Standalone
JF-Expert Member
- Nov 15, 2014
- 676
- 576
MCHUNGAJI Christopher Mtikila, leo amefungua kesi ya kikatiba namba 14 ya mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria kwa ajili ya kuitambua rasmi Mahakama ya Kadhi.Muswada huo umepangwa kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa katika kikao cha Bunge litakaloanza vikao vyake Jumanne wiki hii mjini Dodoma.
Katika mashtaka yake, Mchungaji Mtikila aliye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Democratic (DP), anaitaka mahakama kuu kufanya mambo makuu matatu.
Kwanza, anaitaka imwadhibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kwa kumpa kifungo kisichopungua miaka mitano kutokana na kitendo chake cha jaribio la kuvunja ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Pili, anaitaka itamke kwamba ni kinyume cha sheria kwa serikali kujihusisha katika masuala yoyote yanayohusu Mahakama ya Kadhi au Shirika la Waislamu Duniani (OIC).
Na tatu, anaitaka Mahakama Kuu itamke kwamba adhabu zinazotolewa na Mahakama ya Kadhi kwa mujibu wa sheria za Kiislam (sharia), kama vile viboko, kupondwa mawe hadi kufa, kukata kichwa, na kukata mikono, zinapingana na utu wa binadamu, na ni kinyume cha Tamko la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu.