Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,513
Mtoto mmoja mwenye umri wa miezi minne ameibiwa katika mtaa wa ustawi wa jamii kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela Jijini Mwanza.
Imeelezwa kuwa watu waliomuiba mtoto huyo wamemchukua mama mzazi wa motto huyo kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani lakini baada ya kufika Nyamanoro walimpa shilingi elfu kumi kwenda kununua mkate na baada ya kurudi amekuta tayari wameshaondoka na mtoto wake.
Wakizungumzia kuhusu tukio hilo baadhi ya wananchi wamesema kuwa ni jambo hilo limewashangaza kwani wameshindwa kuelewa lengo la watu hao kumuiba mtoto huyo ni nini na kuwaomba wazazi kuwa makini na watoto wao.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa watu waliofanya tukio hilo mama mzazi wa mtoto anawafahamu hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu hao.
Hata hivyo Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi koani humo linaendelea kuwasaka watu waliohusika na kumuiba motto huyo na kwamba watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya dola.
Chanzo: Mo Dewji Blog