Mtindo wa Magufuli ni moja ya dawa ya matatizo yetu

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
4,108
Points
2,000

Patriot

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
4,108 2,000
Kwa maoni yangu, tuliposhindwa kuunda katiba mpya ilikuwa ni ishara ya utawala mbovu kabisa! Kwamba Bunge na Serikali vyote vilikuwa viko taaban!

Yawezekana biashara ya Ndege ni mbaya lakini kila taifa hutamani kuwa na ndege chache. Treni ni muhimu pia. Tujiulize Ilikuwaje kwa miaka yote hiyo tukashindwa kununua ndege hata moja? Ilikuwaje miaka yote watoto mashuleni wakakosa madawati? Hatukuwa na mradi wowote wa maana kwa miaka yote hiyo na bado bajeti ikapanda kufikia zaidi ta trilioni 22!

Tatizo letu kubwa ilikuwa ni wizi. Kwa kuanza kufukuza na kuzuia wizi ni hatua muhimu. Wezi bado ni wengi lakini hiyo ni ishara ya kufahamu matatizo yako wapi.
 
UCD

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2012
Messages
6,212
Points
2,000

UCD

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2012
6,212 2,000

Good thread!
 
Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
1,164
Points
2,000

Zygot

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
1,164 2,000
Ni kweli! Ukiangalia bajeti yetu ya nyuma unaona trilioni zikiongezeka. Lakini hakuna mradi wa kitaifa unaoweza kuonesha kwamba ndo ulimeza peza hizo zote. Ni kama tulikuwa taifa la zezeta! Sorry!

Angalia bunge la katiba! Yaani bunge zima hawakuona njia ya kupata katiba. Vipofu hawa wakatukanana hadi mwisho. Wakasema wanataka muda wa nyoingeza. Serikali nayo ikawa na watu vipofu wasioona wapi tunakwenda, ikaongeza muda na pesa. Mwisho hakuna katiba. Mijitu hiyo iliyoshindwa kupata katiba, ikahamia kwenye fomu za urais ikitaka kututawala! FOOOOOL!
 
Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,857
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,857 2,000
Unachosahau ni kwamba Chama kinachounda serikali ni kile kile na waliokuwa wakiibia wananchi ni wale wale waliokuwa viongozi katika chama kile kile na serikali hiyo hiyo. Waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho hicho na serikali, Rais wa sasa aliapa kuwalinda kwa hivyo waishi kwa raha bila hofu kwani hakuna wa kuwabughudhi.

Kwa miaka zaidi ya ishirini alishirikiana nao bega kwa bega kama Waziri akitekeleza kwa juhudi mkubwa mipango ya serikali ambayo iliifikisha taifa katika hali hiyo unayoilalamikia. Je amewahi kuwataka radhi wananchi kwa wizi na ufiisadi uliokuwa ukiendelezwa na serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake akiitumikia kwa muda wote huo?

Eti utetezi ni kuwa hakuwa Rais nyakati hayo yote yakiendelea ndani ya taifa hili…unasikitisha, unashangaza na unaudhi.
Mijitu hiyo iliyoshindwa kupata katiba, ikahamia kwenye fomu za urais ikitaka kututawala! FOOOOOL!
Je mijitu hiyo ni pamoja na Rais wa sasa?
 
tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Kwa maoni yangu, tuliposhindwa kuunda katiba mpya ilikuwa ni ishara ya utawala mbovu kabisa! Kwamba Bunge na Serikali vyote vilikuwa viko taaban!

Yawezekana biashara ya Ndege ni mbaya lakini kila taifa hutamani kuwa na ndege chache. Treni ni muhimu pia. Tujiulize Ilikuwaje kwa miaka yote hiyo tukashindwa kununua ndege hata moja? Ilikuwaje miaka yote watoto mashuleni wakakosa madawati? Hatukuwa na mradi wowote wa maana kwa miaka yote hiyo na bado bajeti ikapanda kufikia zaidi ta trilioni 22!

Tatizo letu kubwa ilikuwa ni wizi. Kwa kuanza kufukuza na kuzuia wizi ni hatua muhimu. Wezi bado ni wengi lakini hiyo ni ishara ya kufahamu matatizo yako wapi.
Sikatai Utetezi wako, lakini bado sioni kama Magufuli ni suluhisho la matatizo yetu. Huenda Magufuli amehama kutoka kwenye matatizo ya watangulizi wenzake kadhaa, lakini naona anapandikiza tatizo lingine ambalo litakuwa tatizo kubwa sana baada ya muda fulani. Ukiona kiongozi anaua mifumo yote ya ushindani na kuleta mifumo ya ukiritimba, basi jua kiongozi huyo anapandikiza tatizo ambalo litatugharimu si chini ya miaka 20 ijayo. Huu mtindo wa Magufuli kuongoza ndio alioutumia Nyerere, ambao dakika za mwisho tulikuja kunasa mpaka watu kuishia kuvaa viraka.

