Mtoto analia sana nyakati za usiku

Mtoto analia sana nyakati za usiku

Try this.....give her a pacifier and see what happens (although I know a two week old baby could be too young for one but it won't hurt to give it a go).

In addition, swaddle her and then rock her.

Also try to make sure that the air in the room is not so dry. If it is, buy a humidifier. It's also good to check the room temperature.

From my experience, there is a lot of trial and error when it comes to new babies because every baby is different.

Samahan unaweza kunitafsiria sijaelewa#Nyani Ngadu
 
Samahan unaweza kunitafsiria sijaelewa#Nyani Ngadu

Jaribu hivi....mpe titi/ chuchu bandia uone itakuwaje (japokuwa najua kwamba mtoto wa wiki mbili anaweza kuwa mdogo mno kuanza kumpa titi/ chuchu bandia, lakini haitadhuru kitu ukijaribu).

Vile vile, mfunge kwenye shuka au blanketi halafu mpembeze pembeze.

Pia hakikisha hewa ya chumbani si kavu sana. Kama ni kavu sana basi angalia uwezekano wa kununua kileta unyevunyevu. Ni vizuri pia kuangalia halijoto ya chumba.

Kulingana na tajiriba yangu, kwenye kulea watoto wachanga kunahitaji majaribio na kubahatisha kwingi kwa sababu watoto huwa wanatofautiana.

Unajaribu hiki, kikikataa unajaribu kile, kile kikikataa unajaribu kingine. Hii yote ni kwa sababu watoto hususan wachanga hawana namna nyingine ya kuwasiliana nawe zaidi ya kulia.
 
Hiyo hali ni ya kawaida sana wala usihofu. Mimi mtoto wangu alikuwa analia mpaka sauti inakauka hadi na mimi nikawa nalia. Alipofiksha mwez na nusu hali ilikwisha kbs.
Ha ha ha ha
 
Sio tu Kulia sana kwa mtoto usiku wakati mwengine Mtoto huwa anastuka stuka kisha ndio huanza na kulia. Kulia au kustuka kwake mtoto kunasababishwa nyumba yenu kuna aidha pepo wabaa au nyumba yenu munatembelewa na wanga usiku ndio maana mtoto anawaona na kuanza kulia usiku au mama mtoto ana pepo mbaya anamuinamia fanya hivi jaribu kila usiku anapolala mtoto jambo la kwanza kusiwe giza kuwe na taa sehemu anapolala mtoto, jambo la pili umfukize na magamba ya kitunguu saumu wakati wa kulala mtoto. Dawa zingine nitafute mimi ukiweza kunipata mimi bonyeza hapa.Mawasiliano
Umeongea ukweli mtupu haya ya mapepo au wanga mtoto akiendelea ndio wanahusika sana ,yamenitokea haya mambo sana utotoni ,aiseee mzizi mkavu umetisha
 
Uwe unagandisha maziwa ya ngombe ,halafu unayatikisa kutengeneza mafuta ya samli. Utaona mafuta meupe yatajitokeza. Then chuja mafuta pembeni na utafute maji masafi na salama usafishe ile mafuta kutoa ule umaziwa mgando. Afu umpe maranyingi uwezavyo.
 
Kwa kweli kulia kwa mtoto usiku ni kawaida sana, zingatia usafi wake, zingatia kusali pia jaribu hospital. Kama hakuna tatizo basi vumilia tu baada ya mda fulani ataacha. Inatesa sana, mm twins wangu wamekuja kutulia after 4 months.
 
Back
Top Bottom