Mtazamo: wadada oleweni na wanaume wanaowapenda

Mtazamo: wadada oleweni na wanaume wanaowapenda

prettydiva

Senior Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
101
Reaction score
39
Habari wadada...ni mengi nmepitia kwenye maisha na kujionea jinsi wanaume wanavyowatenda wanawake japo sio wote ila asilimia kubwa.

Na wengi wetu tumekuwa tunaingia kwenye mapenzi na mwisho ndoa na wanaume wanaosema wanatupenda na sisi kukuta tumewapenda zaidi n kuoza kwenye penzi lao kumbe walaghai,nawaombeni wanawake wenzangu oleweni na wanaume wanaowapenda zaidi ya nyinyi mnavyowapenda kwani wako radhi kukupa,kukufanyia kitu kizuri chochote kwa ajili ya penzi lake,kamwe hatakuliza wala kukuumiza atapenda familia yako na kujitoa maisha yote..lakini unayempenda wewe haoni tabu kukuumiza na kukuliza kwa kujua unampenda na huwez kumuacha.

Yamenikuta ndo maana nawashauri wote,oleweni na wanaume wanaowapenda sio mnaowapenda nyinyi.
 
Umeongea ukweli mtupu.afadhali umesanuka mapema
 
Nilishasema sema hapa kuwa usimpende mpenzi wako kwa asilimia zaidi ya 100 watu hawakuelewa mantiki yake, lakini nashukuru umenisaidia, Mpende mtu kwa asilimia 50tu, hizo hamsini ziache coz lolote laweza tokea here between! lakini wewe mtimizie kila kitu chake anachotaka but inakuwa ni siri yako.

CC: miss chagga, ever,

na CC: Data.
 
Duh! Sasa unatuingiza kwenye majanga wanaume. Niliwahi mpenda Dada mmoja kwa asilimia Zote, alichonitenda mpaka leo huwa nalipiza kwa wengine! Sijui kama kuna atakayetokea na kunifanya niwe na tabia kama ya mwanzo.!!
 
Mimi hapa LOL
 
kweli
ila napo ni ngumu..unaolewa na mtu moyo wako uko kwa mwingine
kazi sana
 
ki ukweli wanaume ukimpenda anakutesa sana ... sijuiwanaume hwapendi kupendwa huwa nawaza sana haya makitu sijui yana nini?
 
Wasichana wengi wanakutana na madhira hayo sababu juu moja!! Wale wanaowapenda kwa dhati hawawafati kwa sababu ya kipato sasa siku mtakapo acha kujali maslahi ya pesa na gari na kujali na kuthamini penzi vilio vyenu vitapungua
 
ki ukweli wanaume ukimpenda anakutesa sana ... sijuiwanaume hwapendi kupendwa huwa nawaza sana haya makitu sijui yana nini?

kwan nyinyi mnapenda?? Nani kasema?? Nyinyi mnapenda pesa na gari ndio maana hata mwanaume anakuwa toa kitu weka kitu......... Tutafika tu.
 
Nilishasema sema hapa kuwa usimpende mpenzi wako kwa asilimia zaidi ya 100 watu hawakuelewa mantiki yake, lakini nashukuru umenisaidia, Mpende mtu kwa asilimia 50tu, hizo hamsini ziache coz lolote laweza tokea here between! lakini wewe mtimizie kila kitu chake anachotaka but inakuwa ni siri yako.

CC: miss chagga, ever,

na CC: Data.

hivi hiyo kumpenda mtu kwa asilimia unajuaje kama umefikia hizo asilimia? unajuaje kama zimezidi? vipimo gani vitakuonesha kuwa sasa nampenda mpenzi wangu asilimia 50?
 
Usiombe ukutane na visa vya mwanamke asiyekupenda hata chembe....unaweza ukajiona mavi

kabisa shemeji, yaani hutokuwa na thamani mbele yake. hakuna mazuri atayoweza kukufanyia, lazma ujiandae kukabiliana na dharau za kutosha.
 
kwan nyinyi mnapenda?? Nani kasema?? Nyinyi mnapenda pesa na gari ndio maana hata mwanaume anakuwa toa kitu weka kitu......... Tutafika tu.

nyie vinega mnamatatizo sana mkipendwa mnakuwa mwiba loh!!!!!! na siye tunapunguzia maumivu kwenye wallet zenu
 
Mie ndoa kupenda au kupendwa ni swala la mwisho katika vigezo. Faida ya kuolewa na mtu unayempenda ni kwamba utakuwa na uwezo wa kumsamehe. Haugarantee mbingu duniani.
 
Back
Top Bottom