Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto kuzaliwa na meno

Discussion in 'JF Doctor' started by thereitis, Jan 31, 2011.

 1. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 295
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mtoto wangu amezaliwa akiwa na meno mawili ya chini. Je hali hii inasababishwa na nini? je nini kinasababisha mtoto kuzaliwa na meno?
   
 2. manyoda

  manyoda Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Habari yako ndugu? Awali nikupe hongera kwa kupata mtoto, ni zawadi adhimu mno!
  Kitaalam meno ya mtoto huanza kutengenezwa akiwa tumboni, yaani in intra uterine life, na moja katika hatua zake ni utengenezwaji wa vitu vinavyoonekana kana kwamba ni meno, yaani dental papillae! hizi hazitakiwi kuonekana kinywani, na papillae za meno ya utoto na ukubwa zote hutengenezwa mtoto akiwa tumboni.
  Kwa sababu za kimaumbile, baadhi ya watoto dental papillae zao huonekana kinywani na kuonekana kana kwamba ni "meno ya plastiki", ukweli ni kuwa hizi ni dental papillae ambazo huja kutengeneza meno ya utu uzima, yaani permanent teeth ama ya utoto, yaani deciduous au milk teeth.
  Baadhi ya makabila huyang'oa meno haya, tena kwa vifaa visivyo salama!Haya ni makosa MAKUBWA ambayo huweza kumsababisha mtoto kukosa meno yake ya sehemu husika ya utoto ama ukubwa ama yote! Pamija na hatari nyinginezo km vile kutoa damu kwa wingi, maambukizi, yaani infections nk!
  Kwa kumalizia, meno hayo hayana tatzo kabisa kwa mtoto! Kwa ushauri zaidi mwone daktari wa meno aliye karibu nawe, preferably awe ni Dental surgeon ama assistant Dental officer.
  Tunamtakia mtoto makuzi na malezi mema.
  AHSANTE
   
Loading...