Mtoto: Nilipigwa risasi na polisi


Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,873
Likes
791
Points
280
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,873 791 280
BONYEZA uangalie Bomu lilivyo ripuka swahilivilla: Angalia kwa makini Video ya mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa Chadema . [h=2]Tuesday, June 18, 2013[/h] [h=3][/h]

Arusha/Dodoma. Wakati watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa, amedai kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo
.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kampeni wa chama hicho.


Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani yaliyodhuru ubongo wake.


Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo.


Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma.

Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru.


Mtoto aeleza kupigwa risasi


Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.


Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.


“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.


Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.


“Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni risasi au la,” alisema Semdeli.


Polisi wazungumzia risasi


Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Polisi, Kamishna Isaya Mngulu alisema hakuwa na taarifa za watu kufa na kujeruhiwa na polisi kwa risasi. Hata hivyo, alikiri kuwa wameokota maganda ya risasi, ambayo wanafanyia uchunguzi.


“Ni kweli tulikuta maganda ya risasi kwenye tukio lakini ni vigumu kusema kama polisi ndio walipiga bunduki. Nadhani ni mapema mno kwani bado tuko kwenye uchunguzi,” alisema Mngulu, ambaye yumo katika timu iliyoteuliwa na Mkuu wa Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza tukio hilo.


Lakini, Kamanda wa Polisi wa Arusha, Liberatus Sabas alisema hana taarifa ya watu kupigwa risasi... “Mimi sijui lolote kuhusu watu kupigwa risasi. Naomba usiniulize mambo ya ajabu ajabu,” alijibu kwa ukali na kukata simu alipoulizwa juu madai hayo ya polisi kutumia risasi za moto.


Majeruhi mwingine


Majeruhi mwingine, Abdallah Hilali (39), aliyelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Center, amedai kuwa majeraha aliyopata miguuni yametokana na kupigwa risasi na polisi na kudondokewa na vipande vya bomu.


Alisema alikuwa nyuma ya jukwaa kuu akimsikiliza Mbowe na alipomaliza kuhutubia alishuka jukwaani kukusanya sadaka, ndipo alipoona mfuko wa mweusi mdogo wa plastiki ukipeperuka juu.


“Nilidhani ni upepo unapeperusha kitu, lakini ghafla nilisikia kishindo na nikamsikia mama mmoja akipiga kelele kuwa aliyerusha mfuko anakimbia, nilipogeuka nikajikuta nipo chini,” alisema Hilali.


Alisema alipokuwa anaangalia aliona kijana mmoja amekaribia kumfikia aliyerusha bomu lakini ghafla akapigwa risasi na kuanguka chini na aliyekuwa anafuatia kwa nyuma naye akapigwa risasi akaona anaruka na kudondoka chini huku damu zikivuja.


“Lakini mwisho wa yote kijana aliyerusha hilo fuko aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi. Mimi nilikuwa chini,” alisema Hilal mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alipotembelea majeruhi hospitalini hapo.


Jana, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walitembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali mbalimbali za Arusha.


Mbowe tunawajua watuhumiwa


Mbowe amedai kuwa wamewagundua watu waliohusika na urushaji wa mabomu katika Viwanja vya Soweto Juni 15, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi zaidi ya 60.


Akizungumza jana baada ya kutembelea majeruhi katika Hospitali ya Seliani, Mbowe alisema Chadema tayari imewajua wahusika wakuu wa mabomu hayo kwa ushahidi wa picha. Alidai kuwa ni askari mmoja wa Kikosi cha Polisi wa Kuzuia Fujo (FFU).


Alidai kuwa ushahidi huo unaonyesha kuwa wakati askari huyo akirusha bomu, alikuwa na kofia inayofanana na ile inayotumiwa na Polisi na mara baada ya kurusha bomu na risasi za mfululizo alikimbilia kwenye gari aina ya Land Cruiser na kusindikizwa na Polisi.


“Duniani hakuna siri yoyote ile. Tumeshafanikiwa kugundua chanzo kikubwa na ushahidi unaonyesha wahusika ni polisi. Ushahidi huu tutauweka hadharani na kila mwanadamu aweze kujionea kwa kuwa waliokufa hawana hatia yoyote na sisi tumechoka kila siku kuonewa na Polisi,” alisema.


