Mtoto wa miezi 5 na siku 2 kapewa uji ni sahihi?

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,780
2,712
Wakuu habarini poleni na majukumu.

Kama kichwa Cha habari kinavoelezea hapo juu mtoto Leo katimiza miezi5 nasiku2 kapewa uji je nisahihi maana mama mtu alikosea kuhesabu miezi akijumia leo miezi 6 ndio imekamilika kumbe Leo ndo mwezi wa6 unaanza kuhesabika nakutimia tar29 mwezi huu ndio miezi6 inakua imekamilika.
 
Usiwaze hata kidogo haitakuwa na shida. Sema tu mtoto umpe uji mwepesi na unakuwa na maziwa fresh yasiyo makali. Ila tu uji usije weka lishe nyingi zenye kuleta choo kigumu.

Kwa sisi wachaga watoto huwa wanakula uji na vyakula vyepesi kuanzia mwezi mmoja tu. Hata mie nikiwa na mwezi mmoja nilipewa uji na vyakula vingine na bado nilikuwa nanyonya.

Exclusive breastfeed inashauriwa sana kwa ajili ya afya ya mtoto. Mtoto anatakiwa apate maziwa ya mama kwa miezi sita ili kumkinga na makonjwa na kuhakikisha anapata virutubisho vyote. .
 
Ila wamama wa siku hizi hawali vyakula vyenye nguvu nyingi unakuta mtu kajifungua anakunywa uji wa sembe. Kwetu uchagani lazima ukae miezi mitatu ndani hutoki unalishwa vyakula vyenye nguvu kama mtori, kena, ng'andi nk.

Viko vyakula vingi vya ndizi kumpa mama nguvu na maziwa yenye virutubisho. Hakikisha mke wako anakula vizuri na anakunywa masupu supu ili maziwa yawe na virutubisho vyote. .
 
Wakuu habarini poleni namajukumu Kama kichwa Cha habari kinavoelezea hapo juu..mtoto Leo katimiza miezi5 nasiku2 kapewa uji je nisahihi maana mama mtu alikosea kuhesabu miezi akijumia leo miezi 6 ndio imekamilika kumbe Leo ndo mwezi wa6 unaanza kuhesabika nakutimia tar29 mwezi huu ndio miezi6 inakua imekamilika
Mapema mno ..pls stop that ..Kama ni ishu ya lishe mpeni maziwa ya S26

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mtoto niliona analishwa ugali akiwa na miezi mitatu, yaani ule ugali wanaubinyabinya kwenye mchuzi linakuwa kama li uji lizito wanampa, alikuwa na afya safi afu kinene.

Nilivyomuuliza mama yake akasema yeye ananyonyesha watoto wake miezi mitatu tu.

Labda kama ni mtoto wa kishua wa kisasa ila kama ni mtoto kijijini miezi mitano mpe tu.
 
Kwanza nampongeza huyo mama kwa kutimiza jukumu lake mpaka miezi hiyo yote maana aki na mama wa siku hizi kunyonyesha kwao ni wanauita mtihani.

Pili sikubaliani na mchango #4 wa Mshana. Michango #5 na 6# usiidharau. Mtoto anaweza kupewa ndizi za kupondaponda na mchuzi wa samaki hata akiwa na miezi minne anaonjeshwa bila shida. Waliozaliwa familia za vijijini wanalijua hili wala halina shida.
 
Kisayansi siyo sahihi.Hawa watu wanaopiga maneno mingi hapa wanakupotosha kwa sababu wanashare experience zao na hawaongei facts za kisayansi.

Narudia tena,kisayansi siyo sahihi.Mkatishe huo uji mara moja na aendelee kunyonya hadi miezi sita ipite.
 
Mwisho watoto wakiwa hawana akili muanze kuilaumu serikali wakati hamfuati lishe bora kwa watoto wenu
Acha mara moja kumpa hivyo vyakula bana
 
Kiuhalisia Afrika mtoto anaweza kupewa baadhi ya vyakula vilaini hata kama wana miezi mitatu.

Achana na uzungu,.. Mpe mtoto vyakula vilaini huku akinyonyeshwa.
Mtoto wangu tangu yupo na miezi 5 anapenda vyakula vyepesi kuliko kunyonya hivyo tukaona tumchanganyie kunyonya huku akipiga msosi
 
Back
Top Bottom