Mtoto wa Gaddafi ajirusha… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Gaddafi ajirusha…

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 9, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe.Sifael Paul na Mitandao
  PICHA zinazomuonesha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya aliyeuawa na majeshi ya baraza la mpito la nchi hiyo (NTC), hivi karibuni, Muammar Gaddafi, Hannibal Gaddafi akijirusha na mwanamke aliyetajwa kuwa ni mkewe, Aline ufukweni, zimesambaa katika vyombo vya habari vya magharibi.

  5.jpg

  Habari kutoka mtandaoni zinadai kuwa zipo baadhi ya picha za Hannibal ambazo zilipigwa wakati tayari machafuko ya kumuondoa baba yake madarakani yakiwa yameshaanza.​


  10.jpg

  ...Wakizidi kujivinjari ufukweni.

  Picha hizo zinamuonesha Hannibal akiwa kwenye boti binafsi katikati ya bahari mbali na nchi aliyouawa baba yake, Libya huku wakiweka pozi za ‘kimalavidavi’ kitandani na ufukweni.

  Kusambaa kwa picha hizo za kimahaba zinazomuonesha Hannibal ambaye inasadikiwa alitorokea nchini Algeria na mama na dada yake baada ya hali kuwa mbaya ni mwendelezo wa chokochoko za kuiandama familia ya Gaddafi ili ionekane ilikuwa ikitumbua rasilimali za umma.
  [​IMG]
  HALI IKOJE LIBYA KWA SASA?
  Hali haijatulia nchini Libya kwani vilio dhidi ya vitendo vya ufirauni na mauaji ya kikatili ya Gaddafi bado vinaendelea kwa waliokuwa wakimuunga mkono kiongozi huyo.

   
 2. MGAWARIZIKI

  MGAWARIZIKI JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 306
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapana hizi picha zinaonekana zilipigwa kitambo hata kabla ya machafuko huko Libya
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Tatizo liko wapi? ni msomi mwenye shahada ya elimu ya marine na mba. ajirushe tu, pesa inaruhusu!
   
Loading...