Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

  Mwandishi Wetu
  Raia Mwema
  Novemba 25, 2009
  [​IMG]Kikwete yaanza kumshinda

  [​IMG]Sasa hata Dk. Shein azoza  SIKU chache tu baada ya kutuma ujumbe kwamba akipita mwakani hatabeba mawaziri wazee, Rais Jakaya Kikwete ameanza kutekeleza azma hiyo kwa kuwatangazia mawaziri wake kwamba amechoshwa nao kwa kuwa hawamsaidii, imefahamika.

  Habari ambazo Raia Mwema imepata zinasema kwamba Rais Kikwete na hata wasaidizi wake, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wamekuwa wakali isivyo kawaida yao katika vikao vyao vya kazi.
  Kwa mujibu wa habari hizo, katika kipindi kiasi cha wiki mbili zilizopita, Rais Kikwete amekutana na mawaziri wake mara mbili na katika vikao hivyo amesema waziwazi kwamba mawaziri wake hawamsaidii kama alivyotarajia wakati akiwateua.


  "Hakikua kikao cha baraza, lakini alizungumza kwa ukali akiwaambia kwamba alipowateua alikuwa na matumaini makubwa nao kwamba atakuwa amepunguza kwa kiasi kikubwa uzito wa kazi.
  "Akawaambia amekuwa akilazimika kufanya mambo mengi ambayo yangeweza kufanywa na mawaziri wake aliowaamini na akawapa dhamana," anaeleza ofisa mmoja wa serikali aliyezungumza na Raia Mwema wiki kwa masharti ya kutotajwa gazetini.

  Mtoa habari huyo amesema wiki iliyopita Rais Kikwete alikuwa mkali kwa wasaidizi wake kuliko ilivyopata kutokea tangu aingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2005.

  Imefahamika kwamba kabla ya kikao cha wiki iliyopita, kilichofanyika nje ya Dar es Salaam, Rais Kikwete aliwaita mawaziri wake ghafla katika hatua ambayo ilizua hofu miongoni mwao wakiamini kwamba huenda alitaka kuvunja Baraza lake.

  Habari zaidi zinasema katika kikao cha awali waziri mmoja mwanamke alikwepa kuhudhuria baada ya kupata fununu kwamba Rais Kikwete alikuwa amekerwa na baadhi ya kauli zake za hivi karibuni.

  Habari zinaeleza kwamba, hata Dk. Shein ambaye anafahamika ya kuwa mara nyingi hana hulka ya ukali amebadilika, na sasa naye ameanza kuwa mkali waziwazi katika vikao vya utendaji.
  "Kuna kikao kimoja ambacho baada ya Rais kumbana waziri mmoja kutokana na kuwasilisha waraka uliokuwa umejaa mapungufu, Makamu naye alizungumza kwa ukali akimtaka waziri huyo kuacha kufanya mambo bila kufuata taratibu," anasema mtoa habari huyo.

  [​IMG]

  Dk. Shein

  Anaongeza: " Katika kikao hicho Rais alimkatiza waziri huyo mara kwa mara akitaka ufafanuzi na wakati mwingine kumlazimisha waziri huyo kubadili baadhi ya mambo ambayo aliona yana makosa mengi katika waraka wake.”


  Ukali wa ghafla wa Rais Kikwete, Dk. Shein na Pinda unatajwa kuwa umechochewa na utendaji usioridhisha wa mawaziri wengi unaosababisha viongozi hao wa juu kabisa kulazimika kufanya kazi ya ziada.
  Katikati ya habari hizo ni hali kwamba mawaziri wengi wanashindwa kuitetea na kuisimamia Serikali ndani na nje ya Bunge, mbele ya umma na katika shutuma nyingi zinazotajwa kwenye vyombo vya habari. Anasema mtoa habari huyo: "Rais alieleza wazi kwamba anakerwa na taarifa za mara kwa mara katika vyombo vya habari zikionyesha udhaifu mkubwa wa Serikali yake huku wasaidizi wake wakiwamo mawaziri wakishindwa kutoa hoja zenye nguvu au mkakati mahususi wa kukabiliana na taarifa hizo.”

  Japo tathmini inaonyesha kwamba si rahisi katika muda mfupi uliobaki kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kuwa na mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, Raia Mwema imearifiwa ya kuwa tayari mchakato umeanza ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa wa kuchunguza mienendo ya watu wakiwemo wajumbe wa sasa wa Baraza la Mawaziri na wajumbe watarajiwa ikibidi kufanyika kwa mabadiliko.

  Habari zaidi zinaeleza kwamba yamekuwapo mapendekezo kwa Rais Kikwete ya kutaka abadili baadhi ya mawaziri waliopo kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitajwa kuwa wako msitari wa mbele katika inayotajwa kuwa ni vita ya ufisadi katika hatua ya kukisafisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika tuhuma za ufisadi na migawanyiko ya dhahiri ili kuvutia kura katika uchaguzi wa mwakani.
  Mbali ya kuingiza sura mpya na kupunguza baadhi ya mawaziri, kuna taarifa kuwa yapo mapendekezo kwa Rais ya uwezekano wa kupandisha ngazi naibu mawaziri walioonyesha uwezo mkubwa.

  Haya yakiendelea zimekuwapo taarifa za wizara mbalimbali ambako wafanyakazi wanawalalalimikia mawaziri wao kwa utendaji kazi usioridhisha.

  Kati ya waliotajwa na wafanyakazi hao ni pamoja na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati; Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya na Naibu wake, Dk. Makongoro Mahanga; Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sophia Simba.

