Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Mtoto ALEX FREDRICK SANGA, mwaka mmoja na miezi saba, mkazi wa mapinduzi alikutwa amefariki dunia kwenye korongo lenye maji ambalo lipo jirani na nyumbani kwao
Tukio limetokea mnamo tarehe 18.03.2019 saa 15:45 alasiri huko katika Kitongoji cha Mapinduzi, Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya.
Marehemu alikuwa akicheza na wenzake wakati mama yake akiwa anafua nguo na baada ya muda kama dakika 15 akawa hamuoni mwanae na ndipo alipoanza kumtafuta kwa kushirikiana na majirani zake na wananchi wengine na hatimaye kufanikiwa kumpata akiwa amefariki dunia kwenye dimbwi la maji.