KUNA TETE KUWA LOWASSA ANAMWAANDAA MTOTO WAKE KUGOMBEA UBUNGE-MONDULI.
Mwanae ana haki ya kugombea kama walivyo raia wengine iwapo anatimiza masharti yanayomfanya kuwa mgombea halali. Lakini linalobaki ni maamuzi ya wananchi, wao ndio waamuzi wa mwisho kama kura zinaendeshwa kwa haki.
KUNA TETE KUWA LOWASSA ANAMWAANDAA MTOTO WAKE KUGOMBEA UBUNGE-MONDULI
Kutokana na kashfa nyingi zinazomkabili Lowassa anasita kugombea tena Ubunge-Monduli 2010,hivyo anamwandaa Mtu (Mtoto)wake kwa ajili ya kugombea.Hata hivyo wananchi wa Monduli wasioendekeza takrima wanaonekana kutaka waongozwe na Mbunge safi na asiye tokana na Mtu yeyote mwenye kashfa ya ufisadi au kashfa yoyote ile.Mwenye undani wa suala hili aturushie.
Tetesi nilizozipata ni kuwa Mtoto wa Hayati Edward Moringe Sokoine ndie anaeandaliwa kugombea Ubunge wa Monduli. Habari nyingine pia zinathibitisha kuwa mtoto huyo sie wa kumzaa mwenyewe, bali ni yule aliyewahi kulelewa na Hayati Sekou Toure anaejulikana kama Dr. Ahmed Toure.
Kama mtoto wa Lowassa anataka kugombea, nadhani atakuwa ni Fredrick Lowassa. Sina uhakika kama anakidhi mahitaji sahihi ya watu wa Monduli. Tusubiri tuone.
Recta,
..Dr.Salaash Toure aliwahi kugombea zamani na mpinzani wake akiwa Ole-Molloimet.
Ana haki kama mtanzania yoyote yule, na akishinda itakuwa chaguo la watu wa monduli...waacheni watu wa monduli wachague, ndio demokrasia hiyo hata kama mtoto wa mkubwa, yeye hakuchagua kuzaliwa au kuwa mtoto wa mkubwa...
Ikiwa za kweli au ni za Uwongo ,hilo si tatizo ,shida inapatikana pale wananchi hawafahamu kuwa mabadiliko yanayotakiwa si ya kiongozi bali mabadiliko yanayotakiwa ni kukiondosha Chama Cha Manyang'au na kukivua hatamu za Nchi.
Wananchi mliokuwa mmeshaamka na kuiona dunia anzeni kampeni sasa na kuwaarifu ndugu jamaa pamoja na marafiki popote walipo Tanzania kuwa wabadilike,wachague Chama kingine chochote ,na haswa huko kwenye viti vya wabunge ili kuimaliza nguvu CCM ni lazima CCM ishindwe kwa kishindo kwenye viti vya ubunge.[/QUOTE]
Nakubaliana na wewe kwa hayo mengine lakini kwa hilo nililoli hilight hapo kwa sasa haiwezekani si unaona hao wabunge wa upinzani kwenye suala la mitambo ya DOWANS wamelambishwa asali na sasa wao ndio wamekuwa watetezi kuliko hata hao manyang'au wa CCM? Tanzanians were DOOMED believe me hakuna pa kukimbilia.