Kwa kifupi ni kwamba, Profesa Baregu kaweka Misingi ya Namna gani Imani za Kidini zinatakiwa kuwa approached kwenye Katiba Yetu.
Kama Ndugu Cilla ulivyo quote kifungu cha Biblia, kwamba Biblia imewaelekeza wote wanaojitambulisha kama Wakiristo kwamba wasiape kwa kitu chochote kile including Biblia, Basi Katiba inatakiwa kuhishimu maelekezo hayo, Mtu akiishasema yeye ni dini Fulani basi, Maelekezo ya Imani yake juu ya mchakato wa kuapa yafuatwe.
Na isiishie kwenye Kuapa tu bali kwenye Mambo mengine yote ya Kiimani, Maelekezo ya dini husika juu ya Mambo husika yaheshimiwe.
Ili kujenga Jamii zenye watu wenye Imani zinazoeleweka, uwepo michakato ya kisheria ya kuauthorize Imani fulani za kidini kusambazwa kwa mujibu ya maelekezo ya vitabu vinavyoongoza dini hizo, Kwa maana ya kwamba Imani zote ni lazima maelekezo yake yawe katika Maandiko ama sivyo imani hizo zinabaki kuwa personal issues na haziruhusiwi kusambazwa kwenye Jamii kwa namna yoyote.
Ninaamini kwamba hii itasaidia kuondoa confusion kubwa ya mambo ya kiimani iliyotapakaa nchini kwetu na duniani kwa ujumla kiasi cha kupelekea mifarakano yenye maafa makubwa sana.
Hivi sasa kuna imani inaitwa ya kifreemanson, hakuna vitabu vinavyoilezea authoritatively, imani hii inasababisha hofu kubwa sana kwa wananchi hasa wamijini na inaleta instability kubwa sana kuanzia ngazi za kifamilia.
Bila kuwa na wananchi wenye Imani imara na zisizobadirika badirika kutokana na interpretations za vitabu hivyo zinazoibuliwa na kila namna ya watu, kila kukicha.
Angalia imani ya Kikirsto, ni mparanganyiko mkubwa sana, wakina kakobe, Gwanyima mfufua watu, na kuna mwingine kule Mwanza anaitwa Father God, sikia mambo ya kina mwingira Mama Lwakatare, na wakatoriki na Rais wao chaguo la Mungu, ni rehema za Mungu tu zinazozuia umwagaji damu.
Na apa ifikie sehemu tuweke ukomo wa Malalamiko ya Waislamu ambayo yamekuwa yakileta hofu kila wakati bila sababu za msingi, Nasikia wamechaguliwa kwa wingi kwenye tume hii, Waislamu watumie nafasi hii kuhakikisha kwamba Jamii za kiislamu popote zilipo katika Mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinaendesha Mambo yake kwa Mujibu wa Kitabu chao/Sharia, na waifinyange katiba katika namna itakayowawezesha kufaidika na Jumuiya za OIC lakini pia tutumie fursa hii katika kuhakikisha kwamba, Kwa mujibu wa katiba yetu, haitawezekana hata kidogo makundi ya kihuni yanayotoa roho za watu kwa visingizio vya imani za kidini, kupata nafasi ya kujiinua katika Taifa letu.Kama tunavyoona Nigeria na the Famous Alkaida Movement.
Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu katika Jina la Yesu Kiristo kwa Ujasiri aliompatia Profesa Baregu na kuapa katika namna ambayo leo inaleta mjadala kwenye Jamii yetu.
Tanzania, Nakuombea Rehema na Amani.