CHADEMA hawawezi kumkubalia huyo Mtoto kwani Baba yake alikufa akiwa na Mgogoro mkubwa na Chama chake alichokuwa kama Makamu Mwenyekiti.(Alikufa kwa ajali ya gari)
Chama hicho hakiwezi kumwamini kwani anaweza kulipiza kisasi, Maana baba yake alikuwa anapigania Ruzuku kwenda kwenye ngazi za chini kabisa wilayani na katani ambako Wananchi wengi waliko, Viongozi wa juu wakiongozwa na Mbowe na Slaa walimkatalia Marehemu Chacha Wangwe suala hilo.
Kama ilivyojionyesha sasa Ruzuku hiyo inazidi kutafunwa bila huruma na ushauri wa Chacha Wangwe muda huo haufanyiwi kazi mpaka sasa, kwani:-
1.Slaa ameingiza Chama kwenye Mkataba wa kimangungo ambao inakilazimu chama kumlipa milioni kumi na tatu(13,000,000/-) kwa mwezi bila makato yoyote, bado posho za vikao na kujikimu, matibabu ya mkono wake n.k
Amejikopesha Mamilioni ya Shilingi bila riba kwakuwa yeye ni kiongozi wa ngazi ya juu.
Pia Ruzuku hiyohiyo imemegwa ili kussuport NGO ya Mchumba wake Mama Josephine Mshumbushi iitwayo IGIHETA.
2.Mbowe amehujumu Ruzuku ya Chama kwa kukiuzia Chama FUSO chakavu kwa bei ya Japan ili hali gari hizo zilikuwa used karibu kuwa scrapper.
Ruzuku inamegwa bila huruma.
3. Heche analipwa Posho na Mshahara kinyume na kanuni na taratibu za Chama, huu ni ubadhilifu dhidi ya Raslimali za Chama.
4.Kamati Kuu ikiongozwa na wazee akina Mtei wanajichotea 'Miposho' bila maandishi.
Haya yaliyokuwa yakipiganiwa na Marehemu Chacha Wangwe hayawezi yakaruhusiwa kurejea ilihali Vigogo wa Chadema wa Ngazi za juu wakineemeka,haiwezekani kitumbua kitiwe 'mchanga'
Kama kijana huyo Zakayo Wangwe akifuta Nyayo za Baba yake atajinasibu kuwa Adui namba moja wa Viongozi wa Chadema zaidi ya Zitto kwani Msimamo wa Baba yake hauwezi kuruhusiwa kurejea ndani ya Chadema kipindi ambacho Kundi la viongozi wanakula bila jasho na walioko chini wanaitikia ''NDIO MZEE'' bila kuhoji, haiwezekani..
Kama Zakayo yuko tayari kuwa Chadema ni Lazima ama kwa kuandikishwa au kusainishwa mkataba ama kwa utashi wake akubali bila shuruti kuwa Chadema na kuwa kibaraka wa wakubwa na sio Mpigania Chadema ya Wanyonge hapo ataishi.
KARIBU CHADEMA, CHAGUA MOJA.