Kwasasa sio rahisi madhara hayo kuonekana kwani sasa hivi kusifia ndio fashion, na hakuna ruhusa ya mawazo mbadala kuonekana hadharani. Inaonekana watanzania tumesahau au hatujifunzi kuacha kutumia mawazo ya mtu mmoja kuwa ndio muelekeo wa nchi. Kwa Nyerere tuliona mawazo yake yalivyoabudiwa, lakini alikwama vibaya, na hata alipotoka karibu ya vyote alivyoacha navyo vilikufa.
 
Bome-e

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
11,539
Points
2,000

Bome-e

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
11,539 2,000
Unachosahau ni kwamba Chama kinachounda serikali ni kile kile na waliokuwa wakiibia wananchi ni wale wale waliokuwa viongozi katika chama kile kile na serikali hiyo hiyo. Waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho hicho na serikali, Rais wa sasa aliapa kuwalinda kwa hivyo waishi kwa raha bila hofu kwani hakuna wa kuwabughudhi.

Kwa miaka zaidi ya ishirini alishirikiana nao bega kwa bega kama Waziri akitekeleza kwa juhudi mkubwa mipango ya serikali ambayo iliifikisha taifa katika hali hiyo unayoilalamikia. Je amewahi kuwataka radhi wananchi kwa wizi na ufiisadi uliokuwa ukiendelezwa na serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake akiitumikia kwa muda wote huo?

Eti utetezi ni kuwa hakuwa Rais nyakati hayo yote yakiendelea ndani ya taifa hili…unasikitisha, unashangaza na unaudhi.
Je mijitu hiyo ni pamoja na Rais wa sasa?
Umemaliza,uzi umepata majibu mujarabu kabisa!Case closed!
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
47,289
Points
2,000

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
47,289 2,000
I hate CCM. Chama kina uchawiuchawi mwingi. Mara Mwenge, mara waje kucheza uwanjani na fisi, mara wachawi 1000 wa Gamboshi waseme watamuua mtu yeyote atakaje mpinga Magundu, halafu magindu naye hakupinga wala kukemea kauli ya tamko la uchawi.
Hili kundi la wachawi bila Shaka ndilo linaongoza jahazi letu
 
Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
12,386
Points
2,000

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
12,386 2,000
Hili jambo limeandikwa katika hali ya ajabu sana. Kama alivyosema Mag3 hivi hizo serikali "Zilizopita" zilikuwa zinaundwa na chama gani kama siyo CCM na jee Magufuli hakuwa sehemu ya serikali hizo?

Haya "maendeleo" tunayoyaona sasa hayazuii mambo mengine kufanyika na je ni kwa kiasi gani kwa sasa kuna ule uhuru wa kuonesha upande mbovu wa hayo "maendeleo" yanayofanywa?

Enzi za serikali hizo "Zilizopita" uhuru wa kuzungumzia mambo kama EPA, Tangold, Meremeta na hata Escrow zilikuwa zinajadiliwa kwa uwazi kwenye vyombo mbali mbali vya habari. Jee ile ripoti ya CAG ilijadiliwa kuwa uwazi kiasi gani?

Kama maendeleo ni maelezo tu yanayotolewa na serikali pekee, basi ni lazima mizania ya kupima hayo maendeleo haitakuwepo.
 
Kuchitimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Messages
255
Points
250

Kuchitimbo

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2019
255 250
Waombe Sana Mungu wao usiku na mchana ili huko mbeleni nisiwe Rais wa hii nchi,vinginevyo watajuta,nitaamrisha viongozi wote kuanzia mawaziri na kupanda juu kukamatwa na kuswekwa ndani,waeleze walifanya Nini hapa Tz,wakinipa majibu ya hovyohovyo Ni kifungo cha maisha na Kama Yuko kaburini pia atapigwa kifungo.
Hawa watu wa kijani Bora uishi na mifisi ndani
 
Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
4,108
Points
2,000

Patriot

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
4,108 2,000
Unachosahau ni kwamba Chama kinachounda serikali ni kile kile na waliokuwa wakiibia wananchi ni wale wale waliokuwa viongozi katika chama kile kile na serikali hiyo hiyo. Waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho hicho na serikali, Rais wa sasa aliapa kuwalinda kwa hivyo waishi kwa raha bila hofu kwani hakuna wa kuwabughudhi.

Kwa miaka zaidi ya ishirini alishirikiana nao bega kwa bega kama Waziri akitekeleza kwa juhudi mkubwa mipango ya serikali ambayo iliifikisha taifa katika hali hiyo unayoilalamikia. Je amewahi kuwataka radhi wananchi kwa wizi na ufiisadi uliokuwa ukiendelezwa na serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake akiitumikia kwa muda wote huo?

Eti utetezi ni kuwa hakuwa Rais nyakati hayo yote yakiendelea ndani ya taifa hili…unasikitisha, unashangaza na unaudhi.
Je mijitu hiyo ni pamoja na Rais wa sasa?
Ukianza kusema chama ni kile kile, utawala ni ule ule, itafikia wakati utaona hakuna haja maana ukiendelea kidogo tu utasema watanzania ni wale wale! Ikimaanisha aje CUF, ACT au yeyote mambo ni yale yale! Kuna haja gani ya kupiga kelele wakati hata vyama vya upinzani vilianzishwa na wana CCM waliohama? Si ni wale wale!
 
