Mtazamo wangu kwa CCM na M4C

chief72

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
623
297
Sidhani kama niko sahihi, ila ndo ninachokiamini tatizo sio CCM wala Kikwete, sijui kwa nini watanzania hatujui hili tatizo. Ni sisi wenyewe watanzania kukosa uzalendo na nchi yetu kwa tabia zetu hata akija Barrack Obama ni kazi bure hata tuletewe malaika watukufu kutoka kwa Mungu holaaaa!!!

Je wanaouza ARVs feki ni akina nani, tembo wanateketea maporini, nenda mahakamani kunavonuka rushwa nenda vyuoni rushwa za ngono, watazame walimu wanavohaha kufaulisha watoto wasiojua kusoma na kuandika. Watu tai kubwa maofisini lakini hakuna kinachofanyika, watanzania leo hawapigi kura hadi wapewe kitu kidogo.

kwa njia yoyote sisi kama watanzania tujue nchi ni yetu, hata nchi zilizo vurugika ulimwenguni haikuwa abruptly, but very slowly kama Tanzania.We need a person ataeingia madarakani kwa njia tofauti na hizi tulizozizoea, huu u-CHADEMA, na u-CCM kwa mtazamo wangu si lolote si chochote.

Ni mtazamo jamani,tujadili.
 

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
1,809
595
Sijakuelewa, njia tofauti ipi au ya kutumia jeshi, au kutokea polini, maana utaratibu unaojulikana kisheria ni wa kupiga kura, naomba ufafanuzi kidogo...tafadhari
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,160
50,566
Tatizo kubwa ni jk na serikali yake,we unafikiri jk na mawaziri na wengine wa chini wangekuwa kama mwakyembe si tungefaidi asali na maziwa ya nchi yetu!! Mtoto wa mfalme malori yake yalikamatwa kwa kukwepa kodi mfalme akampigia nyooka kwamba afanye juu chini malori yatolewe!! Kwahyo kuanzia Juu hadi chini kumeoza!! Kuongoza tz ya sasa tunaitaji viongozi waliofyatuka(wasio fagilia makunyanzi) ndio nchi itabadirika lkn tukichagua hawa wakuchekacheka tu mda wote ndio maana tunavuna mabua,mkuu acha kutumika tatizo ni jk na serikali yake! Mie juhudi zangu binasfi bila nia ya dhati ya kiongozi siwezi fanya kitu!! Bora mie nisiwe kiongozi mkubwa maana ntafunga viongozi wazembe! Jk amechagua vilaza wengi mulugo type we unafikiri wataleta nini hao?
 

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
1,809
595
chemsha ubongo kiongozi
unadhani wanaweza kukuachia kwa urahisi uchague njia yako unayo dhani ni sahihi? alafu wao waende wapi, na hiyo ndiyo njia yao pekee ya kufaidi nchi hii... na kitu ambacho na wasi wasi nacho ni hiii katiba mpya ambayo tunadhani itatusaidia... kama waliifanya kwa kulazimishwa unafikili itakuwa kama tunavyo itaka, mambo si rafisi hivyo inabidi kujipanga kweli kweli bila unfiki, ikibidi kumwaga damu...Haki haiombwi!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom