Mtazamo wangu juu ya Tanzania

Mtazamo wangu juu ya Tanzania

Joined
May 15, 2020
Posts
12
Reaction score
4
Habarini ya jioni, na shkamoni wakubwa na wazeee wangu wooote, mimi kijana wenu na kijana mwenzenu nimekuwa na huzuni kubwa na kuumia moyo sana pale linapo kuja swala la watu kuikosoa serikali! yaap kuikosoa ndiyo ila sio katika mtazamo mlioupata hapoooo. Kuikosoa serikali ni jambo jema na linapaswa kupewa kipaumbele na serikali husika kwani katika kukosolewa serikali inapata kujua udhaifu wake na uimara wake. Lakini namna ambayo tunaitumia kuikosoa na kuisema serikali kwa kuilinganisha na Taifa fulani hapo ndipo tunapokwama!

Ukweli ni kwamba wakuu hata katika maisha ya kawaida si vyema sana kupenda kujilinganisha na mtu au familia flani, kumekuwa na kasumba ya watanzania wakati mwingine ni viongozi ambao ni mifano ya kuigwa katika jamii pale wanapokuwa wanadai haki yao (yoyoye ile) hupenda kusema kauli hizi, mbonatu na nchi kama marekani wanafanya ,mbona marekani wanamtukana raisi na hawafungwi, mbona nchi fulani imeweza kufanya hili ambalo sisi hatuwezi? kiukweli uwiano huu sio mzuri hata kidogo, kwanini? ni kwasababu mataifa tunatofautiana kwa vitu vingi saaana. Yaani ni sawa na kuchukua per capita income kwa kila taifa ukatoa jibu la mwenye per capita kubwa ndiye aliye na ubora wa maisha kwa raia wake jambo ambalowachumi ulimwengu mzima watakupinga.

Kwanza kabiasa tunatofautiana katika umri wa taifa, ndiyo! namaanisha muda ambao tumepata uhuru na kuanza kujiongoza kama taifa, huwezi kukurupuka na kulinganisha taifa letu na mataifa ya magharibi tena kwa uwiano yaani (ratio) wanamahesabu watakubaliana namikuwa kama taifa viongozi wamejitahidi saana kuleta maendeleokatika kila sekta kadili ya uwezo wao lakini ni kwa uweledi uliomakinika. Em turudi nyuma kidogo..... mwaka 61 kipindi tunapata uhuru wetu kama taifa tulikua na upungufu wa wataalamu katika kila sekta na nyingine bila shaka hatukuwa na wataalamu kabisa, hakukua na hospitali za kutosha na hata kwa maeneo zilipopatikana ni wachache walioweza kupata huduma hizo, umeme vijijini pamoja na maji ilikua ni shida, Hivyo basi serikali ilianza kujipanga namna ya kujitegemea ikidhamiria kupata wataalamu wake katika kila fani na kutengeneza sera za kusaidia lengo la kujikomboa kutoka katika matatizo makuu matatu yaliyokua yanalikabili taifa umasikini na ujinga ikipewa kipaumbele.

Hivyo ni miaka mingi sana ambayo nchi iliandaa wataalamu wake na kuanza kuzitumia sera zake zilizotungwa kwa msaada wa mataifa mengine hivyo basi ni dhahiri kuwa kwa Umri ambao taifa letu la TANZANIA linao 50+ limejitahidi sana katika kuimarisha uchumikatika nyanja zote yaani barabara, sekta ya elimu, afya, na nishati basi si vyema kulinganisha taifa letu na nchi kama marekani ambayo ima miaka zaidi ya 200. Hata sisi pia endapo tutafikia hiyo miaka tutakua mbali saana japo hatutawafikia wao ila tutakuwa na hatua kubwa tuliyoipiga. Niwaombe ndugu zangu tuunge mkono juhudi za serikali na palipo na kasoro tukosoane pasipo kulinganishana na mataifa mengine, tumejitahidi sana hapa tulipo fika japo ni muda mchache sana tangu tupate uhuru kwani mikoa inaunganisha na barabara nzuri, elimu nayo si haba hata kidato cha nne tunafika tena buuree,lakini yote hayo hatuyaoni bali ni kulinganishana tu

MWISHO tuungane kama taifa, jamii na kila familia kuhakikisha tunapinia maisha yetu haya mafupi kwa mustakabali wa taifa.
 
Back
Top Bottom