Aidha, Mbowe amepinga kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na ile ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Uratibu na Sera), William Lukuvi kuwa Arusha inaharibiwa na wanasiasa pamoja na asasi binafsi.


Nape aituhumu Chadema


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekituhumu Chadema kuwa ndicho kilichofanya mpango wa kulipua bomu lililosababisha vifo vya watu watatu jijini Arusha baada ya kubaini kuwa kitashindwa katika uchaguzi wa udiwani katika kata nne.


Amedai kuwa mpango huo ulipangwa na Chadema baada ya wananchi wa Arusha kuapa kutokichagua tena kutokana na kuchoshwa na kauli za viongozi wake zinazochochea maandamano na vurugu, jijini humo.


Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Nape alisema Chadema kinatakiwa kuacha kutafuta umaarufu kwa mtindo wa kumwaga damu za Watanzania na kwamba juhudi hizo zinatakiwa kulaaniwa vikali.


Alipoulizwa sababu za kukitaja Chadema kuwa kinahusika moja kwa moja licha ya kuwa uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi umeonyesha kuwa mazingira ya tukio hilo yanafanana na lile la kanisani alisema, “Tunasema hivyo kutokana na kauli zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Chadema kabla ya tukio na walipanga ndani ya chama chao ili uchaguzi usifanyike.”


Mamia wakusanyika Soweto


Mamia ya wananchi jana walikusanyika katika Viwanja vya Soweto ulikotokea mlipuko huo, kwa ajili ya kuomboleza.


Mazishi ya waathirika wa tukio hilo yanatarajiwa kufanyika mara baada ya uchunguzi wa madaktari kukamilika na miili itaagwa katika eneo hilo kabla ya kusafirishwa katika maeneo yao ya asili. Mwili wa Judith Moshi utasafirishwa kwenda Kilimanjaro, Ramadhan Juma (Tabora) na wa Amir utapelekwa Lushoto.


Mlipuko huo ulitokea juzi wakati Chadema, kilipokuwa kikihitimisha kampeni zake za udiwani na kusababisha kuahirishwa kwa uchaguzi katika kata za Themi, Kaloleni, Elerai na Kimandolu hadi Juni 30.


Marekani yalaani


Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt ameshutumu vikali mlipuko wa bomu kwenye mkutano huo wa kampeni wa Chadema Arusha ambao ulisababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.


Balozi Lenhardt ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa na kutoa pole kwa wale walioumia.


“Tunaomba vyombo vya dola kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kushtakiwa,” alieleza Balozi huyo katika taarifa yake.


Chanzo - Mwananchi
 
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Messages
1,873
Likes
791
Points
280
Kakke

Kakke

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2010
1,873 791 280
Jee ccm mukimuua Mh Mbowe na viongozi wenzake ndio Chama cha Wananchi Chadema Ndio Kitakufa? Kikwete The Hague haiku mbali Tanzania tunayo yetu Arusha na sio kuwa kifua mbele tu kuwahukumwa Wanyaruwanda na wewe na Viongozi wenzako munaweza kupanda vile vile.
 
V

van the man

Member
Joined
Apr 3, 2012
Messages
12
Likes
0
Points
3
V

van the man

Member
Joined Apr 3, 2012
12 0 3
Damu ya binadamu ni tofauti na ya mnyama, bila kutubu na kuacha huu uovu wahusika wote damu hii inayomwagika katika ardhi yetu itawanenea mabaya mbele za Mungu Mwenye haki naye atawalipa sawasawa na uovu mnaoufanya hasa hao waliopewa dhamana ya kuwalinda watu na sasa ndio wanaowaangamiza. Kama Mungu aishivyo, damu hii haitamwagika bure.Watu wasio na aibu, wenye mioyo ya jiwe isiyo na chembe ya huruma. Mnawaua watu na kusema eti wamejilipua wao wenyewe.Na wengine waongo kiasi hicho mnaitwa makanisani kwenye harambee mnachanga fedha mlizozipata kwa kumwaga damu huku mkinukuu maandiko kana kwamba kuna kumcha Mungu ndani yenu.Hakika mkono wa Mungu hautawaacha mwe salama,mpumzike kwa amani na babu zenu.
 
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,073
Likes
493
Points
180
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,073 493 180
Hivi ndio kusema serikali ya CCM imeshindhwa kushughulikia masuala kama umasikini, maradhi na ujinga sasa imejikita kupambana na watu wahanga wa masuala haya?
 
