mourisous
JF-Expert Member
- Jan 19, 2016
- 443
- 269
TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU WA KUSIKITISHA ILI KINA MAMA WOTE WAUSOME NA KUBADILIKA.
Leo tarehe 27-04-2017 kuna dada amefiwa na mwanae wa miaka miwili aliyekuwa amelazwa hospitali kuanzia siku ya Ijumaa Kuu. Hapa Jijini Dar es Salaam.
Chanzo cha kifo cha mtoto huyu ni kutokana na mama yake kumsuka nywele mtindo wa DREAD ambapo nywele zinasukwa kwa kusokotwa sana.
Mtoto alisukwa siku ya kwanza lakini hakumalizwa. Siku ya pili Alhamisi akamaliziwa kusukwa. Siku ya Ijumaa ambayo ndo ilikuwa Ijumaa Kuu mtoto alianza kuumwa mwili mzima.
Walipoona anazidi kuumwa wao wakahisi nywele walivyombana itakuwa chanzo wakaanza kumnyoa haraka. Lakini wakiwa wanaendelea kumyoa hali ikazidi kuwa mbaya wakampeleka hospitali hivyohivyo bila kummalizia kumnyoa.
Walipofika hospitali daktari aliwagombeza sana kwa kumsuka mtoto kwa kumvuta kiasi hicho nywele zake. Alianza matibabu na walimalizia kumnyoa nywele.
Hali iliendelea kuwa mbaya akawekewa mashine ya kumsaidia kupumua. Bahati mbaya mchana wa leo mtoto kafariki.
Chanzo cha kifo kinasemekana misuli ya kichwa ilivutika kwa kiwango kikubwa ikapelekea matatizo mengine yaliyosababisha kifo.
FUNZO: Kina mama acheni kuwafanyia watoto wenu mambo ya watu wazima. Waacheni watayafanya wao kwa muda wao. Waacheni waishi maisha ya kitoto. Madai yenu ya kwenda na wakati ndo matokeo yake haya.
MUNGU ATUSAIDIE.