia katika office za serikali wakati tukiwa hatupo. Mume wangu alikubali na nikampigia kumueleza tulivyowaza, alifurahi sana na kutoa kila aina ya shukurani.

Kesho yake tukamfuata ofisini kwake tukiwa na mzigo, tukampa maelekezo na kumwambia kila anapouza aweke pesa bank, akakubali, na tukampa pesa ya matumizi. Kijana akawa ameachiwa mzigo usiopungua 8M. Hatuna mashaka si ana ofisi!

Tukaondoka safari yetu nje ya nchi tena. Bila yeye kujua tunafuatilia kinachoendelea, kila alipouza mzigo tulijua lakini kijana haweki pesa bank, mara ya kwanza amepokea 289,000/= akawa hata kwenye simu hapatikani, kwa kuwa client wetu tunawasiliana nao, tukawaambia wasimpe pesa waweke bank wakifika kwake wampe pay slip, Kijana akawa mkali mkija na slip hapa hampati mzigo. Client wetu wakalipa cash kwa kijana tena 210,000/= this time nikimpigia anasema anaumwa sana, ataweka pesa bank akipata nafuu. Moyo ukaanza kwenda mbio nikaanza kuwa na mshaka. Nikampigia simu nikimuuliza vipi mbona unapokea tu pesa huweki bank, akajibu nilikua nimelazwa hospital ndio nimetumia kulipia bill, baba akirudi kutoka Dodoma atalipa. Siku akinijibu hivyo client wetu ameenda kuchukua mzigo mwingine wa 150,000/= nikamtumia sms tena kwamba nina shida sana nahitaji tu 100,000/= akanijibu sister kuwa mpole pesa mbona ziko tu. Kwa kuwa nilikuwa ndani ya east africa nikaamua kurudi mara moja kabla sijapata hasara jumla.

Niliamua kuongea na mmoja wa client wetu ili tupange jinsi ya kumtokea bila kijana kujua, Tukiwa na client wetu akapigiwa simu ya kujulishwa kuwa tunataka mzigo, akawauliza wa sh ngapi, wakajibu million moja, akawauliza mmeweka pesa bank au uko na cash, clent akajibu ndio naenda bank, Kijana akamwambia usipeleke pesa bank uje na cash. Hapo ndio nilijua kweli kijana ameamua kula. Ikabidi nambatane na client tukamtokea ghafla na hapo ndipo nilipoweza kuokoa mzigo wetu wote. Jumla ya mzigo aliouza ni sh: 969200/= na mpaka sasa haonekani kujali zaidi ya kuniuliza kwa nini mje bila taarifa.
 
Inawezeka it is a shocking, strange story hasa inapomhusu mtu aliyeaminiwa hata kukasimiwa madaraka makubwa ya nchi, ila nahisi umeinyima uzito sehemu hii uliyoiita ya kwanza maana haina pa kuanzia ku-comment. Lakini pengine ngoja tuone hiyo sehemu ya pili sijui ndiyo itakuwa ya mwisho ili tupate somo na kuona pa kuanzia ku-comment!
 
Kuna haja gani ya kuiweka nusunusu halafu haieleweki??
Sasa kama hapo unataka nini??

Ok! Hongera! au Pole!
 
Imenibidi niandike hatua kwa hatua, ili nisijichanganya kwa machungu. I hope mpaka mwisho wa story mtanielewa. Na labda nitapata msaada.
 
Sasa unataka nini JF?
Dont waste peoples time for threads like this!
 
Hii nafikiri inaweza kuwa njia rahisi ya kumfikia mheshimiwa waziri.
 
Usiimalizie, utanidhalilisha it was a deal between me And you!
 
Nafikir hii habari ungepata wasaa wa kuiandika pemben kwanza kwenye simu au kompyuta ndo uweze kuiweka jamvin ikiwa imekamilika kuliko ulivyoileta robo. Kwa sasa huwez kupata mchango wowote kwa watu inakuwa kama zile hadithi za kwenye magazeti pendwa yanayotoa stori wiki baada ya wiki ili watu waendelee kununua sio hapa jamii forums jamani. Iweke ikiwa imekamilika tafadhali vinginevyo tunachoshana jamani
 
Imenibidi niandike hatua kwa hatua, ili nisijichanganya kwa machungu. I hope mpaka mwisho wa story mtanielewa. Na labda nitapata msaada.

Unaonaje ungesubiri kwanza machungu yaishe halafu ndio ukatupa hadithi kamili, kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. !
 
Haah lipa pesa zangu, maana kama ulipi kudhalilishwa ndio njia pekee, ili kila mmoja akujue. Si unaona story itaendelea kesho, bado una muda wa kulipa.
 
huo ushamba tu! hatutaki hiyo part 2 yako kaa nayo, umeona hatuna kazi mpaka tuje kesho kusubiria part 2 yako?
 
Usiimalizie, utanidhalilisha it was a deal between me And you!

lipa pesa zangu kabla sijamalizia. Si umeonanitamalizia kesho. Hahaha nacheka kwa machungu.
 
Sasa ndo nini tena jamani! WENGINE HUMU ADDICTS WA UMBEAAAA! Hapo nishahisi watu zaidi ya 20. Mwaga mambo banaaaaa! Tupate cha mujuni wikiend yote inayoanza!!!! AU UNAMUOGOPA, UNAMTISHA TISHA INCASE ATARUDISHA? Sheria MMALIZE KABLA HAJAKUMALIZA!!!! Kama ni ------- ndo amekuchota KINGI bora umwage mambo humu, akijua tu unataka kuuza CD ata BBM FASTA MKE WA MTU ANIHONGA! NILIPOKATAA KUMLA KIBOGA ANICHAFUA JF!!! Mbaaaaaaya yule!!!!( jotizi voice) Sasa anaewahi KUROPOKA NDO MWENYE HAKI!!!!! We cheza makida kama hajakugeuzia kibao. Ngoja nizame BBM jst incase akikuwahi!!!! LOL!
 
Mwizi hatishiwa nyau wewe,kesho utashangaa ukiandika modes wanaitupa kauni,weka kila kitu leo mida hii,may be machungu yako yanasukari kiasi,wenye machungu humwaga everything ata a time.
 
Yaani hapo ANAPEWA WARNING, ASIPOLIPA KESHO STORY INAEDELEA ! KAZI KWAKE!
 
Hata mm kanidhalilisha huwezi kuja na Mumeo ktk Contract kubwa km hii
 
Back
Top Bottom