Mtoto wa Chacha Wangwe kuvaa viatu vya baba yake

Mtoto wa Chacha Wangwe kuvaa viatu vya baba yake

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,196
Reaction score
11,623
JULAI 28, mwaka huu wananchi wa Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara waliadhimisha miaka mitano tangu alipofariki dunia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Chacha Zakayo Wangwe.

Maadhimisho hayo yalianzia nyumbani kwa marehemu Wangwe, kijijini kwake Kemakorere, mahali alipozikwa majira ya asubuhi, ambapo viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Manispaa ya Musoma walifika kwa ajili ya kuweka maua na kushiriki ibada fupi iliyoandaliwa na familia ya marehemu. Nikiwa mmoja wa watu waliofika nyumbani kwa marehemu kuadhimisha misa hiyo, nilivutwa na kuguswa zaidi na kijana mkubwa wa marehemu Wangwe ambaye alikuwa amevalia magwanda ya CHADEMA. Huyu ni Zakayo Chacha Wangwe, ambaye mwonekano wake ulivuta macho ya wengi.

Niliamua kufanya mahojiano naye, sababu kubwa ikiwa ni kutaka kujua kilichomsukuma kuwa ndani ya mavazi ya aina hiyo. Kwanza, kabla ya kujibu swali hilo, Zakayo alizungumzia hatua ya familia hiyo kuandaa maadhimisho hayo. Zakayo anasema lengo ni kukumbuka yale yote ambayo marehemu baba yake aliyasimamia na kwa bahati mbaya akafa kabla hayajakamilika.

Anasema baada ya kifo cha baba yake Wilaya ya Tarime imeyumba sana, kwani haijapata kiongozi shupavu ambaye anaweza kusimamia na kupigania maendeleo ya wananchi wa Tarime na Watanzania kwa ujumla. "Ipo tofauti kubwa kati ya uongozi wa marehemu baba yangu na uongozi wa CCM na ndiyo maana unaona sasa hivi Tarime hali si nzuri. "Marehemu baba alikuwa mtetezi wa wanyonge, na kwa bahati mbaya kwa sasa hakuna lolote licha ya wilaya hii kuwa na wabunge watatu,'' alisema Zakayo.

Zakayo ambaye kwa sasa amehitimu elimu ya chuo kikuu na kupata shahada ya mipango ya maendeleo baada ya kuacha kazi katika Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom jijini Dar es Salaam, anasema ameamua kuacha kazi na kurudi nyumbani kwao Tarime ambapo sasa imeingia rasmi katika harakati za kisiasa.

Zakayo anaeleza kuwa ana amini kazi aliyokuwa ameianza marehemu baba yake ya kuwakomboa wana wa Tarime hususan ni wale wanaonyanyaswa katika maeneo mbalimbali yakiwamo ya wachimbaji wadogo wadogo, wamachinga na Wananyamongo ambao hadi leo hawajalipwa haki zao licha ya mgodi wa Barick kupora maeneo yao.

Anasema kazi hiyo alikwisha kuianza marehemu baba yake lakini baada ya kufariki dunia mwaka 2008 hadi leo hakuna kiongozi ambaye amejitokeza na kutetea wananchi hao ambao hadi leo wanazidi kunyanyaswa, jambo ambalo limemfanya aamue kuvaa viatu vya baba yake.

"Nimeamua kuacha kazi ili nije nivae viatu vya baba yangu, nimeona tangu afariki dunia miaka mitano sasa hakuna mtu ambaye ameshajitokeza, mimi nimeamua, nina imani ninaweza, ninachoomba ni wananchi wa Tarime waniunge mkono ili tuweze kuleta ukombozi, alichokiacha marehemu baba yangu nina imani nitakikamilisha, maana baba yangu alikuwa na kaulimbiu ya Kikurya: ‘Ghasi mborake', yaani kweli kutakucha. Hii ni kaulimbiu aliyokuwa akiitumia baba, akiamini Tarime ipo siku kutakucha na wananchi watapata haki zao,'' anasema Zakayo.

