Mtoto kutotoa haja kubwa tatizo nini?

loupa

Senior Member
Jul 22, 2016
121
72
Habari ndugu wana Jamii Health,

Mimi nina mtoto mwenye umri wa miezi 2 na wiki 2, tatizo la mtoto wangu ni kwamba hatoi haja kubwa, yaani ananyonya tu ila hakuna haja kubwa, ila mkojo anakojoa kama kawaida.

Sasa naomba wenye uelewa na hili labda tatizo ni nini? Nitumie mbinu/dawa gani mtoto awe katika hali ya kawaida?
 
Nitumie mbinu/dawa gani mtoto awe katika hali ya kawaida?
Usithubutu kamwe kumpa dawa mtoto kwa ushauri toka mtandaoni, Utahatarisha afya ya mtoto wako mpendwa

Kwa umri huo wa mtoto ni Daktari pekee ndio anapaswa kupendekeza na kutoa dawa stahiki kwa mtoto iwapo tu ataona kuna tatizo na inahitajika kutumika dawa.

Je nini unatakiwa kufanya | Ili kujiondoa na wasi wasi ulionao mpeleke mtoto hospitali inayoeleweka, onana na daktari na utashauriwa nini cha kufanya.
mwenye umri wa miezi 2 na wiki 2
=
 
Kuwa subra anapupu tu... Huwa inatokea hata wiki 2 bila haja... Ila atakwenda tu siku...

Ikishindikana tafuta mafuta ya mnyonyo chemsha kwenye kijiko kidogo.
 
Habari ndugu wana Jamii Health,

Mimi nina mtoto mwenye umri wa miezi 2 na wiki 2, tatizo la mtoto wangu ni kwamba hatoi haja kubwa, yaani ananyonya tu ila hakuna haja kubwa ila mkojo anakojoa kama kawaida.

∆ Sasa naomba wenye uelewa na hili labda tatizo ni nini?
∆ Nitumie mbinu/dawa gani mtoto awe katika hali ya kawaida?
kabla ya kutumia dawa yoyote ile mpeleke hospital dr ndo atakupa ushauri wa dawa na vyakul ambavyo unatakiwa kumpa mtoto
 
Kawaida tu Kwa watoto wachanga, kama anajampa Haina shida. Imewahi kunitokea Kwa mwanangu. Kabla sijaelimishwa na Dr nilijawa na wasiwasi.
 
mwanangu wa pili alikua anakaa hata wiki na masiku kadhaa bila kupoo nilikua nakua muoga sana sjawahi kuexperience hio kitu mama alikua akiniambia ni kawaida muhimu mcheulishe akishanyonya na akiwa anajamba kidogo ni nafuu lakini sasa nikawa nampa ile scotts maarufu kama mafuta ya samaki now yupo sawa kama unahofu mpeleke hospital
 
Chukua hatua mpeleke hospital mapema wenyew ndio watakupa ushauri mzuri hapa utapata uzoefu tu wa kumjaribia mtoto
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom