KALYANKOZILE
Member
- Apr 24, 2013
- 19
- 1
Baada ya baba kuwa na familia alijaliwa watoto wa kike wawili na wa wakiume mmoja wakati huo huo baba huyu alijipenyeza na kwenda nyumba ndogo ambapo alijipatia pia mtoto wa kiume na baada ya kufikisha umri wa miaka 14 baba yake ameamua kuweka mambo wazi kwa mke wake na mke wake kumuelewa na hivyo kijana huyo kuanza maisha mapya kwenye familia yao lakini Kijana huyu amekuwa mtata pale anashindwa kuwaelewa ndugu aliowakuta kwenye familia hiyo hasa wa kike na kuanza kuwauliza maswali; nyie mnasema mimi ni ndugu yenu mbona mna mama yenu na mimi nina mama wa kwangu? na baba huyu ni baba yenu wa kwangu mama aliniambia alifariki nikiwa mdogo je inakuwaje awe huyu au amefufuka!!!matokeo yake ameanzisha mahusiano ya kimapenzi na watoto wote wa kike na kubahatika kumpatia mimba msichana mmoja na penzi lao kujifunua kwa wanafamilia wote kwani wameshindwa kuficha mahusiano yao.Swali je na wa kurahumiwa ni nani? na nini kifanyike kwani hadi sasa mto umeanza kuwaka kwenye familia hiyo.