TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,551
- 20,259
Wadau mi kuna kitu nimegundua. Nadhani hawa watengenezaji wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki kama simu, tablet na kompyuta ni WEZI na hawana lengo zuri kabisa na sisi walaji na wanashirikiana kutufilisi bila sababu yoyote kwa kisingizio cha kukua kwa teknolojia.. We hebu jiulize..
Ni kwanini kiila mara watengenezaji wa softiwea za simu na kompyuta wanatoa "vesheni" mpya za softiwea, ambazo zina mahitaji makubwa zaidi ya zile zilizotangulia, huku kukiwa hakuna tofauti yoyote ya kimsingi ya kiutendaji kati ya vesheni ya zamani na ya sasa? Jambo ambalo linatulazimisha sisi walaji kila mara ku- apdeti hadwea au kununua kompyuta/simu mpya, kwa kuwa eti tulizo nazo hazina "spesifikesheni"?
Nitatoa mfano: Mimi nimeanza kutumia kompyuta rasmi mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili. Enzi zile, tulikua tunatumia Windows 98, japo windows 95 zilikuwepo kuwepo bado.. Basi bwana kipindi kile "Maikrosofti Wedi" ilikua ni ya 97. Kwa wale ambao hamkuwepo naomba niwaambie tu kwamba.. Microsoft Word 1997 ilikua inafanya kila kitu ambacho Word 2013 inafanya na zaidi!! Ila Windows 98 na Office 97 zote kwa pamoja zilikua zinaenea kwenye kompyuta yenye 1Gb HDD, na nafasi inabaki kuubwa tuu.. hapo una RAM yako ya 32Mb na processor 133Mhz..aah shwari kabisa..
Sasa hivi ku install Windows 8 unatakiwa uwe na minimum ya 16 - 20Gb HDD, 2Gb RAM na processor ya 2Ghz!!
- Windows 8 kazi yake ni kuwasha kompyuta....... Kama ilivyokuwa Windows 98
- Microsoft Word 2013 ni ya kutaipu barua ........... Kama ilivyokua Word 97
- Functions zote zilizoko kwenye Excel 2013 ......... Ni kopi pesti ya Excel 97.. nakadhalika.
- Windows Media Player ni ile ile.. Paint ni ile ile.. Solitaire HAMNA!! Sasa huu kama sio WIZI ni nini?
Kwanini hawa wanaotengeneza kompyuta na software hawatengenezi software bora lakini zenye ujazo mdogo ili kupunguza mzigo wa gharama kwa watumiaji? Au watoe "Windows 7 Lite" au "Mini" au "Windows 8i" kwa sisi watu wa kawaida ili tusinunue kompyuta mpya ndani ya walau miaka kumi? Eeeh!
Hebu jiulize, watengenezaji wa injini za magari wanawezaje ku maintain "aspekt reshio" ya ukubwa wa injini na "Horsepower"? Kama wangekua kama hawa watengeneza softwea, si gari zote V8 zingekua na injini kubwa kama kichwa cha treni?? :thinking:
Wadau hebu niambieni tunaondokaje kwenye huu mtego? Maana naona na kwenye simu trendi ni hiyo hiyo.. Android 2.1, 2.2, 2.3, 3.0, 3.1, 3.2, 3.3, ....4.0, 4.1, 4.2, 4.3.. Bora tena kwenye kompyuta softwea zinakua kubwa huku hadiwea zinapungua ukubwa, sasa kwenye simu softiwea zinakua kubwa NA simu nazo zinakua kubwa!! Mwisho tutakua na simu kubwa kama kompyuta, na kompyuta ndogo kama simu..!!