Mtoto wa miaka 12 auawa kisha kunyofolewa sehemu za siri na macho

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa kitongoji cha Mbughantigha kijiji cha Matongo tarafa ya Ikungi, ameuawa na watu wasiojulikana na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa, SSP Isay Mbugh alisema Mei, 18 mwaka huu saa sita mchana wakati ambao Dorcas alipoondoka nyumbani kwao kwa lengo la kwenda shambani kuchuma mahindi, umbali wa kilometa 70.

Alisema mtoto huyo amenyofolewa macho yote mawili, kukatwa matiti yote na kuondolewa sehemu zake za siri.

“Mtoto Dorcas hakuweza kurudi nyumbani kitendo kilichosababisha ipigwe yowe ili watu wakusanyike kwa ajili ya kumtafuta. Haikuchukua muda mrefu, mwili wa Dorcas ulikutwa ukiwa umenyongwa hadi kufa kwa kamba ya ngozi,” alisema.

Alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mauaji hayo yanahusishwa na imani za ushirikina na hadi sasa hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo.

Katika tukio la pili, Kaimu Kamanda Mbugh, alisema watu wawili wamepoteza maisha kufuatia kutokea ajali ya gari anina ya Noah, tukio ambalo lilitokea Mei, 20 mwaka huu saa 6.45 mchana huko katika kijiji cha Mwaja tarafa ya Unyankumi Manispaa ya Singida.

“Ajali hiyo imehusisha noah T.402 DFH iliyokuwa ikiendeshwa na Said Shaban (33), na chanzo cha ajali ni mwendo kasi kitendo kilichosababisha ashindwe kulimudu. Waliofariki kwenye ajali hiyo,ni Elia Daniel (34) mkulima kijiji cha Mwankoko na mwanamke mmoja ambaye jina wala makazi yake,hayajafahamika,” alisema.

Aidha, aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Mratibu Elimu kata ya Mtamaa, Nicodem Elias (45), Juma Ramadhan, mwalimu Chuo cha Maendeleo ya Wananchi, Elia Bilau mkulima na mkazi wa Magungumka Kapela Donad (28).

Kaimu kamanda huyo, alisema dereva wa Noah hiyo Said Shaban anashikiliwa na Jeshi la Polisi na upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: Mo Blog
 
Dah...... jamani. Sasa hiyo kamba waliomnyongea na mwili wake ulishikwa hawaachi finger prints kweli? Na Polisi si watumie ushahidi huo kuwasaka waliofanya hayo?
 
Mtoto miaka 12.
shambani kilometa 70.
Lazima ushangae..lakini ndo hali halisi ndugu...Kuna maeneo vijijini huko ni hsida hatari.

Kijijini kwetu tulikuwa tunatembea mwendo wa masaa matatu kulima maharagwe..sababu ardhi ya pale kwetu ilikuwa haikubali
 
Si mnasema uchawi uko Tanga, sumbawanga na kigoma mbona hatusikii mikoa hiyo wakichunana ngozi na kunyofoana viungo?
 
Watu wanajisahau sana na dunia wakidhani wataishi milele.
Hakika adhabu yao ni kali mno mbele ya Mungu.
 
Nilijua itakuwa kibiti,bwana ametoa bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe
 
Mleta mada,hii mada huwezi kupata comment nyingi,ila ungesema huyo binti kauawa huko Uarabuni basi humu pasingekalika kwa kashfa na matusi na kuingiza udini!!
 
Lazima ushangae..lakini ndo hali halisi ndugu...Kuna maeneo vijijini huko ni hsida hatari.

Kijijini kwetu tulikuwa tunatembea mwendo wa masaa matatu kulima maharagwe..sababu ardhi ya pale kwetu ilikuwa haikubali
Hiyo hali hata mimi naijua na nimetembea pia.

Shida ni huyo mtoto kuwa peke yake kwa umbali huo na ukizingatia ni porini.

Uko wapi wajibu wa mzazi kwa mtoto?
 
Back
Top Bottom