khaligraph
JF-Expert Member
- Nov 19, 2016
- 1,083
- 961
Watalaam wamemwambia n sahihi then wewe ambae sio mtalaam umasema sio sahihi...wabongo achen kuingilia taalum za wa2...Aisee mpaka nimesisimkwa na mwili wote, ndugu yangu kwa kifupi rudini hospital kiumbe kikatolewe.
Nilichoshuhudia mwaka jana kupoteza mtu kwa ushaur kama uliopewa nimetokea kuogopa hata kumuangalia mjamzito wa aina yoyote.
Nenda hospital kubwa zaid huyo dada akasaidiwe hicho kiumbe kitoke, msikubali kusubir siku 14(sina uhakika kama kitaalam ni sahihi)
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante sana,Ndo utaratibu ulivyo.
Kila kitu kina umuhimu wake, siku 14 zijipita kama ilishindikana ataenda hosp, then utaratibu wa kuzalisha utaanza, ukishindikana utaenda utaratibu mwingine.
Sasa unaporuka step moja, shida ikitokea ama ikishindikana next step ni way forward na ni more aggresive than previous.
Thats all I have to say.
Shukrani shukrani shukraniAchana na story za humu. Watu wanaongea wengi wao sio professionals. .
Mtoto akifia tumboni anaweza kaa tumbon had wiki 2 bila kusababisha tatizo lolote kwa mama.
Kama uchungu hautanza wenyewe in 2 weeks ndipo wanaanzisha dawa za uchungu. Lkn, sometimes hua inaleta psychological issues kwa mama, so, wataalam wengne hua wana opt kuanzisha uchungu right away lkn sio swala la dharura ikiwa ndan ya siku 14
Sent using Jamii Forums mobile app
Brother! Humu wengi wanakupa stress, wengi wanabwabwaja bila ufaham wowote wa mambo ya afya.
Trust me! Hayo maelezo ulopewa apo hospital tako sahihi..just chillup and wait!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Watalaam wamemwambia n sahihi then wewe ambae sio mtalaam umasema sio sahihi...wabongo achen kuingilia taalum za wa2...
Sent using Jamii Forums mobile app
Asa angalia...akili zako umesahau wap bro??Toa ujinga wako hapa,nimesema sio sahihi? Nishaweka angalizo kuwa ''sina uhakika kitaalamu kuwa ni sahihi'' na nikaeleza niliyoyaona kwa ushauri wa namna hiyo wewe unakuja na hekaya zako za ''wabongo''
Taaluma gani unaongelea bongo? Angalizo ni muhimu kuliko hicho unachokiita ''taaluma za watu''
Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi waliookolewa maisha yao je??Usikute kuna Watu wenye Mamlaka Wizara ya Afya wanafungua Uzi wanafunga na kwenda Jukwaa lingine....
Ningekua nna Mamlaka ningehakikisha namtumbua huyu Doctor/Nesi aliyetoa Maelekezo tajwa hapo juu!
Wameua watu wengi bila kujari kuwa Mishahara yao inatokana na Kodi za wakiwemo Wajawazito na Wagonjwa.....
Shenzi zao wenye Mamlaka!
Poleni sana...
Maelezo aliyopewa yanalingana na jinsi gani vipimo vya huyo shemeji yako vinasemaje....watu wanatofautiana sana.
Kuna wengine wanapata stillbrith wakiwa na matatizo mengine ya kiafya na hivyo kufanyiwa mtibabu tofauti na wengine.
Inapaswa shemeji yako awe anachunguzwa kila baada ya masaa 48 na sio kusema aende nyumbani hizo siku 14 asirudi hospitali mpaka apate uchungu.
Hii itasaidia kutambua kama kutakuwa na maambukizi yoyote kwa mama na pia kuweza kujua afya ya akili ya mama.
Kwa wale ambao wangependa kufanya uchunguzi wa kujua sababu ya mtoto kufa , basi itabidi atolewe mapema ili asiharibike sana , uchunguzi ukashindwa kubaini sababu ya kifo...kwa manufaa ya kuzuia vifo vingine mbeleni.
Mkuu mimj ni moja ya medical practioner ndiyo maaba nakwambia nenda hosp kitolewe kiumbe
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenifanya nikumbuke maumivu ya kumpoteza dada yangu sababu ya mtoto kufia tumboni
Mkuu Fanya hima nenda Hosp zinazoeleweka vinginevyo yasije wakuta yaliyotukuta
Sent using Jamii Forums mobile app
Aise pole sana mimi nazijua kesi mbili ambazo na wahusika nawajua
Moja iliishia vibaya sana
Mmoja alipata ujauzito wa kwanza na hakujua kuwa Mtoto amefariki mpaka baada ya muda na miezi ilikuwa imeenda
Lakini bahati alisafishwa ingawa hakujaaliwa kupata mtoto tena
Mwangine ni kama unavyoogopa
Huyo mtoto wake aliozea tumboni na kusababaisha akatwe miguu miwili na mkono kwani ilikuwa imeharibika sana na kuoza
Mungu mkubwa wote bado wako hai
Ila ndio hivyo tena
Mpeleke private akasafishwe achana na gov hospital kama wanazingua
Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hospital makini ikitokea hivyo mama huwekewa kidonge cha uchungu chini kisha kuambiwa afanye mazoezi ya kupanda ngazi na kutembea ili uchungu uje, dalili za uchungu zikianza anawajulisha kisha njia ikifunguka wanamwingiza leba kiumbe kinatolewa mara moja!
Hayo mambo ya kumwambia mama ambae ameshakuwa disappointed eti nenda kasubiri hadi siku 14 haingii alikini kabisa !
So what?
Anyway
Sent using Jamii Forums mobile app
Ireland women
Hawakutoa Option, maelezo niliyo toa ndio tuliyopewaShukrani....imejielezea vizuri.
Nina mashaka kama ni utaratibu ulioko Tanzania, maana ukifuatilia maelezo yamtoa mada...Shemeji yake hakupewa nafasi ya KUCHAGUA njia iliyo rahisi kwake kukabiliana na tatizo lililomtokea.