Mtoto amepata maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kinyama kimetokea na kurudi ndani

jnbg

Member
Apr 12, 2016
77
49
Nina mtoto mdogo wa miaka 3½ ambaye siku ya Jana alikuwa analalamika wakti wa kujisaidia haja kubwa lakin baada ya masaa kadhaa alijisaidia kumbe alikuwa anapata maumivi ndani ya haja kubwa.

Wakati anajisaidia kilijitokeza kinyama laini ivi na alipomaliza kikarudi ndani na hali Kama iyo imejirudia tena leo wakti wa kujisaidia Hali ambayo imetupatia wasiwas mkubwa labda ndo Ugonjwa.

Naamini katika jukwaa hili Kuna watu huenda wame-experience tatizo Kama hili. Naombeni ushauri wa kitiba juu ya hili tatizo
Mungu awabariki sana.

Nawawasilisha
 
Mkuu mwanao anaonyesha anayo maradhi ya Bawasiri mpeleke hospitali akafanyiwe uchunguzi wa Ma-Daktari.
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
786813_f260.jpg



Vipimo na uchunguzi
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
 
Back
Top Bottom