Mtoto wa miezi mitano hajaanza kusimama

Mtoto wa miezi mitano hajaanza kusimama

Daniel Sanare

Member
Joined
Sep 29, 2022
Posts
21
Reaction score
15
Ndug wana JF naombeni ushauri nina mtoto wa miezi 5 lakini huyu mtoto Kila ukijaribu kumsimamisha hata miguuni anakunja miguu lakini ana uwezo wa kurusha miguu vizur lakini unapohitaji kumsimamisha anakunja miguu kama vile Hana nguvu hadi ananijaza hofu.

Naomba mwenye uzoefu na hili kama ni tatzo anisaidie iwe dawa ,lishe ya kumpa n.k
 
Jinsia gani nawewe huyu mtoto Kama wakike sikubali Sana Kama wakiume mkaushie kimtindo Ila mwambieni msaidizi wenu awe anacheza na mtoto mkiwa hampo

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Ndug wana JF naombeni ushauri nina mtoto wa miezi 5 lakini huyu mtoto Kila ukijaribu kumsimamisha hata miguuni anakunja miguu lakini ana uwezo wa kurusha miguu vizur lakini unapohitaji kumsimamisha anakunja miguu kama vile Hana nguvu hadi ananijaza hofu.

Naomba mwenye uzoefu na hili kama ni tatzo anisaidie iwe dawa ,lishe ya kumpa n.k
Hajachelewa kuwa na subra mitano michache bado
 
Mbona mapema sana mpeni mda mm wangu katembea ana mwezi tisa ww km unaona afya yake iko sawa wala usianze kwenda kumti amanuksi kwa waganga.
 
Miezi 5 hata kiuno bado hakijakomaa vizuri unataka asimame?

Miezi 5 hata kukaa peke yake ni amewahi.

Stages za ukuaji mtoto ni kukaza shingo, kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea.

Usiwe na haraka.
 
Mleta mada unataka asimame na kutembea kwa haraka ili uongoze mtoto mwingine chap?
Umesikia rais kasema punguzenu speed ya kuzaa kidogo.
Any way bado mchanga mwache aendelee kukua acha haraka isiyo na maana muda utaongea na kuamua.
 
Miezi 5 hata kiuno bado hakijakomaa vizuri unataka asimame?

Miezi 5 hata kukaa peke yake ni amewahi.

Stages za ukuaji mtoto ni kukaza shingo, kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea.

Usiwe na haraka.
Sawa kaka nashukuru ngoja niwe na subira
 
Wengi walio comment inaonekana hawana watoto na kama wanao basi hawajakaa kabisa na watoto wao enzi za uchanga

Mtoto akizaliwa tu baada ya wiki ukimsimamisha anatakiwa anyooshe miguu yake na asimame wima, yaani sio ukimshikilia asimame mtoto anakunja miguu
Wengi wanadhani ni kusimama kabisa kama mtu mzima

Mleta mada nilipitia hali hiyo kwa mtoto wangu wa kiume wa kwanza na niliogopa sana
Nikampeleka hospital nikaambiwa yupo Ok

Kipimo kizuri kama mtoto yupo ok ni anavyoweza kupush miguu
Yaani ukichukua kalamu ukamkunja mguu kisha mchome kiani mguuni akisikia maumivu atasukumu mguu kuuonyosha..... hapo ujue yupo ok
Lakini kama atabaki hivyo hivyo kakunja tu mguu basi ujue kuna tatizo mpeleke hospitali

NB
Usimchome ukamtoboa
Just to disturb him/her ili a push mguu
 
Ifikapo miezi sita mtoto ataweza kuhimili uzito wake na kujiinua kwa kusimama. Ukimsimamisha kwenye mapaja yako ataanza kuruka juu na kutua,kuruka itakua shughuli yake anayoipenda katika umri huu. Ikiwa mwanao hajaweza kuhimili uzito wake kwenye miguu yake akifika miezi nane ongea na mshauri wako wa afya.​
 
Back
Top Bottom