Mugabe one

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2016
Messages
1,968
Points
2,000

Mugabe one

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2016
1,968 2,000
Ni kweli! Ukiangalia bajeti yetu ya nyuma unaona trilioni zikiongezeka. Lakini hakuna mradi wa kitaifa unaoweza kuonesha kwamba ndo ulimeza peza hizo zote. Ni kama tulikuwa taifa la zezeta! Sorry!

Angalia bunge la katiba! Yaani bunge zima hawakuona njia ya kupata katiba. Vipofu hawa wakatukanana hadi mwisho. Wakasema wanataka muda wa nyoingeza. Serikali nayo ikawa na watu vipofu wasioona wapi tunakwenda, ikaongeza muda na pesa. Mwisho hakuna katiba. Mijitu hiyo iliyoshindwa kupata katiba, ikahamia kwenye fomu za urais ikitaka kututawala! FOOOOOL!
Mmmh, umenikumbusha jamaa wa bunge la katiba alijilipa Pesa za kufulu mpaka nataka kutapika yaani watz tuko hovyo sana! MAGUFULI KANYAGA GIA TWENDE MBELEE!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
1,164
Points
2,000

Zygot

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
1,164 2,000
Unachosahau ni kwamba Chama kinachounda serikali ni kile kile na waliokuwa wakiibia wananchi ni wale wale waliokuwa viongozi katika chama kile kile na serikali hiyo hiyo. Waliokuwa viongozi wakuu wa chama hicho hicho na serikali, Rais wa sasa aliapa kuwalinda kwa hivyo waishi kwa raha bila hofu kwani hakuna wa kuwabughudhi.

Kwa miaka zaidi ya ishirini alishirikiana nao bega kwa bega kama Waziri akitekeleza kwa juhudi mkubwa mipango ya serikali ambayo iliifikisha taifa katika hali hiyo unayoilalamikia. Je amewahi kuwataka radhi wananchi kwa wizi na ufiisadi uliokuwa ukiendelezwa na serikali ambayo yeye alikuwa sehemu yake akiitumikia kwa muda wote huo?

Eti utetezi ni kuwa hakuwa Rais nyakati hayo yote yakiendelea ndani ya taifa hili…unasikitisha, unashangaza na unaudhi.
Je mijitu hiyo ni pamoja na Rais wa sasa?
Utawala huwa ni mtu, pamoja na kwamba tunapenda kutumia neno chama. CUF ya Lipumba ni tofauti na ile ya wakati wa Maalimu. CCM ya nyerere ni tofauti na ile ya Kikwete na Magufuli. CHADEMA ya Mbowe na Mnyika siyo ile ya Slaa wa mwembeyanga. Nenda nje; Republican ya Trump siyo ya Bush!

Una jipay?
 
Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
1,164
Points
2,000

Zygot

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
1,164 2,000
Mmmh, umenikumbusha jamaa wa bunge la katiba alijilipa Pesa za kufulu mpaka nataka kutapika yaani watz tuko hovyo sana! MAGUFULI KANYAGA GIA TWENDE MBELEE!

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti Sita akajiita samaki aliyerudi majini! Aliishia kutafuna pesa na majigambo ya kibwege tu! Baadaye naye akajitokeza na basi lake mikoani akitafuta sahihi za kuwa rais wa nchi. Ahkika nchi inaweza tawaliwa na mtu mzembe!
 
Livejr

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Messages
1,380
Points
2,000

Livejr

JF-Expert Member
Joined Feb 6, 2014
1,380 2,000
Kwa maoni yangu, tuliposhindwa kuunda katiba mpya ilikuwa ni ishara ya utawala mbovu kabisa! Kwamba Bunge na Serikali vyote vilikuwa viko taaban!

Yawezekana biashara ya Ndege ni mbaya lakini kila taifa hutamani kuwa na ndege chache. Treni ni muhimu pia. Tujiulize Ilikuwaje kwa miaka yote hiyo tukashindwa kununua ndege hata moja? Ilikuwaje miaka yote watoto mashuleni wakakosa madawati? Hatukuwa na mradi wowote wa maana kwa miaka yote hiyo na bado bajeti ikapanda kufikia zaidi ta trilioni 22!

Tatizo letu kubwa ilikuwa ni wizi. Kwa kuanza kufukuza na kuzuia wizi ni hatua muhimu. Wezi bado ni wengi lakini hiyo ni ishara ya kufahamu matatizo yako wapi.
Nimeshindwa kuelewa kabisa ulikuwa unataka kumaanisha nini? Au Rais Magufuli ni bora zaidi?

Kama umeshindwa kufikiria ni kwamba, Biashara yoyote lazima iwe na faida usingesema kuhusu ndege. Yaan unazungumzia suala la ndege kwa kuwa tu ni ufahari na sio biashara.

Ungeniambia upo Mkoa/Mtaa/kijiji gani ningekuambia nenda shule fulani ukaone watoto wamekalia mkeka na wengine mawe au tofali na pia wapo ambao wanasomea nje na wengine wanaingia kwa shift.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,390,951
Members 528,310
Posts 34,067,712
Top