Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 458
- 500
Sina budi kupongeza serikali kwa hatua mbalimbali za kutulea. Hapa nakusudia serikalika za awamu zote.
Pamoja na pongezi hizo, napenda kukumbuka usemi wa wahenga hapo juu.
Mashirika yetu yote ya umma Yana changamoto kubwa ninayoifananisha na malezi ya mtoto. Kuna kulea mtoto ili aweze kujitegemea na Kuna malezi yanapelekea mtoto kuwa tegemezi maisha yake yote.
Kwa maoni yangu, naona mashirika yetu ni Kama yule mtoto anaelelewa kuwa tegemezi daima. Bilashaka tunajuwa hakuna shirika hapa nchini linaweza kujiendesha hata kwa miezi sita bila mkono wa serikali. Hali hiyo, inapelekea mashirika hayo kulala usingizi wa pono na kukosa kuona mwelekeo sahihi wa kustawisha mashirika yao.
Ni mfano tu, TANESCO Hana uwezo wowote wa kutekeleza mradi mkubwa wowote bila serikali au Kodi za nchi yetu na hawaoni njia ya kunasua shirika. Wapo gizani. Hawajuwi chanzo chao Cha mapato ni kipi, na wanakiboreshaje kwakuwa serikali ipo na inatoa pesa za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme.
Ona miradi ya mifuko yetu ya hifadhi za jamii inavyotekeleza miradi isiyo na tija na kupelekea mkwamo wa kuhudumia walengwa! Yote hayo ni kwakuwa serikali inalipa mishahara yao.
Kwa muktadha huu, ni vema sasa tutambuwe tofauti ya huduma na biashara. Kama ni huduma iwe huduma kweli na kwa sheria Bora tulizojiwekea.
Mashirika yetu yanahita kufanyiwa tathimini ya kina na maboresho Yenye tija kwa wote