  Lakini akizungumza na Raia Mwema wiki iliyopita Chiligati alisema “hawezi kufanya mtihani na kujisahihishia mwenyewe.”
  “Hayo maoni ya watu siwezi kuyaingilia, mimi siwezi kufanya mtihani na kujisahihisha mwenyewe lakini naamini watendaji ofisi wanajua naingia ofisini saa ngapi na natoka saa ngapi,” alisema Chiligati na alipoulizwa kuhusu shughuli za chama kuingilia majukumu ya serikali, alisisitiza kutotaka kujisahihishia mtihani.
  Katikati ya mwezi huu akizungumza na vijana wa kutoka nchi mbalimbali za Afrika mjini Dar es Salaam, Rais Kikwete alituma salamu za mwanzo kwa wateule wake kwa kuwaambia vijana hao ya kuwa endapo atajaliwa kuongoza tena Tanzania mwakani, atafanya jitihada kubwa kuondokana na sura za wazee ambao atawabadilisha na vijana.

  Akizungumza katika mkutano wa vijana hao wa kulea viongozi wa Afrika, Rais Kikwete alisema atafanya mabadiliko makubwa kwenye Serikali yake akshinda uchaguzi ujao.
  Alisema Kikwete: “Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”
  [​IMG]
   
 2. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kila aina ya usanii utaonekana kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2010, vilio vyote kutoka kwa wananchi? Walikuwa wapi muda wote matatizo ya maji, njaa, umeme, huduma mbovu za afya na elimu, mikataba ya kuiteketeza nchi na mengineyo lukuki wasiyaone tangu walipoingia madarakani?.
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Ssi tunachotaka ni huduma nzuri ambazo ni haki ya raia kikatiba. Kama watagombana au mawaziri watabadilishwa, si la msingi kama ambavyo kila kiongozi angetekeleza wajibu wake bila upendeleo au kwa ajili ya kutimiza matakwa yake ya kujinufahisha binafsi. Acha wajikosoe, wakiwajibika vizuri, hiyo ndo neema kwetu wananchi.
   
 4. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Until I see the Prezidaa actually do something I will remain with my set notion that he can't do jack schiit, nada, nothing!

  And the same old shit goes on, over and over, same old tired song.......ain't this a b*@^h!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hana lolote, he us out to save his skin. Ni njia nyingine ya JK kutaka kujisafisha mbele ya wananchi ili aonekane safi isipokuwa wenye matatizo ni watendaji wake. Asilolijua ni kuwa watu wenye akili watamuona mwenye hatia kwa sababu kwanza yeye ndiye aliyewateua hao watu ambao wameshindwa kufanya kazi kwa matarajio yake. Pili, ana mamlaka ya kuwatimua au kuwabadilisha kwa jinsi anavyopenda yeye, kuwafikea tu itasaidia nini na imeshaonyesha kuwa hili ni sikio la kufa?
   
 6. kilema

  kilema Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  TATIZO LETU WATANZANIA NI KUTOKUWA NA MALENGO REALISTIC NA NDIO MAANA HATUWEZI KUWABANA VIONGOZI WETU. TUNAISHIA KUPEW ALILIMIA KADHAA BARABARA KADHAA? NINA MASHAKA KAMA MAWAZIRI WENYEWE WAKO NA MALENGO YA NAFASI WANAZOTUMIKIA

  TUKITAKA KWENDA MBELE BASI TUCHAGUE VIONGOZI WALIO NA MALENGO YA KUELEWEKA ILI TUWEZE KUPIMA MAFANIO YAKE. MFANO KATIKA KIPINDI CHANGU NITAJENGA SHULE FULANI MTAA FULANI YENYE MADARASA KADHAA KWA KUWANGO FULANI. BARABARA ZA MITAA FULANI ZENYE UREFU WA MITA KADHAA ZITATIWA LAMI.NITAONDOA FOLENI HAPA JIJINI KWA MIKAKATI HII. N.K.
  SIYO MTU ANAKUJA MIMI NTAJENGA MASHULE NITAJENGA HOSP. NITALETA MAJI SAFINA SALAMA. WANAOOMBA UONGOZI WAKITOA AHADI WAJE NA MIPANGO KAZI YA NAMNA YA KUTIMIZA HIZO AHADI ZAO. 2010 hATUDANGANYIKI
   
 7. M

  Mchili JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Usanii mtupu, alitegemea nini alipokua anawateua bila kuangalia uwezo wao!!! Hata mawaziri washajua udhaifu wake, sawa na mbwa hana meno anakubwekea una haja ya kukimbi?
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Strong analysis, safi sana!

  Respect.


  FMEs!
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  "Hayo maoni ya watu siwezi kuyaingilia, mimi siwezi kufanya mtihani na kujisahihisha mwenyewe lakini naamini watendaji ofisi wanajua naingia ofisini saa ngapi na natoka saa ngapi," alisema Chiligati

  Sijui kama wenzangu mmenotice hapo lakini hivi huyu Chiligati anajua kwamba kuingia kazini muda unaotakiwa na kutoka muda unao takiwa haku maanishi ni mchapa kazi? Mtu anaweza akaingia kazini saa mbili asubuhi atoka saa kumi asubuhi lakini utendaji wake usiwe wa kuridhisha. Kusema ukweli kauli ya hapo juu ya Chiligati imenifanya nimuone huyu jamaa ni hana common sense.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Alisema Kikwete: "Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana."

  Issue siyo kujaza tu vijana. La muhimu ni kuwaka watu ambao wanaweza kufanya kazi ipasavyo. After all JK, EL na wengi wa hao mawaziri hawaku anza leo wala jana uongozi na wote ni a product ya ujana huo huo. What's the point of raising the youth of today to be the failures of tomorrow?
   
Loading...