Mtela Mwampamba: Biashara na uongozi wa umma - Azam Two

Mtela Mwampamba

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
537
347
Ndugu Wazalendo, Salaam!!

Kesho 16/05/2016 saa 1:30 asubuhi ndugu MTELA MWAMPAMBA katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo atakuwa live ( Moja kwa moja) kupitia kipindi cha Morning Trumpet ndani ya Azam Two, Kujadili Muswada Wa Sheria Ya Kutenganisha Biashara na Uongozi Wa Umma.

IMG-20160508-WA0182.jpg


Karibuni tushiriki wote kwa kuangalia na kutoa maoni yetu kwa njia ya simu.

Ahsante!!!
Ndugu Watanzania Wazalendo, leo nikiwa Azam Two Tv, nimezungumzia umuhimu wa kupitishwa muswada wa Sheria unaolenga kutenganisha Biashara na Uongozi wa Umma ili kuepusha migongano ya kimaslahi inayopelekea Taifa kupata hasara kwa baadhi ya viongozi wengi kutumia vibaya madaraka yao kwa manufaa yao binafsi. Mbali na maudhui ya Muswada huo nimesisitiza Kuwepo na Ushirikishwaji wa wananchi pale viongozi wanapotaja Mali au Madeni yao na Biashara wanazomiliki ili kuwepo na uhalisia na ukweli kama vile TAKUKURU inavyotushirikisha wananchi wa hali nchi maana huku ndiko ukweli uliko Pia Watanzania wenzangu tuwashauri wabunge wetu wapitishe huu muswada hata kama maslahi yao wanaguswa kwa kiasi kikubwa.#WatanzaniaTuungeMkonoMuswadaUpitishweUongoziNiUtumishi
 

Attachments

  • WP_20160516_004.jpg
    WP_20160516_004.jpg
    184.1 KB · Views: 83
Naweza kupoteza muda wangu kumsikiliza msariti? Saa moja na nusu siyo muda wa kazi? kwa W M wanapongeza na huku wanapongeza. Hovyo!
 
Nafikiri muda huo waTZ watakuwa makazini hivyo hawatapata nafasi ya kuangalia...

Kwanini usingefanya kipindi saa00:00 muda huo waTZ wamerudi majumbani?
 
Nafikiri muda huo waTZ watakuwa makazini hivyo hawatapata nafasi ya kuangalia...

Kwanini usingefanya kipindi saa00:00 muda huo waTZ wamerudi majumbani?
Wengine wanakuwa off, watawawakilisha watakaokuwa makazini
 
Safi sana Comredi. Nakuaminia sana ndugu
We Dada punguza njaa, kule uzi wa PM kukataza matangazo ya live umechangia kuwa muda wa asubuhi ni Muda wa kazi na waTZ wajikite kufanya kazi na si kuangalia Bunge...

Hapa kwa MTELA Mwampamba unaunga hoja kuwa ni sawa tu tena vizuri kufanya mjadala kwenye TV muda wa asubuhi...

Sijui una waume wangapi wewe Dada hadi umekuwa na usahaulifu wa kiasi hiki
 
Wengine wanakuwa off, watawawakilisha watakaokuwa makazini
Hiyo off duty ni kwa kipindi cha Mtela tu, panapo Bunge waTZ wote wanakuwa ON DUTY?

Kuna mambo ni amazing ila mengine yanashangaza zaidi
 
Ndugu Wazalendo, Salaam!! Kesho 16/05/2016 saa 1:30 asubuhi ndugu MTELA MWAMPAMBA katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo atakuwa live ( Moja kwa moja) kupitia kipindi cha Morning Trumpet ndani ya Azam Two, Kujadili Muswada Wa Sheria Ya Kutenganisha Biashara na Uongozi Wa Umma. Karibuni tushiriki wote kwa kuangalia na kutoa maoni yetu kwa njia ya simu. Ahsante!!!
sasa si mnasema hamtaki mambo ya live coz atu hawafanyi kazi wanaangalia TV? sasa wewe unamtangazia nani asiyefanya kazi atakayekaa akutazame muda huo? hivi nyinyi mna afya ya akili kweli au ni wanajimu?

maana ulipaswa ujiulize hiyo live coverage atakuangalia nani? Watanzania mnatia huruma na aibu sana kwa uduni wa fikra.
 
Back
Top Bottom