Kijana huyo ambaye ameonyesha ushujaa amesema kwa sasa yuko tayari kuwatetea wananchi wa Tarime na Watanzania wote na akawataka Wanatarime kuvunja makundi na kuwa kitu kimoja na kumpa ushirikiano ili aweze kuwatumikia na kukamilisha malengo ya baba yake. Zakayo anafafanua kuwa anataka kumuenzi pia baba yake kwa kufungua mfuko wa maendeleo wa Jimbo la Tarime, mfuko utakaoitwa ‘Wangwe Foundation', mfuko ambao utatumika kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu.

Tofauti na ule usemi usemao nabii hasifiwi kwao, kwa Zakayo ni tofauti, kwani anaonekana sasa kuungwa mkono na vijana wenzake, kina mama na hata wazee, ambapo juzi baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Tarime katika sherehe za kumbukumbu ya kifo cha baba yake alionekana kulimudu jukwaa na alisema maneno mazito ambayo yalianzisha hisia nzito kwa kila mwananchi aliyekuwepo. Ni dhahiri kabisa kuwa nyota ya Zakayo huenda ikaanza kung'aa kutokana na msimamo wake wa kufuata nyao za marehemu baba yake, jambo ambalo wananchi wanaliunga mkono, kwani wengi walisikika wakisema;

"Ama kweli mtoto wa nyoka ni nyoka." Wananchi wanasema tangu amefika wilayani hapo amekuwa chachu kubwa katika kuwahamasisha wananchi katika mambo mbalimbali lakini pia ameonekana kuwa karibu na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) harakati ambazo wananchi wanasema hata baba yake alianza hivyo.

Katika mji wa Tarime kijana huyu sasa anaonekana kuwa gumzo kubwa, wananchi wengi wanaamini kuwa huenda wakapata mkombozi wa kweli atakayeweza kuwatetea katika mambo yao, kwani kila kijana huyo atembeapo amekuwa akiitwa na makundi mbalimbali ambayo yamekuwa yakimutia moyo katika harakati zake alizoanza za kufuata nyao za marehemu baba yake. Msimamo wake wa kukataa wananchi kunyanyaswa na kutopewa haki zao, kupinga vitendo vya ukatili na manyanyaso wanayofanyiwa wananchi wa Tarime na wananchi wengine, umekuwa kivutio kikubwa kwa Wanatarime.

Zakayo anaamini kuwa anatosha kabisa kuwatumikia wananchi wa Tarime na kwamba muda ukifika ana imani kuwa umri wake utakuwa umefika, hivyo hana kipingamizi chochote kitachomuzuia kuomba uwakilishi wa wananchi wa jimbo lake. Anapingana na hoja za kuitwa mtoto, kwani bungeni wapo vijana kama yeye ambao sasa ndio wanaoonekana kufanya kazi zaidi kuliko wazee wengi ambao kazi yao ni kulala bungeni na kupiga makofi hata kwa vitu visivyofaa.

"Katika harakati za kuleta mabadiliko hakuna suala la mtoto, mimi nimeamua kuacha kazi na kuja nyumbani, nimekuta mapungufu mengi ambayo baba yangu aliacha hajayatimiza, mimi ni lazima niyatimize, hivyo wale wanaoniita mtoto waache mara moja,'' anasema kijana huyo.

Huyo ndiye Zakayo Chacha Wangwe, kijana wa aliyekuwa mbunge wa Tarime ambaye ameamua kuvaa viatu vya marehemu baba yake ili aweze kulikomboa Jimbo la Tarime kutoka mikononi mwa ‘magamba'.
 
Anapoteza muda, baba yake alishughulikiwa pamoja na kuwa makamu mwenyekiti wa chadema taifa, yy alie tu, labda agombee kwa chama kingine
 
Angepitia ccm hapo angeeleweka ila kwa anarudi kwa wauwaji wa baba yake, hana jipya

Hivi mnategemea kijana graduate awe na ubongo wa kuku wa kumeza propaganda za wauwaji wa baba yake?

Poleni sana kwani mlitegemea watanzania wataamini propaganda yenu, mkamtoa uhai baba wa watu! watanzania sio wajinga muulize Rev.Mtikila walicho mfanya wanaTarime alipoenda na brah brah zenu!
Nenda Zakayo Chacha Wangwe na Mungu akufanikishe.
 
