Mti uliotoa machozi Dumila

Mti uliotoa machozi Dumila

14 August 2012: DUMILA; MOROGORO

Nilikuwa nimetimiza wiki mbili ndani ya Dumila, mji mdogo unaounda kata za wilaya ya Kilosa.

Kilosa ni moja kati ya wilaya zinazounganisha Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania. Harakati zangu za kupambana kufubaza makali ya ugumu wa maisha, ndizo zilizonifikisha hapo.

Kwa zaidi ya wiki mbili, nilikuwa nikizunguka toka kijiji kimoja hadi kingine, nikikusanya mazao ya chakula. Hii ilikuwa biashara niliyojikita kwa zaidi ya miaka miwili tangu nilipoachana na ajira rasmi.

Nilinunua nafaka toka kwa wakulima wadogo vijijini na kuyahifadhi kwa muda katika ghala ndogo iliyopo Dumila. Baadaye niliyasafirisha mpaka jijini Dar es salaam, nilipoyauza kwa bei ya juu kidogo na kupata faida iliyonisaidia kusogeza siku.

Katika safari hizo, nilikutana na simulizi ya kusisimua kutoka kwa msichana wa miaka kumi na sita katika kijiji kimoja nilichotembelea. Msichana huyo aliishi na watoto wawili wa kiume wenye asili ya Kiholanzi katika mazingira duni ya kijiji kiitwacho Matale.

Kilichonishangaza zaidi ni namna walivyoonekana kuwa na uhusiano wa karibu; waliishi kama mapacha watatu, wakiwa na mshikamano wa kushangaza kila walipopita.

Maswali mengi yalinijia kichwani; Ilikuwaje msichana huyu akaishi na watoto wa kizungu katika kijiji cha ndani kama hiki? Wazazi wa wavulana hao walikuwa wapi? Uhusiano wao ulitokana na nini?

Nilipowadadisi wenyeji, nilipata fununu kwamba wavulana hao walikuwa raia wa Uholanzi lakini msichana alikuwa Mtanzania, mzaliwa wa Dumila. Hata hivyo katika hali ya kushangaza, hakuna aliyefahamu kwa hakika chanzo cha uhusiano wao wala sababu iliyopelekea waishi pamoja.

Kwa asili yangu ya udadisi, sikuweza kuondoka kijijini hapo bila kufahamu ukweli. Nilihisi kuna siri nzito nyuma ya maisha ya msichana huyo na hao watoto wawili.

Kama mtu ambaye daima hunyemelea simulizi zisizo za kawaida, sikuweza kuondoka bila kutanzua fumbo hili. Lakini haikuwa kazi rahisi. Msichana huyo alikuwa mkimya na mgumu kumzoea. Ilibidi nivute subira, nikitafuta jinsi ya kujenga mazoea na uaminifu kwake.

Hatimaye baada ya juhudi na uvumilivu, alikubali kunieleza historia yake. Tulipata wasaa adimu wa kufanya mazungumzo kwa siri. Ndipo akafunguka kuhusu historia nzima ya maisha yake na jinsi alivyokutakana na hao watoto.

Simulizi yake iliniacha katika taharuki nzito. Nilijikuta nikiamini kwa dhati, kuwa dunia hii imebeba mambo mazito, yanayostaajabisha na kutisha kuliko unavyoweza kudhani.

Endelea kufuatilia.....
Tumalizie mwamba nishandaaa 🍿
 
1000046112.jpg
 
Machozi ni kimiminika kama yalivyo maji....imekuwaje kama hicho kilichotoka kwenye mti kiwe machozi badala ya maji?
 
Back
Top Bottom