Mtibwa yapania kuwaduwaza Yanga

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
mtibwa.jpg

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar imepania kuiduwaza Yanga kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mtibwa inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 10, sawa na Azam wakitofautiana mabao ya kufunga baada ya kucheza mechi nne.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amesema wamedhamiria kufanya vizuri msimu huu kama ikiwezekana kuifikia historia yao waliyoiweka miaka ya 1999-2000, walivyochukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Katwila alisema; "Ili kufanya vizuri zaidi msimu huu ni kuzifunga Simba, Yanga na Azam au kupata pointi nyingi kutoka katika timu hizo na kwa matokeo hayo ndio tutakuwa na uhakika wa kuwa katika nafasi nzuri.”

“Yote yanawezekana na tunauwezo wa kuzifunga timu hizo, kwani malengo na nia yetu tuliyoyaweka msimu huu ni kufanya vizuri kuliko msimu yote ambayo tunaanza vizuri na kumaliza vinaya,” alisema Katwila.

Chanzo: Mwananchi
 
Yanga wamejitapa kuwa wale wachezaji wenye mahaba na Simba wameisha huko Mtibwa, waliobaki mambo safi tu.
 
Back
Top Bottom