Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani

Dr Mallesa

Member
Sep 8, 2013
21
5
Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mtoto huyo, Bob Chacha Wangwe (24), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alibadili msimamo jana aliposomewa shtaka hilo kwa mara ya pili, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wangwe alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Mei 11, na alisomewa shtaka linalomkabili na alikiri kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa anapokiri kosa, kwa kawaida Mahakama inaweza kumtia hatiani na kumpa adhabu kwa mujibu wa sheria, kulingana na kosa siku hiyo hiyo au siku nyingine yoyote.

Baada ya kusomewa shtaka na kukiri, Hakimu Mkazi Mkuu, Waria lwande Lema, aliamuru mshtakiwa huyo apelekwe rumande hadi jana, Mei 17, kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo hakuwapo.

Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alipopandishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo, ili kusomewa maelezo ya awali kabla ya Mahakama kumtia hatiani na kumhukumu, tofauti na siku ya kwanza, alikana kutenda kosa hilo.

Kutoka na mshtakiwa huyo kukana kosa, Wakili wa Serikali, Salim Msemo, aliieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliiomba ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.

Wakili wa mshtakiwa huyo Peter Kibatala aliiomba Mahakama impe dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika, maombi ambayo yalikubaliwa na aliachiwa kwa dhamana na kesi iliahirishwa hadi Juni 15.

Wangwe ambaye baba yake kwa sasa ni marehemu, anadaiwa Machi 15, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
 
We should use our time appropriate, kama upo shule concentrate kwelikweli, haya mambo yakudandia dandia mbaya sana anaweza akakosa vyoote asipoangalia,
 
Huyo dogo anatafuta umaarufu ili aje kupewa jimbo, lkn awe makini na hao wanaomtumia sio watu wazuri hata mzazi wake ambaye ni marehemu alikuwa akiwajua vizuri sana hao watu, hawana maana hata kidogo ukigusa saccos yao
 
We should use our time appropriate, kama upo shule concentrate kwelikweli, haya mambo yakudandia dandia mbaya sana anaweza akakosa vyoote asipoangalia,

Tusiandike tu mradi unataka kuandika
Masomo ya chuo kikuu in zaidi ya kusoma vipolo vya mawazo ya wenzio vilivyo hifadhiwa kwenye vitabu it needs more.

Tukubaliane tu kuwa tunaingia dhama nyingine ya utawala wa mabavu kila sector.
Ukweli hata usipoutungia sheria upo palepale.
Kwani alichoandika huyu dogo nani asiyekijua au tatizo lake ni kusema.
Ukiangalia True History Of the Union

Utagundua kuwa dogo ni mhanga wa hali halisi.
 
sasa alivyokuwa rumande hizo tests na assignment mh! aangalie asije akarudia mwaka uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii (repeat a year)
 
Back
Top Bottom