Mtoto mchanga kulia sana usiku wa manane

Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
14,083
8,374
Wakuu mtoto ananipa wakati mgumu sana, ana wiki 6 sasa na amekua analia sana usiku yani kilio cha yowe kabisa.

Nimejaribu kumpa dawa 'infacol' na bonnisan lakini tatizo bado liko pale pale shida itakua nini? Hizo dawa nimepewa baada ya kumuona pediatrician.
Alafu mida yake sasa ni kuanzia sa 7,8, 9 mpk sa10 tu kila siku. Mchana halii kabisa kabisa, daah ananipa wakati mgumu sana huyu mtoto.

Naomba uzoefu please
 
Pole sana mkuu
Hiyo hali mara nyingi hutokea kwa baadhi ya watoto, jaribu kumtafutia kifaa hiki "baby pacifier" kinaweza kusaidia kupunguza tatizo lkn uwe makini asikizoee sana sbb navyo nadhani vinamadhara kama matumizi yatazidi

Lakn pia kama utaweza muache alie usimbembeleze anapoanza kulia baada ya muda ataacha mwenyewe japo siyo rahisi lkn pia inasaidia
 
Labda mtoto hashibi, niliwahi kumuona mama mmoja akihojiwa kuhusu mtoto wake aliyekuwa anasumbua sana usiku wa manane kwa kulia hata masaa mawili/matatu akahangaika huku na kule kwa madaktari bila ahueni yoyote mpaka alipokutana na daktari aliyemwambia huyu mtoto kote ulikopita hawakuona tatizo la kiafya mchana anashinda vizuri kabisa usiku wa manane ndiyo anaangusha kilio. daktari akasema labda mtoto hashibi jaribu kuhakikisha mtoto anashiba na labda maziwa yako hayamtoshi hivyo alimshauri anunue maziwa ya kopo. Yule mama akadai baada ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya kopo pamoja na ya kwake kulia usiku wa manane kukafikia ukomo.

Wakuu mtoto ananipa wakati mgumu sana, ana wiki 6 sasa na amekua analia sana usiku yani kilio cha yowe kabisa.

Nimejaribu kumpa dawa 'infacol' na bonnisan lakini tatizo bado liko pale pale shida itakua nn? Hizo dawa nimepewa baada ya kumuona pediatrician.
Alafu mida yake sasa ni kuanzia sa 7,8, 9 mpk sa10 tu kila siku. Mchana halii kabisa kabisa, daah ananipa wkt mgumu sana huyu mtoto.

Naomba uzoefu please
 
mkuu usijali nliwahi kuwa na tatizo kama hilo nlihangaika sana lakini alivofikisha miezi mitatu aliacha mwenyewe
 
Tafadhali elezea jinsia ya Mtoto. Kwa mujibu wa maelezo yako nahisi ni mwanaume please confirm then nikushauri.
 
Pole sana mkuu
Hiyo hali mara nyingi hutokea kwa baadhi ya watoto, jaribu kumtafutia kifaa hiki "baby pacifier" kinaweza kusaidia kupunguza tatizo lkn uwe makini asikizoee sana sbb navyo nadhani vinamadhara kama matumizi yatazidi

Lakn pia kama utaweza muache alie usimbembeleze anapoanza kulia baada ya muda ataacha mwenyewe japo siyo rahisi lkn pia inasaidia

Mkuu asante ila kwa kweli nimechanganyikiwa kwa hili tukio
 
Labda mtoto hashibi, niliwahi kumuona mama mmoja akihojiwa kuhusu mtoto wake aliyekuwa anasumbua sana usiku wa manane kwa kulia hata masaa mawili/matatu akahangaika huku na kule kwa madaktari bila ahueni yoyote mpaka alipokutana na daktari aliyemwambia huyu mtoto kote ulikopita hawakuona tatizo la kiafya mchana anashinda vizuri kabisa usiku wa manane ndiyo anaangusha kilio. daktari akasema labda mtoto hashibi jaribu kuhakikisha mtoto anashiba na labda maziwa yako hayamtoshi hivyo alimshauri anunue maziwa ya kopo. Yule mama akadai baada ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya kopo pamoja na ya kwake kulia usiku wa manane kukafikia ukomo.
Kama kushiba mtoto huyu anashiba mpk maziwa yanavuja kwa mama ake. Sasa sijui labda kujaribu kusuppliment hiyo maziwa ya kopo. Asante sana kwa ushauri mkuu
 
