Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwaka 2004 ndipo Mkuu Freeman Mbowe alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA.
Mtoto aliyezaliwa mwaka huo, mwaka huu anafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Kwa maneno mengine huu mwaka 2017 ni wa 13 wa uongozi wa Kaka Mbowe.
Taratibu siku zinasogea, ikifika January 2018 utakuwa ni mwaka wa 14 kwenye uongozi.
Unaposema JPM ni one man show inabidi pia uwe na ujasiri wa kusema CHADEMA ni one man party. CHADEMA inahitaji damu mpya, akili mpya, fikra mpya, na yote hayo kutoka kwa uongozi mpya.
Achana na habari kwamba siasa zimepigwa marufuku, maishani binadamu ili afanikiwe ni lazima awe na sifa ya kubadilika kutokana na wakati usiomsubiri mtu.
Wazungu husema adaptability, uwezo wa kufanana na mazingira yanayokuzunguka haswa jinsi yanavyobadilika.
Ifike mahali mwana CHADEMA mwenye kupenda mabadiliko awe tayari kujenga hoja kwenye mikutano ya ndani, juu ya umuhimu wa chama kupata visions mpya.
Uhai wa CHADEMA ndio uhai wa CUF na ndio uhai wa CCM, twende mbele turudi nyuma.
2017 uwe ni mwaka ambao mwenye kupenda afya ya siasa ya Tanzania na awe wa kwanza kuanzisha vuguvugu la mabadiliko ya kweli ndani ya CHADEMA.