Mtazamo: wadada oleweni na wanaume wanaowapenda

Mtazamo: wadada oleweni na wanaume wanaowapenda

basi msilie mkikimbiwa na mimba dawa si nikushkishana adabu??

mimi ukikimbia mimba yako hakuna shida nenda tena nenda salama ila jua tu mwanao atajua baba yake alikuwa mbakaji... kwa bmaana hiyo nilibakwa nikapata mimba wala hainipi shida
 
Sijui nisemeje, angalau wanawake hujifunza kupenda(hata kama hakukuwa na chemistry, biology kama ipo inatosha) hasa kama mwanamme anakidhi vigezo.

Ukitaka kujua utamu wa penzi, mwanamme akupende mweee. Zombie for life!

ila pia kuolewa na mtu anaekupenda wakati wewe humpendi ni mateso vile vile.
 
Ni kweli unachokiongea bt inakua ngumu kumjua mwanaume kama anakupenda kwel coz nowdays pretendng ni kama chumvi kwenye mboga lazma iwepo
 
Nimerudi tena ni baada ya kwenda mwezi asali(honey moon) na kukimbiwa. Kwa hili naona pande zote zinahusika mwanaume anapomtaka mwanamke halafu mwanamke asimtimizie mume mambo yote hususan yanayo muondolea stress upendo unapungua. mwanamke pia akikosa haki yake pia shida.
 
Sijui nisemeje, angalau wanawake hujifunza kupenda(hata kama hakukuwa na chemistry, biology kama ipo inatosha) hasa kama mwanamme anakidhi vigezo.

Ukitaka kujua utamu wa penzi, mwanamme akupende mweee. Zombie for life!
mie somo la kujifunza kupenda nilipata divishen faivu na sitaki tena kurisiti. mateso ni yale yale tu, kumpenda asiekupenda na kupendwa na usiempenda. ukiniambia wanawake wanaweza kupretend kwa kuishi na mtu hata kama hampendi nitakukubalia asilimia zote ila si kujifunza kupenda.
 
Habari wadada...ni mengi nmepitia kwenye maisha na kujionea jinsi wanaume wanavyowatenda wanawake japo sio wote ila asilimia kubwa.

Na wengi wetu tumekuwa tunaingia kwenye mapenzi na mwisho ndoa na wanaume wanaosema wanatupenda na sisi kukuta tumewapenda zaidi n kuoza kwenye penzi lao kumbe walaghai,nawaombeni wanawake wenzangu oleweni na wanaume wanaowapenda zaidi ya nyinyi mnavyowapenda kwani wako radhi kukupa,kukufanyia kitu kizuri chochote kwa ajili ya penzi lake,kamwe hatakuliza wala kukuumiza atapenda familia yako na kujitoa maisha yote..lakini unayempenda wewe haoni tabu kukuumiza na kukuliza kwa kujua unampenda na huwez kumuacha.

Yamenikuta ndo maana nawashauri wote,oleweni na wanaume wanaowapenda sio mnaowapenda nyinyi.

hili nifunzo pia kwetu wanaume kuoa wanawake tunao wapenda na sio tunao watamani na pia kuoa mwanamke unaekupenda sio kukutamani labda kwasababu ya pochi,status n.k....
 
Hizo asilimia 100 au 50 huwa unazipimaje?! Unatumia nini kifaa gani kupima that number?! How can you measure feelings?!
 
Tatizo watu wana tafuta a perfect relationship...which is unrealistic...
 
Huu ushauri dada naoma kama umeutoa ukiwa na hasira hivi, hebu tulia kidogo uangalie usije wavuruga warembo wakawa wanakaa nasi mguu mmoja ndani mwingine nje.
 
Back
Top Bottom