Tafadhali elezea jinsia ya Mtoto. Kwa mujibu wa maelezo yako nahisi ni mwanaume please confirm then nikushauri.
Mkuu huyu ni jinsia ya kike, ni mtoto wa2 na dada yake hakuwahi sumbua kiasi kama hiki
 
Labda mtoto hashibi, niliwahi kumuona mama mmoja akihojiwa kuhusu mtoto wake aliyekuwa anasumbua sana usiku wa manane kwa kulia hata masaa mawili/matatu akahangaika huku na kule kwa madaktari bila ahueni yoyote mpaka alipokutana na daktari aliyemwambia huyu mtoto kote ulikopita hawakuona tatizo la kiafya mchana anashinda vizuri kabisa usiku wa manane ndiyo anaangusha kilio. daktari akasema labda mtoto hashibi jaribu kuhakikisha mtoto anashiba na labda maziwa yako hayamtoshi hivyo alimshauri anunue maziwa ya kopo. Yule mama akadai baada ya kuanza kumpa mtoto maziwa ya kopo pamoja na ya kwake kulia usiku wa manane kukafikia ukomo.
Ulichokiongea ndio uhalisia wenyewe wa mambo, hakuna uchawi hapo! Wampe mtoto maziwa ya kutosha halafu waache kumfunga pampas, wamwache awe huru, wakati mwingine mtoto analia kumbe ni pampas imelowa au imefungwa vibaya plus njaa, Kweli mtoto asilie?
 
Kama kushiba mtoto huyu anashiba mpk maziwa yanavuja kwa mama ake. Sasa sijui labda kujaribu kusuppliment hiyo maziwa ya kopo. Asante sana kwa ushauri mkuu
Wakati mwingine huwa ni mepesi sana kutegemeana na msosi wa Mama, Aache kwanza kula chips yai
 
Vipi kitumbo chake hakimumi gesi? Na vipi choo anapata kikawaida?
choo kawaida tu, ila gesi ni mojawapo ya sababu coz huwa anajamba jamba sana. Hata ivyo niliambiwa na Doc kua Bonissan ndio inamaliza gesi tumboni. Cha ajabu ni kuwa mchana anakua poa sana isipokua ikifika sa 6-10 ni balaa mtoto anapiga yowe ni vile tu naishi nyumba sehem ambapo sio rahisi kusumbua jirani
 
Ulichokiongea ndio uhalisia wenyewe wa mambo, hakuna uchawi hapo! Wampe mtoto maziwa ya kutosha halafu waache kumfunga pampas, wamwache awe huru, wakati mwingine mtoto analia kumbe ni pampas imelowa au imefungwa vibaya plus njaa, Kweli mtoto asilie?
mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako kwa kweli Mungu awabariki wote kwa ushauri huu. Nimeuchukua na nitaleta feedback kuanzia usiku wa leo.
Diapers ni rahisi zaidi kumsaidia mtoto kwani kuna wakati anakua na frequent pee so badala ya kubadili nepi inasaidia kumbaidili kwa mda kidogo.
 
Usimfunge hayo madude please, muache kabisa aiseee
 
Wakati mwingine huwa ni mepesi sana kutegemeana na msosi wa Mama, Aache kwanza kula chips yai
nimeshauriwa asile vitu vyenye asidi mfano maziwa mgando, broccoli, cauliflower, malimao, machungwa, maharage, juice, lemonade nk viepukwe. Chips nooo hali
 
Back
Top Bottom