Mtoto aliyezamia ndege Zanzibar aanika uchawi wake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,325
33,131
[
attachment.php

SAKATA la mtoto Happiness (10) aliyetikisa kwa tukio la kupanda ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar bila kujulikana limeibuka tena, safari hii katika sura mpya kufuatia mtoto huyo kufungua kinywa chake na kuanika mambo ya kichawi, Uwazi lina mkanda mzima.



attachment.php

Happiness (10) anayeishangaza jamii kwa matukio ya kimazingara.


Mtoto huyo aliyaanika mambo hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki na kumfanya afande huyo kupigwa butwaa. Aidha, alizungumza na Uwazi, nyumbani kwao, Mkuranga.


ALICHOSEMA AWALI NI HIKI
Awali akizungumza kwa kujiamini, mtoto huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mkokozi Kata ya Vikindu wilayani Mkuranga, Pwani, alikiri kusafiri kwa ndege hadi Zanzibar akidai alikwenda kumfuata baba yake mzazi aishiye huko.


Hata hivyo, mama yake mzazi, Sarah Zefania alimpinga mwanaye huyo na kusema: "Baba yake haishi Zanzibar, yupo Kipunguni (Ilala jijini Dar es Salaam)."






Mtoto Happiness akiwa na mama yake

KUHUSU UCHAWI

Mtoto Happiness alikwenda mbele zaidi kwa kujiongeza akisema katika maisha yake amekuwa akifanya mambo ya kishirikina lakini si peke yake. Alisema ana mshirika wake (hakumtaja jina).

Happiness aliutaja ushirikina huo. Alisema amekuwa akisafiri usiku mara kwa mara na mshirika wake huyo wa karibu kwa kutumia usafiri wa ungo!!

ATAJA PAKA, NYOKA NA MBUZI.

Kama vile haitoshi, mtoto huyo ambaye ametokea kushangaza wengi huku akipachikwa majina ya ‘mtoto wa ndege', ‘mtoto wa uchawi' na ‘mtoto wa miujiza', alisema akiwa katika safari hizo amekuwa akiwaona paka, nyoka na mbuzi.

AFIKA POPOTE BILA KUJALI UMBALI.

Aliongeza kuwa, kwa kutumia ungo na huyo mshirika wake, wamekuwa na uwezo wa kufika popote wanapopataka bila kujali umbali.


MAVAZI YA SAFARINI.

Akizidi kufunguka, Happiness alisema mara nyingi wanapokuwa katika safari hizo ambazo alisema watu hawawezi kuwaona, huvaaa nguo nyeupe, nyeusi au wakati mwingine nguo nyekundu ili kufanikisha masuala yake ya usiri.

Mtoto huyo aliyasema hayo kufuatia Septemba 16, mwaka huu kudakwa tena maeneo ya Feri jijini Dar akiwa na begi ambapo alisema anamfuata baba yake (hakusema wapi).

Baada ya walinzi wa eneo hilo kumgundua ni ‘mtoto wa ndege' walimfikisha Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar ambapo mama yake aliitwa.

Mama alishtuka baada ya kumwona mwanaye akiwa amebeba begi lililokuwa na nguo kwa madai ya kuwa alikuwa akielekea kwa baba yake mzazi.



attachment.php


Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Dar, SACP Mary Nzuki

SIKU YA KUTOROKA MARA YA PILI
Akisimulia kisa cha kutoroka mara hii ya pili, Happines alisema siku ya tukio mtu mmoja ambaye alidai kuwa ni kaka yake wa kambo alifika nyumbani na kumchukuwa yeye na begi lake la nguo akidai anampeleka kwa baba yake Zanzibar lakini baada ya kufika Feri mtu huyo alitokomea kusikojulikana.

KAULI YA MAMA

Wakati mama huyo (pichani) akizungumza na Uwazi alimtaka baba wa mtoto huyo, Julius kujitokeza ili kunusuru hatima mbaya ya mtoto wao.

WACHUNGAJI WANENA

Waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho nchini ili wazungumzie tukio la mtoto huyo.


NI MAPEPO
Mchungaji wa Kanisa la Paradise International la jijini Dar, Gideon Parapanda alisema tatizo linalomsumbua mtoto huyo ni pepo mchafu wa kuzimu hivyo kwa kutumia maombi ndani ya makanisa hali hiyo itatoweka.

"Happiness kama alizaliwa salama na hali hiyo imemkuta ukubwani na kufanya mambo ambayo hayaeleweki ni pepo wachafu ambapo akimtumainia Yesu tatizo hilo litaisha mara moja," alisema Mchungaji Parapanda.

WAZAZI WASIENDE KWA WAGANGA

Naye Mchungaji wa Kanisa la Cathedral of Joy, pia ni Nabii John Komanya, yeye alisema Happiness anasumbuliwa na pepo wachafu, kitu pekee ni maombi na alitahadharisha wazazi au ndugu wasiende kwa waganga wa kienyeji.

ASKOFU KAKOBE ATAKA APELEKWE FULL GOSPEL

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe yeye alisema matatizo ya Happiness yataisha kwa Jina la Yesu kama ndugu, walezi au wazazi wataamua kumfikisha kanisani kwake.

"Kinachomsumbua mtoto huyo ni roho chafu, akiombewa katika makanisa ya kiroho atafunguliwa, hata kama ndugu wakiamua kumleta hapa Full Gospel ni sawa tu, atakombolewa," alisema Kakobe.

Chanzo: GPL

 

Attachments

  • mtoto.jpg
    mtoto.jpg
    70.3 KB · Views: 2,182
  • 3333.jpg
    3333.jpg
    62.5 KB · Views: 2,164
  • mfuko.jpg
    mfuko.jpg
    96.2 KB · Views: 1,483
  • RPC maryNzuki.jpg
    RPC maryNzuki.jpg
    34.8 KB · Views: 2,119
  • kakobe.jpg
    kakobe.jpg
    22.7 KB · Views: 1,465
Wazazi wake wanayo siri na majibu, yaonesha huyu wa kipunguni siyo biological father, mama alichepuka sasa anaumbuka sababu spirit ya mtoto iko kwa biological father ambaye hajui aliko, ndiyo maana hata baba wa kipunguni hatoi ushirikiano. Bora mama awe mkweli amtaje biological father wa mtoto ili spirit yake itulie.
 
Tanzania kwa mazingaombwe...........akili zote zinahamia huko,hakuna hata wa kufikiri kwa upana zaidi, yale yale ya LOLIONDO.
 
kuamini mtuu ana paa angani naungo bado sana mmmmh watu wanavyo tamani kuende sehemu tofauti na alipo akajione tu hapati usafiri iweje ujeni ambia mtuu ana paa na ungo...... mpaka kesho sito aminii....
 
kuamini mtuu ana paa angani naungo bado sana mmmmh watu wanavyo tamani kuende sehemu tofauti na alipo akajione tu hapati usafiri iweje ujeni ambia mtuu ana paa na ungo...... mpaka kesho sito aminii....

sasa kwa taarifa yako leo asubuh nilikuwa CHAD Na Nimerudi Ndani Ya Dakika 27
 
kwa nn mnapaa kwenda usiku kurudi alfajiri.? Na isiwe kwenda na krudi any time.

naiti mazingira huwa tulivu sana halafu netwek inashika kinyama sana!

jaribu. nchana uone!
 
Back
Top Bottom