mtazamo wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mtazamo wangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kitalolo, Feb 22, 2011.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nafikiri kuwa huyu bwana aliyengangania kurudi ikulu kwa kusaidiwa na tume ya ccm ya uchaguzi kuchakachua matokeo ya kura za uraisi ndiye ndiye mtu pekee naweza kusema aliyekabiliana na changamoto nyingi pengi kuliko watangulizi wake tangu awamu ya kwanza mpaka hii aliyolazimisha kuiongoza yeye, pengine kuna baadhi ya changamoto alizorithi kutoka awamu ya kwanza na ya pili na ya tatu, ila kibaya zaidi ni pamoja na yeye kuongeza changamoto ambazo ni mbaya zaidi ya zile alizorithi, mtazamo wangu ni kuwa kwa kushindwa kwake kuwajibika na kuwawajibisha wenye kusababisha changamoto hizo ndivyo ambavyo inamuwia vigumu zaidi kuzidi kushindwa kuliongoza taifa hili.
  imefika mahali kila mtu anauliza ikiwa taifa hili lina viongozi au na familia yenye watoto yatima wa watoto wa mitaan wanaorandaranda bila kujua hatma yao. pengine pia ni sawa na familia ambayo baba au wazazi ni walevi na wazembe wasiojali familia zao na wako tayari kufumia rasilimali za famili katika kuhongo au kuwanunuliwa wenzao pombe bila kujali ikiwa familia ina chakula hata cha siku hiyo tu. wako wazazi ambao ukiwakuta bar na ofa wanazozitoa kwa wenzao pamoja na hongo wanazitoa kwa malaya ni kubwa mno na huwezi amini kuwa familia zao hazina mlo wa siku hiyo.
  nadiriki kusema naweza kulifananisha taifa hili la Tanzania na familia yenye wazazi au mzazi wa aina hii asiyejua majukumu ya familia yake. na kuangalia yanayotokea katika familia hii ya tanzania naweza kusema pengine baba au mama au wazazi nikimaanisha viongozi wa familia hii ni wazembe au ni walevi. na nafikiri hata baba wa awamu ya pili alilitambua hili na akadiri kusema kuwa tanzania ni sawa na kichwa cha mwenda wazimu unaposema tanzania unamanisha watanzania.
  kwahiyo ndugu zanguni watanzania kwa kauli hii ya mzee ruksa tuihamishhie kwenye hali halisi kuwa tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu kila mtu anakuja kujifunzia kunyolea hapo. hivyo kwa maana ya awali ya tanzania ni watanzania .
  swali je kanini tukubali kuwa kichwa cha mwenda wazimu na kuruhusu kila mtu kujifunza kunyolea kwenye kichwa chetu?
  wakati mwingine huwa natafakari kuwa huwenda kutokana na changamoto zinazolikabili taifa letu pengine hata huyu bwana wa awamu ya nne amefika mahali akaona kabisa kuwa yeye ameshindwa lakini katika hali ya kibinadamu hata baba huwezi kuwaambia watoto au mkeo au majirani kuwa familia imenishinda kwa hofu ya kuchekwa lakini kwa kuangalia tu kwa nje majirani wanaweza kutambua kuwa kuwa huyu baba au hawa wazazi familia imewashinda, wakati mwing9ine pia ni rahisi sana kuwanyooshea kidole na kuwacheka lakini wao wenyewe wanajifanya kuwa wanaparangana na maisha.
  huyu bwana kweli anadanganywa na hawa watu waliokwisha kutambua kuwa tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu na ameliwa sifa wanazompa wakati wametuketisha chini na kutunyoa kwa viwembe vya kuokota au mikasi mibutu pale ambapo wanampeleka nje kupatanisha wenzake na kuwaambia kuwa walichakachua matokeo hivyo wanastahili kuachia ngazi.
  pia pengien anahitaji sisi tulione wenyewe kwamba familia hii imekwisha mshinda hivyo anahitajika kluondoka sasa hapo ndipo pale inapotakiwa nguvu ya umma na kutokana na ulevi wa mvinyo aliopewa yeye atafikiriki kuwa bado anaouwezo wa kulongoza taifa hili na ndipo hapo atakapongangania kwa kuwapiga watu wabomu au kwa kuchakachua matokeo ili aendelee kuongoza kwani wanaompa mvinyo wanamsifu kuwa mzee bado una uwezo wa kuongoza na amelewa mvinyo huo.
  kwa mtindo aliouanzisha wa kutoa majibu mepesi kwa maswali mazito na pengine kunyamaza kimya kwenye baadhi ya ishu itakuja kumgharimu sana, amajisifu kwamba aliweza kumaliza mgogoro wa zanzibar lakini utakapolipuka wa bara lazima ungarimu na waje kumsuluhisha kama atasalia madarakani au pengine kumgharimu hata maisha yake kama sio kukibia nchi,
  Ni wazi na ni dhahiri huyu bwana nchi imemshinda kutokana na kushindwa kuchukulia haya mambo yanayotekea katika hii nchi kwa uzito unaotakiwa ni kielelezo tosha cha kushindwa.
  kitu kingine kinachomdanganya huyu bwana ni hivi vijidigiri vya heshima wanavyompa hao mabwana wake ili kuzidi kumlewesha sidhani kiama kuna kiongozi yeyeto aliyeweza kupata vijidigirii vingi hapa tanzania kama huyu na hii naweza kusema ndio inayochangia kushusha kiwango cha elimu katika hii nchi maana sasa hata watoto wadogo wanalelewa katika mazingira ya kupewa zawadi za digiri unategemea mtoto atasoma tena wakati anajua anaweza kuzawadia digiri hata akiwa pumbavu?