Anapoteza muda, baba yake alishughulikiwa pamoja na kuwa makamu mwenyekiti wa chadema taifa, yy alie tu, labda agombee kwa chama kingine
Acha kulazimisha watu wayafuate mawazo yako... Demokrasia ni uhuru wa mtu kuchagua na sio wewe kumchagulia ukipendacho wewe.. Nenda ukagombee wewe kwa Tiketi ya LUMUMBA...
 
Utaifakwanza,inaonekana una roho mbaya sana! Prof. Wangwe ni kaka wa marehemu Chacha Wangwe, aligombea ubunge Kibaha 2010 ccm wakamfanyia hujumu kwenye kura za maoni. Leo bado unataka Zakayo aje ccm, ili naye mmfinyange kama Prof.!! Naamini hata profesa Wangwe bado kapotea njia, kubakia ccm!! Utahangaika sana na propaganda zenu, lakini Wana Tarime wanajua thamani ya Chadema kwao, na wala hata uende na tarumbeta hutabadilisha chochote kwao!!
 
Ila aachane na wauwaji kwa tindikali na sumu ie chadema

Kama ni wauaji si nyie mna serikali ambayo mnamiliki wapelelezi na waendesha mashitaka? Wafikisheni mahakamani. Hiki ni kizazi kipya hakikijui chama cha Nyerere kinajua chama chenye sera zinazotekelezeka. Hiyo single ya tindikali na mauaji ya Wangwe haiingii akilini mwao.

Watanzania wa siku hizi wanataka kusikia waliomwaga tindikali wamepatikana na hatia mahakamani na si kuambiwa huyu kamwaga tindikali halafu mnashindwa kupeleka ushahidi mahakamani. Hizo watanzania wa kisasa tunaziona kama propaganda dhaifu zilizopitwa na wakati.

Ukumbuke kuwa hizi propaganda badala ya kuwajenga zinawamaliza maana zinaifanya serikali yenu iendelee kuonekana ni dhaifu. Watanzania tunashangaa, CCM yenye serikali yenye vyombo vya uchunguzi inajua kuwa CHADEMA walimuua Chacha Wangwe. Lakini la kushangaza Imeshindwa mpaka leo kuwafikisha wahusika mahakamani. Ni Udhaifu ulioje? Hii si inaashiria serikali ya CCM ni dhaifu kiasi inashindwa kuwalinda raia wake?????
 
Kijana amesema matakwa yake, sasa wenye matakooo wanataka ayatake yao.
 
Propaganda hizo kama ingekuwa kweli mngewakomalia PoliCCM itafute ukweli mpate pa kuanzia kuhusu Chadema.

Yule mchakachuaji wa elimu ya Tanzania ndugu Nyambari Nyangwine amekalia kuti kavu maana ye ni kugonga meza na kusema NDIOOOOOO...
 
He needs to grow up,baba baba baba baba, have too much of babas,or he wants him resurrected?
 
Nimevutiwa na Maono ya kijana wa Chacha Wangwe.Najua ni pigo kwa wapinzani wake lakini anakila sababu ya kutimiza azma yake.Mungu Ambariki kufikia malengo yake.
Atakutana na vikwazo vingi kwa kuwa wanaoitaka nafasi hiyo ni wengi.Soma Biblia kitabu cha Zaburi 23.Jimbo ni lako.
 
kijana huyu namsifu sana na mungu atakuongoza na kukuonesha nia katika harakati zako hakika utapita na kushinda vizingiti amina
 
mtazungumza sana magamba ila kijana atachukua tu.
magamba mnaweweseka sana mpaka mapovu,jamani
hakuna kingine cha kufanya zaidi ya kutunyonya?
 
Siungi mkono siasa za aina hii...!Only merits should matter.Sio baba yangu alikuwa fulani basi tukuchague.Atwambie yeye ni nani sio mtoto wa nani.Watu walimkataa Sioi Sumari kwa hoja za ku'jificha mgongoni kwa baba' kama hizi....!
 
Angepitia ccm hapo angeeleweka ila kwa anarudi kwa wauwaji wa baba yake, hana jipya
kama Olisi wanasema kwamba Mwangosi aliuwawa na kitu kilichotupwa kutoka wanachama wa chadema na wanasema walijipiga bomu wenyewe huko Arusha watashindwaje kusema kwamba chadema walimuua kiongozi wao Chacha Wangwe?
 
Back
Top Bottom