Mtenda akitendwa huhisi kaonewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtenda akitendwa huhisi kaonewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JAPHET MAKUNGU, Mar 3, 2011.

 1. JAPHET MAKUNGU

  JAPHET MAKUNGU Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Basi bwana, katika soma soma yangu threads katika jumba hili nikajawa na uchungu sana kuona baadhi ya makada wa Mapinduzi wakilalama CDM wanapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya Siri kali yao.

  Nikakumbuka back in the days nlivokuwa mwanachama (lakini siyo kada) nikiwa jimboni kwangu, mara Green guards wakapita katika pilika pilika zao. Wakawafanyia dole gumba la mkono baadhi ya wananchi jimboni kwangu, nao wananchi wakapunga vidole viwili juu, punde si punde wale Green wakashuka katika gari na kuwapiga vibaya wale wananchi wakidhani ni makada wa vidole viwili, kumbe walikuwa wamechoshwa na dole gumba linalomaanisha tupeni tena tule (Give us chance to chop Tz small)

  Kwa tukio lile nilirudisha kadi kwa katibu wa tawi wa Mapinduzi na kuamua kuchukua kadi ya vidole viwili. Nilichukia sana kwa sababu Mapinduzi yalikuwa yanawapindua hata wananchi waliokuwa wanajibu salaam ila kwa lugha nyingine tofauti kidogo. Nilienda mpaka kituo cha polisi walikopelekwa wananchi nikawataka wawaachie haraka, wananchi walivoachiwa tuliungana pamoja kukataa kupinduliwa hata uhuru wetu.

  Sasa najiuliza sana, hivi wanachokifanya Mapinduzi (kupindua haki za wanyonge)na wanachokifanya CDM (kuelimisha wananchi juu ya uadilifu katika usimamizi wa rasili mali za nchi na utawala bora) ni wepi wanaotishia amani ya nchi?

  Everybody deserves as much as to the extent of what s/he sows!!!!!! Haya wanayoyaona ni wao wameyatengeneza, na hawakujua kama wao wenyewe "are the authors of their own destruction" Kwa nini wanawanyooshea wengine vidole?

  Logic: Hivi watanzania ni mazuzu hata washinikizwe kuhudhuria maandamano na mikutano ya hadhara ya CDM? Hivi Watz hawawezi kupembua pumba na mchele? Hivi hawayaoni hayo madudu ambayo Siri kali inayafanya?

  Nimeogopa sana jana, siku mbili baada ya rai ya mkuu wa nchi kuwataka wananchi kuipuuza CDM na maandamano yao, huko Kagera maandamano yamevunja record kwa kukusanya watu wengi kuliko sehemu nyingine yeyote kanda ya ziwa.

  Nadhani mkuu alimaanisha kuwatia hamasa wananchi wahudhurie zaidi.

  Hii ni lugha rahisi na inayoeleweka ya wananchi wakiiambia Siri kali, " Tumechoka............ tumechoka.............. hatuwezi tena kuendelea"

  Heri mwenye macho akayaona haya na mwenye masikio akayasikia na kuyaepuka mapema.

  I beg to submit your excellencies!
   
 2. P

  Paul J Senior Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wao wanadhani bado watanzania bado tumelala kama walivyozoea, wananchi tumeamka viongozi wa ssm bado wamelala na tusiwashutue waache waendelee kulala hivyohivyo wakidhani bado ni wakati wa kutumia uzoefu uleule wakati technology ilishabadilika. Rais kama angelikuwa creative asingelalama kwenye TV badala yake angesolve matatizo yanayowakabili raia na si kuwatisha eti cdm ina nia mbaya wakati wanajua kabisa serikali na ssm ndo wanyonya damu wakubwa wa watanzania!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia marudio sijui ni ya kipindi gani tbc1 Wasira akiwa na gabriel anawalaumu cdm kwa kupandikiza chuki kwa watz nkajua kweli ccm wamefulia yaani anaargue kama conservative and ignorant peasant nkaamua kuzima tv!
   
 4. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  mbaazi ukikosa maua husingizia jua"-dr. yusuph makamba
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unashauri Mh. Raisi awapongeze CDM kwa kufanya kazi ya kuelimisha raia wake bila kutumia gharama za serikali? Sijui kama atafanya hivyo
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,778
  Likes Received: 6,110
  Trophy Points: 280
  CDM haihitaji kupongezwa na Mh.Rais au **** mwingine yeyote ndani ya CCM, NCCR, UPDP, CUF, fisadi, au kibaraka yeyote yule. Nguzo kuu ya CDM ni umma wa watanzania wanyonge na maskini ambao jasho lao linamwagika kila siku kwa ajili ya taifa letu bila wao kuboreshewa maisha yao. Hao, tena hao tu, ndio watakaoipongeza CDM na kwa hakika wameshafanya hivyo. Udumu UMMA wa watanzania, idumu tanzania.
   
 7. G

  Glad Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua imefikia kipindi baadhi ya viongozi wetu wanafikiri wao wanaakili sana kuliko watu wasio wanasiasa!! Haingii akilini hata watu wanaojiita ni wa vyama vya upinzani leo wanakandia CDM,lkn uzuri ni kwamba kwa kufanya hivi ndio wanaipandisha chati saaaaana CDM bila wao kujua naomba waendelee hvhv..
   
Loading...