  wito wangu kwa wananchi tulikomboe taifa letu ambalo kwasasa ni darasa la chini ya mti kwa vinyozi wote, na baada ya ukombozi nashauri taifa hili libadili jina huwenda hata hili jina linatuathiri, maana haiwezekana taifa lililo na rasimali nyingi namna hii kuendelea kuitwa taifa maskini katika ulimwengu huu tungeweza kuzitumia rasilimali zetu vizuri nafikiri taifa hili lingekuwa na viwanda vingi sana vya aina mbalimbali, lingekuwa linaongoza kwa kuzalisha mazao yaaina mbalimbalia na kusambaza duniani haswa kwa wakati ambao kunatokea matatizo ya upungufu wa chakula katika nchi nyingine sisis tungechukua fursa hizo katika kuliongezee neema taifa hili badala yake na sisi tunaenda kujiunga na wengine wanaoishi jangwa kuomba vyakula vya msaada. nafikiri kama tungekuwa na viongoze wenye mitazamo na sio usanii mambo mengi sana yangeweza kufanyika kwa ufani katika taifa hili ila kwa sababu ya tamaa, uroho na ubinafsi wa watawala wetu na taifa hili linakwenda kusiko siwezi kusema kuwa watawala au viongozi wetu ni wajinga au mambumbu kwasababu ninahakika wamepita japo ile mwalimu alikuwa anaiita futa ujinga na pengien wamekwenda mbali zaidi ya hapo.
  nafikiri tunmgekuwa naviongozi waadilifu na wawajibikaji na wenye uwezo wa uongozi basi pengine hata misaada tu tunayoipata tanzania ingesaidia sana kulifanya hili taifa kuonekana kama mahali bora pa kuishi.
  sifikiri kuwa amani hii tunayojivunia inatusaidia sana wakati ambapo bado tuna matatizo ya msingi, ni afadhali tungepitia kwenye kipindi kigumu na cha mpito hata bila amani lakini tuweze kutoka hapa tulipo na tuanze upya. sishabikii vita lakini ikibidi kupigana vita na tupigane ili kuweza kulikomboa taifa letu tanzania

  Shaloom Tanzania
   
Loading...