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2010
Messages
999
Likes
6
Points
135
N

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2010
999 6 135
Namshaurimdogo wangu Nape ajue kuwa Mungu amempa nafasi ya kujipambanua, kujionyesha nakuwa kioo cha vijana wa Tanzania kupitia CCM, Napeusimpige Mungu kofi kwa kujiona umfika na kujifungia kwenye hako kabox kachama,fikiri zaidi ya CCM, Fikiri zaidi juu ya Tanzania, Fikiri juu ya Afrikamashariki, Fikiri juu ya Afrika na ikiwezekana juu ya Ustawi wa Dunia. Nafasiuliyopewa ni funguo wa vijana kuaminiwa na jamii, kama vile wazee wa Tanuwalivyo mwamini Julius Nyerere kuwaongoza kudai uhuru. Niaibu endopo utashindwa kuitumia nafasi yako kuwaunganisha vijana Watanzania nabadalaya yake unawagawa kwa itakadi zao.Kumbukawajibu wakuwalinda Watanzania wote wakiwemo wa CDM, CCM, CUF, NCCR na wasio na vyamakama hawa watoto waliouwawa ni serikali ya CCM. KamaCDM walipanga kujilipua na wewe ulikuwa na taarifa hukuchukua hatua, moja kwamoja unahusika na mauwaji haya.
 
D

duchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Messages
1,766
Likes
3
Points
0
D

duchi

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2012
1,766 3 0
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
 
SERGIO

SERGIO

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Messages
348
Likes
6
Points
0
SERGIO

SERGIO

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2012
348 6 0
Nimuulize Nape: Hivi kati ya CCM na Chadema ni chama gani kilichokuwa na hofu ya kushindwa kwenye uchaguzi wa kata nne za Arusha? Jibu haraka! Pambaf.
 
Kufa c mwiko

Kufa c mwiko

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Messages
552
Likes
54
Points
45
Age
43
Kufa c mwiko

Kufa c mwiko

JF-Expert Member
Joined May 26, 2013
552 54 45
Je ni kiongozi chama kipi alisema watahakikisha nchi haitatawalika? je ni kiongozi wa chama kipi alisema wanahakikisha arusha watashinda kwa gharama yoyote? hiyo ni "circumstantial evidence" kuwa mauaji yote ya arusha yanapangwa na chadema ili watu waichukie serikali yao. Kumbuka kesi ya kupanga njama za mauaji iko mahakamani.
duh!? Acha njaa ya mk.nd. Wazi unahalisha chochote unachojisikia?!
 
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Messages
14,691
Likes
1,314
Points
280
Arushaone

Arushaone

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2012
14,691 1,314 280
Kama siyo hapa duniani hata akhera CCM mtakuja kulipa tu damu za watu wote na hasa watoto wote mnaoshiriki na mlioshiriki kuwaua. Damu zao hazitapotea bure kamwe!
 
K

kibelaa

Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
95
Likes
3
Points
0
K

kibelaa

Member
Joined Apr 2, 2012
95 3 0
Pole mtoto,ww pamoja na wenzako wote,hakika damu zenu hazitaenda bure,nyie mlikua mnapita,mmetoka madrasa,hamkuwa kwenye mkutano. Maumivu na kilio chenu kimefika kwa Mungu yeye alie Hakimu wa yote.
 
R

Rato

Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
92
Likes
0
Points
0
Age
50
R

Rato

Member
Joined Jul 10, 2012
92 0 0
Viongozi onyesheni hekima sasa tuweze kujua tumsikilize nani
 
Kiwi

Kiwi

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
1,031
Likes
258
Points
180
Kiwi

Kiwi

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2009
1,031 258 180
Mwalimu Nyerere alisema, 'Ukianza kula nyama ya mtu hutaacha'

ccm sasa mmefikia kutuua na kula nyama za watu, hamtaacha kamwe...
Mmeshakuwa ma 'dracula', mnataka kututoa uhai sote ili kuendelea kula nyama za watu.
Simba mla watu dawa yake ni moja tu, huwindwa mpaka auawe...
Siku zenu zinahesabika!!!
 

Forum statistics

Threads 1,275,212
Members 490,932
Posts 30,535,930