G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,015
Sakata la elimu ya bure kama inavyonadiwa na serikali ya CCM linaweza kuisambaratishia mbali elimu ya Tanzania kama serikali itaendelea kuja na misimamo iliyo nayo sasa!
Mashule mengi mambo yamesimama, wakuu wa shule wanapewa shilingi 30000 hadi 2000 as Kitanzania kuendesha shule!
Mathalan shule moja iliyopo Manyara mkuu wa shule amepewa 2000 kuendesha gharama zote za mambo ya utawala ikiwemo kununua vitendea kazi! Kabla ya sera 'mbovu' ya CCM kutekeleza elimu bure, shule hiyo 90% ya waalimu wake walikuwa wa kujitolea huku wakilipwa na michango ya wazazi. Kwa sasa shule hiyo imebaki na mkuu wa shule pamoja na waalimu wawili wote wakiwa ni wa masomo ya arts baada ya wale wa kujitolea kuachishwa na sera ya "elimu bure" kwa sasa wanafunzi wanaingia madarasani kutazama tu kuta za shule na paa huku wakiifaidi vilivyo elimu bure bila gharama! Huo ni mfano mmoja miongoni mwa shule lukuki sana ambazo siwezi kuziorodhesha hapa kutokana na muda ila zinaonekana na kila mtu!
Asilimia 90 ya shule zote Tanzania zimekwama kwa kiwango cha juu kuliko kawaida! Hizo asilimia 10 zilizobaki zimeamua kujiendesha na kuipuuzilia mbali sera ya midomoni ya CCM ya elimu bure! Wazazi wameamua kushikamana na waalimu kuendesha shule zao ili watoto wao wafanikiwe!
Mtihani matokeo yakiwa mabaya mawaziri watakutana kutoa matamko na kutisha waalimu pamoja na kutekeleza ile kauli yao ambayo mimi sipendi kuitumia ya majipu! Ila CCM ikumbuke kuwa hao 10% walioipuuza sera ya CCM watakuwa tofauti sana hawa ni pamoja na wale wa shule binafsi wanaojiendesha! Wale 90% watoto watarudi nyumbani huku ndani ya 'visiku ' vichache serikali ikitoa matamko kutafuta mchawi! Baada ya hapo ni biashara itaendelea kama kawaida!
Shule hazifundishi mambo hayaendi na muda unasonga! NECTA watatoa mtihani kwa hao wa shule za wale kutoka 10% za walioipuuza sera mbovu ya CCM, watatoa kwa wale 90% wanaofaidi 'elimu bure ya kutazama kuta za madarasa pamoja na mapaa' Pia watatoa mtihani huohuo kwa akina Feza schools na st. Marian na wengineo! NECTA itawapima katika mzani mmoja!
Mheshimiwa Simbachawene endelea kutoa matamko!
Waziri wa elimu na naibu waendelee kuhubiri elimu bure! Huko mashuleni itatekelezwa ila "Mchimba kaburi haingii yeye"
Elimu bure ingetekelezeka kama kungekuwa na misingi thabiti lakini siyo haya maigizo yaliyokithiri yanayoendelea kwa sasa!
Unampa mkuu wa shule shilingi 3000 aendeshe shule huku ukimpa matamko yanayopishana masikioni mwake Eti ole wako ufanye hivi ole wako itokee vile ole wako sijui nini.....!
Narudia tena "mchimba kaburi humtia mtuwe"