Wana JF Doctor habari zenu wote.
Mwanangu amemeza gololi tangu jana majira ya saa 3 asbh. Ni hizi gololi wanazonunua madukani na kuchezea(sijui vizuri materials zake,lakini sio zile za chuma zitumikazo kwenye baiskeli nk). Hadi sasa yupo kawaida tu,halalamiki maumivu yoyote wala hakohoi.
Hapa JF ndipo penye ushauri yakinifu. Nisaidieni jamani wanajamvi.