Mtihani wa darasa la saba waludiwa leo

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Jana na leo shule tano za kinondoni na moja ya Ilala zinaendelea kufanya mtihani wa darasa la saba kwa mala ya pili, msemaji wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi amesema kuwa ni kwa ajili ya utafiti kama walitazamia au la!

Swali ni hili,
1. je ni wote watakuwa hawajasafili nje ya mkoa?
2. tangu wamalize masomo, ni kweli bado wanakumbuka masomo au ni mbinu za kuwafelisha?
3. NK
 
Ukiona hivyo, watoto wao jamaa hao wa wizara hawasomi shule hizo. Huwezi kufanya kitu kama hicho kwa kujaribu ati kama kisu hiki kinakata kweli au kinachoma, kwa kurudia kisu kilichokujeruhi juzi. Wasitufanyie kiini macho hawa. Kama wizi wanaufungulia wenyewe kwa kuwapa watoto wao, au la kama wamo watoto wao basi huenda wamewapa maswali hayo watoto wao ili walio hohehahe wafelishwe.

Wanapima skills au wanapima uwezo wa kufaulu mitihani? Ni kitu cha kawaida mtu kujiandaa kwa kufaulu mtihani, ukijaniuliza baadaye swali lilelile baada ya mwezi usidhani nitajieleza kama nilivyokueleza wakati wa kwanza, kwani mtihani ukiisha na akili yangu naibwaga ipumzike. Kuna mtu anachekelea kufanyishwa mtihani?

Ufisadi mwingine huu, wanatafuta namna ya kuitafuna fedha ya wananchi kwa kisingizio cha utafiti wa kufanyisha watoto mitihani. Ukiuliza wametumia kiasi gani usishangae wakikuambia Bilion nne. Mbona wizara hiyo hiyo imeshindwa kuwashikisha adabu walimu wanaoiba pesa ya wazazi kwa kusingizia mia mja ya mtihani kila siku na mia tano kila weekend kwa wanafunzi, na mtoto asiyetoa pesa hiyo hulambishwa njiti, na DSM hapahapa? Hawaoni hilo?

Leka
 
Kiswahili cha Kaitaba kinaboa: mtihani "waludiwa" badala ya warudiwa. "Mala" ya pili badala ya mara ya pili. "Hawajasafili" badala ya hawajasafiri. Kaazi kweli kweli!
 
Ukiona hivyo, watoto wao jamaa hao wa wizara hawasomi shule hizo. Huwezi kufanya kitu kama hicho kwa kujaribu ati kama kisu hiki kinakata kweli au kinachoma, kwa kurudia kisu kilichokujeruhi juzi. Wasitufanyie kiini macho hawa. Kama wizi wanaufungulia wenyewe kwa kuwapa watoto wao, au la kama wamo watoto wao basi huenda wamewapa maswali hayo watoto wao ili walio hohehahe wafelishwe.

Wanapima skills au wanapima uwezo wa kufaulu mitihani? Ni kitu cha kawaida mtu kujiandaa kwa kufaulu mtihani, ukijaniuliza baadaye swali lilelile baada ya mwezi usidhani nitajieleza kama nilivyokueleza wakati wa kwanza, kwani mtihani ukiisha na akili yangu naibwaga ipumzike. Kuna mtu anachekelea kufanyishwa mtihani?

Ufisadi mwingine huu, wanatafuta namna ya kuitafuna fedha ya wananchi kwa kisingizio cha utafiti wa kufanyisha watoto mitihani. Ukiuliza wametumia kiasi gani usishangae wakikuambia Bilion nne. Mbona wizara hiyo hiyo imeshindwa kuwashikisha adabu walimu wanaoiba pesa ya wazazi kwa kusingizia mia mja ya mtihani kila siku na mia tano kila weekend kwa wanafunzi, na mtoto asiyetoa pesa hiyo hulambishwa njiti, na DSM hapahapa? Hawaoni hilo?

Leka
Kwa kweli uliyoyaeleza wangeyazingatia sidhani kama wangewapa watoto adhabu hii ya kurudia mtihani

Big up mkubwa
 
hii wizara sasa inafanya nini, sasa kama hivi watoto wengine wamekwenda likizo ina maana tayari wamefeli
 
Itakuwa hivyo, maana msemaji amesema kuwa wamefanya ghafula ili wizi usiwepo, kama kuna waliokuwa likizo mikoani hawakupata taharifa.
 
Watz hawajaweza kutumia lawyers tu mpaka leo? Ishu hii unawapa lawyers wanapeleka shule na wizara mahakamani. Kama wanahisi wanafunzi wame-cheat na kushindwa kutumia mbinu zao kuvumbua, imekula kwao!! That's how the real world works. Huwezi ku-replay kila kitu!
 
Nani anajua ni shule gani hizo mimi nipo mbali na mtoto wangu alifanya mtihani huo sasa nimesafiri naye.
 
[ amesema kuwa ni kwa ajili ya utafiti kama walitazamia au la!,

jf kwa kulaumu...
 
Back
Top Bottom