Mtoto Azinduka Makaburini Kabla ya Kuzikwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
UONGOZI wa Hospitali ya Temeke umelazimika kuunda tume kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la mtoto aliyezinduka akiwa makaburini katika harakati za kuzikwa ambapo mtoto huyo alihisiwa si hai hospitalini hapo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Bi. Aisha Mahita amesema kuwa, tume hiyo inatarajia kutoa majibu kwa muda wa siku mbili kuanzia jana kutokana na uzito wa tukio hilo.


Tukio la mtoto huyo kufufuka limekuja baada ya mtoto huyo kuhisiwa kuwa amekufa kutokana na uzito aliokuwa nao mtoto huyo sio wa kawaida kwa watoto wanaozaliwa.


Wataalamu waliomzalisha mama huyo waliruhusu vichanga hivyo vizikwe bila ya uthibitisho wa kina wa vichanga hivyo vilivyozaliwa mapacha hospitalini hapo.


Mganga Mkuu huyo alisema kuwa watoto hao walizaliwa huku mmoja akiwa na gramu 500 na mwingine gramu 1000.



Mwanamke Aisha Jabir [32] mkazi wa Mbagala Maji Matitu alifikishwa hospitali ya Temeke kwa ajili kuangalia afya yake huku akiwa na mimba ya miezi saba, lakini ghafla hali yake ilibadilika na kujifungua watoto wawili mapacha wa kiume ambapo madaktari waliomzalisha walidai kuwa watoto hao walikuwa wamekufa.


Ndipo vichanga hivyo vilipochukuliwa uamuzi wa kuzikwa na mmoja kati yao akiwa katika harakati za mazishi makaburini alionekana akiwa hai


Hata hivyo baba wa vichanga hao aliyetambulika kwa jina la Allly Athumani alitoa tarifa kwenye vyombo vya habari kuwa anatarajia kufungua kesi Mahakamani kwa kuthibitishiwa kuwa watoto hao walikuwa wamekufa kumbe mmoja alikuwa hai na kudai huenda wote walikuwa hai.


http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3709474&&Cat=1
 
Back
Top Bottom