Mtazamo wangu juu ya Rais Magufuli na Bajeti 16/17

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
Nawasalimu in the name of our living GOD.May his mercy be upon us all!

Wakati Rais Magufuli alivyoshinda uchaguzi,niliamini kuwa kweli mabadiliko yanakuja Tanzania.Pamoja chaguo langu hakuwa Magufuli,usiku ule niliona kuwa lowassa asingekuwa chaguo sahihi kwa watanzania,ni bora magufuli alichukua nchi katka wakati huu.

Naamini kabisa,Lowassa asingeweza kazi kama ya Magufuli,pamoja naweza kusema amejaribu,hajaweza moja kwa moja.Bado kuna watuhumiwa sema ni wakubwa hakuna wa kuwashika.

Baada ya hapo,Naibu speaker Dr.Tulia akapewa ubunge na kuwekwa ndani ya bunge hapo ndio nikajua kuwa,hapa kuna mchezo mchafu unakuja.Kilichotokea ni kuwa Tulia alichaguliwa kuwa Naibu Speaker in the blink of an eye.

Ikaja suala la Nape kupiga kelele huku Dr.Tulia akiwa nyuma yake kupinga bunge kuonyeshwa live.Kama mtanzania nilijuliza sana na kuuliza nia hasa ya rais Magufuli na watu wake katika nchi hii.

Lazima tukubali,uhuru una gharama yake na limits zake.Ila suala la kuminya uhuru wa kupata habari kwa wananchi ambao, pia kwa kiasi kikubwa ulisaidia sana watu kuelimika na kufahamu mwelekeo wa siasa na nchi ulifanya wabunge kutorudi bungeni na bila kusahau umuhimu wa upinzani.Rais Magufuli,huwezi kuminya habari hasa katika dunia tunayohishi sasa,hilo suala ni kujipa moyo.

Likaja suala la LUGUMI,rais akawa kimya infact hakutaka hio issue iwe ijadiliwe bungeni huku ukiwa unamtumia Tulia kuzuia mijdala muhimu kwa ajili ya mustakabali wa taifa;huu ni unafiki wa hali ya juu.Huwezi kusimama kutetea wachache huku ukiamini kuwa unataka kuwaletea watanzania maendeleo huku ukiwatoa kafara wachache,kwani wale elite wananini? kwa hili utaulizwa na Mwenyezi Mungu siku yako ikiwadia.

Suala la bajeti.Nimesoma sana.Nilichogundua ni kuwa imekaa kisiasa zaidi na sio katika kumbeba mwananchi wa kawaida.Tunarudi kwenye zama za kale kuwa serikali ndio inakila kitu,inafanya kila kitu,tena zile serikali za kimabavu.Falsafa ya Magufuli,ni siasa ya ujaama na ubabe,wakati hata china wenyewe hawafanya siasa za kijamaa maana walishtuka kuwa hailipi.

Kwa ufahamu wangu nimegundua kuwa,nchi nyingi za Africa tunaamini sana katika kuwa na serikali kubwa ambayo gharama zake ni kubwa,ambayo investment return yake kwa wananchi ni ndogo sana ukizingatia majukumu inayojibebesha.Tunajaribu kurun the goverment in the form of no return investment to its people.

Rais Magufuli nakubaliana na mawazo mapya katika kuongeza stream of new tax revenues lakni,je bunge liko wapi,kuangalia mizigo ya kodi kwa wananchi ambayo hawastahili?Hapa ndio tunaona kuwa Magufuli alimweka Dr Tulia ili kuweza ku-control bunge meaning; its one man show.Kiongozi ambaye hataki healthy debate au criticism ni hatari. Kuongoza nchi sio suala la mtu mmoja bali vyombo vitatu vikuu kushauriana.

Kama rais anataka kubana matumizi,basi tuanze na kupunguza serikali ikiwa na pamoja kuachana na magari ya anasa kama kweli tunataka kubana matumizi.Tusifike wakati,watu wa class ndogo ndio wawe wa kubana matumizi na kuishi maisha magumu huku viongozi wake waki wa wanatanua na maisha mazuri kwasababu wapo serikalini.

Kama serikali inakimbilia kupandisha gharama ya vitu huku ukubwa wa serikali inazidi na hakuna restructuring ya utawala kupunguza matumizi hio ndoto ya viwanda na middle class ni ndoto za alinacha.Kuna kazi sana katika kupunguza utiriri mkubwa wa vyeo vilivyopo serikalini.

Tuanze kwanza hapa kabla hatujakimbialia kupandisha gharama za maisha ili nyie mpate marupurupu yenu.Kingine,kuongeza kodi katka miamala ya pesa kama mpesa ni kitu cha ajabu sana.Ningeelewa kama kuongekuwa na kiasi ambacho kitachotonzwa kodi ya asilimia 10 lakini tukumbuke kuwa mifumo hii ndio rahisi kwa watu wa kawaida na wale wasiojiweza.

Kupandisha kodi kwenye bandari na utalii ni uwendawazimu wa ajabu sana.Nashidwa kuelewa washauri uliokuwa nao ni wakina nani.Lazima kama nchi,na Bunge kwa pamoja ijaribu kushauri serikali ni njisi gani ya kuweza kuwa na sera ambazo zitalinda, ikiwa na pamoja na kuboresha mazingira rafiki ya kufanya biashara kwa kila mmoja wetu kuinua uchumi.

Sera za rais haziwezi kamwe kuinua uchumi wa mtanzani wa kawaida,infact itaua hata yule muuza pipi na karanga.Mtazamo wangu na ushari wangu kwa raisi ni kuwa aache kuingiali katiba,Bunge na kazi zisizo muhusu.Yeye ni mkuu wa nchi.Itabaki hivyo,kazi yake ni kuongoza na sio ku over-rule decisions,agenda kwa manufaa yake bali kwa taifa.

Rais,anahitaji kuheshimu mihimili mingine kama mahakama na Bunge katika maamuzi na taratibu zake.Bajeti kama hii ya kipuuzi itaua biashara nyingine sana mjini.Ndio mwanzo wa kurudi kwenye zama za CUBA.Rais wa Marekani JFK aliwahi kusema " its a paradoxical truth that tax rates are too high today and tax revenues are too low,and the soundest way tor raise the revenues in the long run is to cut the tax rates"
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona na kulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so kaa kimya na angalia nchi inavyotake off!
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona nakulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so funga bakuli lako na angalia nchi inavyotake off!
Tatizo la waafrika sio uwezo .Tatizo letu ni kuutumia uwezo tulio nao kutatua matatizo na changamoto tulizo nazo katika muktadha husika.Worlbank IMF alikuwa anafuata miongozo ,Afrika is another kettle ..........
 
Wewe tuliza na angalia mpira uone hii nchi inavyotoka sasa, muda wetu umeshafika...
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona nakulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so funga bakuli lako na angalia nchi inavyotake off!
Huu ndio Ukosefu wa Unywaji Chai.
 
peleka siasa msalani,,kwa cv ya mtu ndo utendaji jibu hoja kwa hoja,,,watanzania wangapi wanye nafasi kubwa wamefanya kazi kwenye hizi taasisi na mpaka leo wameifanyia nini mama Tanzania ,,,,kasome maazimio ya huu mkutano unaiitwa /Bretton_Woods_Conference ulozaa Bretton woods institution...machozi wa maskini ni laana na inatimia haraka sana na matokeo ya dhuluma ni mauti,,,mwisho wa siku wote ni ubatili mtupu
 
Hizi ni zama zingine, muda wetu umeshafika so sit back, relax and enjoy the ride baby! Hii kasi siyo mchezo ni lazima mchanganyikiwe kwa maana imewakuta hamkujiandaa ...
 
Easier said than done! Ten years down the line well be where we were or worse,

Nini miaka 10 rudi hapa baada ya 5, wewe kama ukiweza lala halafu uje uamke 2020 uone kama utaitambuaTZ yetu kwa jinsi itavyokuwa imepaa ...
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au ImfaMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona na kulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so kaa kimya na angalia nchi inavyotake off!
Jamaa ukweli ubaki ukweli Mfano issue ya mobile transaction inatumiwa zaidi na watu hasa maskini wasio hata na kadi ya bank leo inawekwa vat, kwanini mikodi isitozwe kwenye madini? Utalii na bandari kodi ikiwa juu washindani wako wa biashara watashusha na watalii na mizigo ya bandarini itapita kwao.
 
Hizi ni zama zingine, muda wetu umeshafika so sit back, relax and enjoy the ride baby! Hii kasi siyo mchezo ni lazima mchanganyikiwe kwa maana imewakuta hamkujiandaa ...
we mbona hujibu hoja unasema taarabu,,zamani kwani world bank imekufa ,,we kwanza unanipotezea muda
 
Hizi ni zama zingine, muda wetu umeshafika so sit back, relax and enjoy the ride baby! Hii kasi siyo mchezo ni lazima mchanganyikiwe kwa maana imewakuta hamkujiandaa ...[@Barbarosa## inasikitisha mtoa mada anapotoa hoja nzito af unajibu kirahs hivi, hizi ndo cheap politics. ]
 
Jamaa ukweli ubaki ukweli Mfano issue ya mobile transaction inatumiwa zaidi na watu hasa maskini wasio hata na kadi ya bank leo inawekwa vat, kwanini mikodi isitozwe kwenye madini? Utalii na bandari kodi ikiwa juu washindani wako wa biashara watashusha na watalii na mizigo ya bandarini itapita kwao.

Nipo na wewe hapo kwenye kodi kwamba ni lazima tupanue wigo wa kodi hasa kwenye Majumba tunapoteza fedha nyingi sana, Wahindi wote wana mapartsments Upanga hawalipi kodi stahiki wanachukuwa fedha na kuhamishia nje ya nchi, haiwezekani mtu anajenga nyumba anapangisha mpaka dola 4 000 -10 000 za Kimarekani lkn hakatwi hata sumni hiyo siyo sawa, wenye Nyumba za kulala wageni, Mahoteli ya kitalii ilipaswa kila kitanda kunacholaliwa na binadamu kikatwe VAT, kwenye uuzwaji wa viwanja watu wanauza viwanja mpaka milioni 500 lkn hakuna hata shilingi inaingia Serikalini hivyo kwa upande wangu ni sawa kabisa Mpesa &Co,. zikatwe VAT kwanza ningekuwa mimi ningeenda mbali zaidi kwamba hata muuza chapati na nyanya gengeni alipe kodi siyo lazima VAT lkn hata achangie tu kiasi fulani ambacho kitatumika labada hata kusafishia hapo anapouzia ili naye awe na mchango wake, kwa kifupi kila mtu alipe kodi!
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona na kulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so kaa kimya na angalia nchi inavyotake off!

Wewe hujali chochote kuhusu hii nchi. Wewe ni mfia tumbo na usiyekuwa na mwelekeo kimaisha,fikra na itikadi. Ni bora niishi kama upepo maana hata upepo unasehemu yake na kazi yake. Kuliko kuendelea kuishia kama mtumwa,mpumbavu nisweza kujiuliza wala kufikiri.
Kama upo hapo hauna maana kuendelea kuishi. Hatuwezi kuendelea kutetea chama na serikali. Tanzania kwnanza!!!
 
Wewe hujali chochote kuhusu hii nchi. Wewe ni mfia tumbo na usiyekuwa na mwelekeo kimaisha,fikra na itikadi. Ni bora niishi kama upepo maana hata upepo unasehemu yake na kazi yake. Kuliko kuendelea kuishia kama mtumwa,******** nisweza kujiuliza wala kufikiri.
Kama upo hapo hauna maana kuendelea kuishi. Hatuwezi kuendelea kutetea chama na serikali. Tanzania kwnanza!!!

Usijali haya ni maoni yangu binafsi na mimi najiwakilisha mimi hivyo hauna haja ya kupaniki kwa maana ni mimi mmoja tu mwenye mawazo kama haya na wapo maelfu wenye mawazo kama yako hivyo wala usijali ...
 
Kwani nchii hii kuongozwa na ma phd na maprofesa katika wizara mbali mbali imeanza mwaka huu??? Jipe moyo tu
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona na kulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so kaa kimya na angalia nchi inavyotake off!
 
Utalii Tanzania unatosha sana kulea mapato ya kutosha. Inakuaje dubai wana jangwa wameweza kuwekeza kwenye utalii?
Iweje sisi tunafikiria kuhusu wanyama tuu?? wale waliosomea utalii wanaweza kusema.
Huyu waziri wa utalii ni mzigo watafute mtu anaweza kuifanya hii wizara ikaingiz fedha kuliko kuanza kuhangaika na mabodaboda na watu hali ya chni. Huu ni upuuzi.
Tatizo letu waafrica hatukai tukafikiria tunaridhika sana kwa haraka.
 
Waziri wa Fedha Mpango (PhD) ni mchumi aliyebobea na alishakuwa Mchumi mkubwa wa IMF na mpaka leo hii anaweza kutuma CV World Bank au IMF au taasisi yoyote ile ya Kimataifa na akapata kazi, hivyo analoliona na kulifahamu Waziri Mpango(PhD) wewe na bosi wako Mbowe (Dj) hamuwezi kuliona hata mpande juu ya mnazi, so kaa kimya na angalia nchi inavyotake off!
Aahaha haha-mchumi mkubwa wa IMF analeta "hotuba hewa" bungeni?
 
Back
Top Bottom