Mtoto Akataa shule; Bora aende jela

Sawa ila nilichokua nasema ni huyo mtoto atajutia mbelen maana kama anaacha shule kabla hajajua kusoma na kuandika ni hasara kwake
 
Dunia nzima watu wote wakiwa na mawazo kama yako basi Dunia itarudi kwenye maisha ya enzi za ujima.
 
Kwa maoni hayo dogo yupo sahihi kabisa
 
Huyo dogo inaonekana anajua kusoma na kuandika maana hapo pembeni naona kitabu kama cha physics atakua dogo wa kidato huyo.
Ni maoni yangu lakini.
 
Wazo zuri ngoja tuone ila dogo labda maisha ya shule yanamtesa maana kule nako dah
 
Dunia imebadilika Sana.Diamond angesoma asingemiliki rose royce.
Samatta angesoma asingemiliki ghorofa.
Bakresa angesoma asingekuwa milionea
 
Wazo zuri ngoja tuone ila dogo labda maisha ya shule yanamtesa maana kule nako dah
Dogo kaamua akapige singeli inalipa kuliko shule.
Elimu sahihi ni form four kisha ingia mtaani upate elimu ya maisha.
Kusoma zaidi ni kujitakia umasikini
 
Tuache kujidanganyaa humuu, basic education ambayo dogo anaikosa ni muhimu..
Advance na degree sawa hapo nakubali waweza utemane nako ila angalau basi form four,

Asaivi hata ukiishia st7 utapoteana, kwa nature ya maisha ya sasa ile tunaiita elimu ya msingi jina tuu ila 4m4 ndio ingekua ya msingi(basic), std 7 ingekua elimu ya awali...
Kinyume na hapo subiri kujiendeleza baadae au kubali kupigwa kwenye mambo mengi..
 
Haja kanaweza kujiua kama watakalazimisha,waheshimu mawazo yake.

Maana elimu haina mwisho,kakija kushtuka baadae katarudi shule.
Hilo na neno maana kamepanic kinoma
 
Ila hapo kwa namna nyingine dogo yupo sahihi kabisa
 
Wakapeleke pale Soweto kwenye gereza la watoto mbeya jiji anakaa wiki moja akirudi atatulia shule.
 
Best wewe ticha?
 
Ujuzi gani mkuu, samahani tufungue.
 
Sawa ila nilichokua nasema ni huyo mtoto atajutia mbelen maana kama anaacha shule kabla hajajua kusoma na kuandika ni hasara kwake
Kusoma kuhesabu na kuandika sio lazima ujifunzie shule. Nyumbani kwangu kuna mdada alikuja hakuwahi pelekwa shule na wazazi wake, amejifunzia kusoma nyumbani tena mtoto wangu wa darasa la 3 ndio aliemfundisha. Mimi kazi yangu tu kuwapa vitabu vinavyoendana .
 
Huyo mwanao nae kajifunzia home?Watu wagumu sana kuelewa kama unaona elimu haifai mkatishe masomo mwanao wa darasa la tatu. Huoni hausigeli kaona umuhimu wa elimu mpaka kafanya bidii ajue kusoma na kuandika
 
Mbona unajichanganya mkuu? Kwani huyo dogo amekataa shule akiwa form 6?
 
Huyo mwanao nae kajifunzia home?Watu wagumu sana kuelewa kama unaona elimu haifai mkatishe masomo mwanao wa darasa la tatu. Huoni hausigeli kaona umuhimu wa elimu mpaka kafanya bidii ajue kusoma na kuandika
Umeona sehemu nimeandika elimu haina umuhimu. Elewa mantiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…