Mtazamo wangu kuhusu vyama vya kisiasa

barite

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
227
120
Ngugu wa JF,hongereni na majukumu yenu ya leo.Mimi binafsi na kwa mtazamo wangu naona hakuna umuhimu wa kuwa na vyama vya kisiasa hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemon Tanzania kwani lengo la chama chochote cha kisiasa ni kuhakikisha wanashika serikali na kuongoza nchi ila kwa nchi nyingi zinazoendelea watu huwa wanaanzisha vyama vya siasa kama chanzo cha mtaji mfano ni pale CDM walipo mteua Dr slaa kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi uliopita viongozi waandamizi wa cdm walisema kuwa slaa ana mvuto kwa wananchi hivyo chama kitapata kura nyingi na kuongeza ruzuku na kweli kwa bahati cdm ikapata kura nyingi na ruzuku ikaongezeka ila matumizi ya ruzuku ndo hayo tunasikia mbowe kauzia cdm magari yaliyochakaa kwa bei kubwa,mara DR kajikopesha mamilioni ya chama.na kwa upande wa ccm na vyama vingine ni hivyohivyo mara kaenda ziara nchi za nje n.k na hayo yote ni matumizi mabaya ya pesa ya mlipa kodi wa Tanzania.pili katika nchi nyingi zainazoendelea ndo hivi vyama vya kisiasa huwa ndo chanzo cha mauaji wa wananchi hasa wakati wa uchaguzi na hii inajidhihirisha katika nchi nyingi za kiafrika,je?hu si muda mwafaka wa kufuta vyama vyote vya kisiasa kwani ndo chazo kikubwa cha kuvavuruga wananchi na pia kuwatenganisha kwa kupandikiza chuki baina ya wananchi kwasababu wanafanya siasa za chuki hasa hapa Tanzania?je,hi hela ya ruzuku zinazolipwa chama na kutokomea mikononi mwa watu wachache si kumnyonya mlipa kodi?na vp hizi hela zikaelekezwa kwenye mipango ya maendeleo .hitimisho kama watanzania tutakubali kuwa na mgombea binafsi kama rasimu ya katiba inyopendekeza basi ni dhahiri shairi kuwa hakuna umuhimu wa kuwa na vyama vya kisiasa.Ni hayo tu kwa sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom